East
JF-Expert Member
- May 9, 2022
- 603
- 1,722
Utangulizi
Natumauni ni mzima wa afya, leo nitagusia baadhi ya kozi zinazohusiana na masuala ya teknolojia. Katika karne hii inakupasa ufahamu baadhi ya vitu ili uweze kuelewa tupo wapi na tunaelekea wapi. Pia kujifunza teknolojia itakusaidia kuelewa na kutatua matatizo madogo na hata makubwa mimi mwenyewe ni moja ya watu ambao napenda kujifunza na imenisaidia sana na baadhi ya watu hudhani nimesoma IT kumbe sivyo. Hivyo, nawe usisite kujifunza leo bila kujali eneo ulilopo. Utumiaji wa kiingereza utahusika ili nisiharibu maana husika au kukuchanganya na kushindwa hata jinsi ya kuzitafuta.
(Picha kutoka mtandaoni).
Unaanzaje ?.
Maamuzi yapo mkononi mwako na vitu vya kuzingatia katika kujifunza ni kama ifuatavyo :
1. Fanya tafiti ya kozi husika.
2. Tafuta rasilimali husika za kujifunzia, kwa mfano udacity kuna rasilimali za kutosha kujifunza.
3. Pangilia muda wako vizuri kabisa ili upate muda wa kutosha kujifunza.
4. Anza kujifunza bila kuchelewa.
5. Usiogope kuuliza na kuomba msaada endapo ukipatwa na changamoto.
6. Shiriki kazi zako kwa wenzako. Mfano Github
Tovuti ambazo zitakupa rasilimali bure ila kuna baadhi ni za kulipia.
Baadhi ya tovuti hizo ni Kama vile W3school,Udemly,Udacity,Edx,FreeCodeCamp,Cloud Academy,Coursera,Alison,Cybrary,DataCamp, Harvard Online Learning na Egghesd.
Baadhi ya kozi au teknolojia bora kwa sasa na baadae.
Baadhi ya teknolojia hizo ni kama ifuatavyo :
1. Artificial intelligence na Machine Learning.
(Picha kutoka mtandaoni).
2. Data science (sayansi ya data).
(Picha kutoka mtandaoni).
3. Digital marketing (soko la kidijitali).
(Picha kutoka mtandaoni).
4. Cloud computing (Huduma za utunzaji data).
(Picha kutoka mtandaoni).
5. Deep Learning.
(Picha kutoka mtandaoni).
6. Big data.
(Picha kutoka mtandaoni).
7. Animation (uhuishaji).
(Picha kutoka mtandaoni).
8. DevOps.
(Picha kutoka mtandaoni).
9. Blockchain.
(Picha kutoka mtandaoni).
10. Cyber security (Usalama wa mtandao).
(Picha kutoka mtandaoni).
Tunajifunzaje ?.
Graphics design (Michoro ya kubuni). katika kujifunza kubuni vitu mbalimbali kama vile picha, kalenda na mabango yakupasa ufanye yafuatayo :
1. Soma kanuni za ubunifu zitakazo kuongoza kwenye uchoraji.
2. Jifunze program ya uchoraji, mfano inkscape na hata programu za Adobe kama Photoshop. Upande wa watumiaji wa simu kuna photo studio, canva, snoppa na baadhi ya programu za Adobe.
3. Baada ya hapo anza kutengeneza kazi mbalimbali iwe bure au kwa malipo ili kujiimarisha zaidi.
(Picha kutoka mtandaoni).
Programming language (lugha za kutengeneza programu) kufahamu lugha yoyote inakupa uelewa zaidi ya namna mifumo mbalimbali inavyofanya kazi, mfano wa lugha hizo ni C, C++, C#, Python, Swift, Go, Java na Kotlin. Hatua za kufuata ni
1. Chagua lugha moja kwa wanaoanza Python ni bora zaidi na rahisi.
2. Tambua programu inayokubalika kwa lugha husika. Mfano upande wa Python unaweza tumia pycharm na watumiaji wa simu kuna pydroid playstore.
3. Anza kujifunza misingi ya lugha husika.
(Picha kutoka mtandaoni).
Utengenezaji wa tovuti (Web design and development) Uwepo wa tovuti ni muhimu na upatikana kwa kubuniwa kwa kutumia html, css na JavaScript kwa upande wa muonekano ili mtumiaji aweze kuelewa. Upande wa utunzaji data unaweza jifunza PHP, Python au Node.js. Programu za kujifunzia ni notepad, sololearn, Acode na Dcode. Unaweza pia jifunza kupitia WordPress na wix.
(Picha kutoka mtandaoni).
Uundaji wa apps unaweza unda kwa mfumo wa android au IOS. Najifunzaje ?
1. Chagua lugha ya kutengeneza app, Java au Kotlin upande wa android au swif na objective-c upande wa IOS (Apple).
2. Jifunze misingi ya lugha husika.
3. Jifunze programu za kutengeneza apps, mfano Android studio.
4. Anza kutengeneza apps.
(Picha kutoka mtandaoni).
Hifadhi data (database) hii ni kama ubongo katika utunzaji wa data mbalimbali kama kumbu kumbu kwa baadae. Hatua za kuanza kujifunza ni Kama ifuatavyo :
1. Jifunze lugha za database kama vile sql, oql na xquery.
(Picha kutoka mtandaoni).
2. Baada ya hapo jifunze mifumo yake kama vile mysql, casandra, oracle, Microsoft access na Microsoft sql. Chagua moja tu inatosha. Pia unaweza jifunza kwa njia ya simu kupitia tivuti Kama W3school na LearnSql.com upande wa app kuna SQLite database editor.
Cloud computing teknolojia hii inahusika na utoaji huduma za kuhifadhi rasilimali mbalimbali ambazo unaweza kuzipata muda wowote na mahali popote. Hapa rasilimali zako utatunzuwa na sio kutunza wewe. Je , utaisomaje ?
1. Elewa misingi ya cloud computing, mifano ya misingi hiyo ni ulinzi wa talakishi, misingi ya mifumo endeshi (Linux, window) na miundo yake.
2. Fahamu hata lugha moja ya kutengeneza programu, mfano Go, pyyhon au java.
3. Jifunze baadhi ya majukwaa, mfano AWS (Amazon Web Service), Azure, GCP(Google Cloud Platform).
4. Chagua eneo moja na ujikite zaidi, mfano upande wa ulinzi au uhifadhi rasilimali.
(Picha kutoka mtandaoni).
Usalama wa mtandao (cyber security) ni teknolojia inayohusika na ulinzi wa mitandao, mifumo, programu dhidi ya mashambulizi ambayo hufanywa na wadukuzi. Ni moja ya kozi nzuri kujifunza, tunajifunzaje ?.
1. Fuzu masomo kwa ngazi yoyote hasa stashahada au shahada ya IT au sayansi ya talakishi (computer science).
2. Tathimini ujuzi wako katika masuala ya utumiaji wa lugha za kutengenezea programu, misingi ya ujuzi wa mtandao mfano computer networking na uwezo wa kutatua changamoto za kidijitali.
3. Jifunze misingi ya usalama wa mtandao (cyber security).
4. Hakikisha unapata cheti, mfano CompTIA, ISC2 au ISACA.
5. Fanya masoezi kadri uwezavyo ili ujiimarishe vizuri.
(Picha kutoka mtandaoni).
Mwisho kuna mengi zaidi ya kushiriki nanyi itoshe kusema inatosha kwa leo sababu ya ukomo wa maneno. Mimi si muelewa zaidi ya masuala ya teknolojia na nimejaribu ninachoweza. Karibuni kwa maoni, ushauri na hata kuchangia mada hii na uweze kupata mawili matatu.

Upvote
10