robert_k
Member
- Sep 27, 2019
- 42
- 19
Leo kwenye pita pita zangu mtandaoni, nikakutana na habari ya tajiri mmja wa marekani aitwae Marc Randolph. Huyu ni muasisi wa kampuni wa Netflix, kwa wale wapenzi wa movies na series mnaijua vizuri sana
Anasema wakati akiwa amemaliza college akiwa na miaka 21, baba yake alimpa karatasi ambalo aliandika kwa mkono wake sheria 8 za mafanikio. Sheria hizo ambazo hadi sasa akiwa na miaka 61 bado anazo nyuma ya kioo chake cha bafuni. Na copy zingine kawapa watoto wake. Unaweza kuona jinsi gani wenzetu wanadhamini ushauri wa wazazi wao hadi wajukuu kwa wajukuu wanakua wakiisoma waraka wa ushauri wa babu juu ya mafanikio
Anasema sheria hizo za mafanikio hazikumfanya tu kuwa tajiri ghafla ila alipitia mlolongo mrefu. Akiwa na miaka 23 alianza kazi, alikuwa anafanya kazi kampuni ya kupangisha nyumba ya mama yake. Kwa miezi 8 hakufanikiwa kumpangisha mtu yeyote, mwisho wa mwaka alikuwa hajatengeneza hata shilingi katika mauzo hivyo ikamlazimu apange yeye mwenywe apartment mmja
Maisha yakaenda, akapata kazi katika kampuni ndogo sana ya mziki kama mkurugenzi. Kazi ambayo pia alipitia changamoto nyingi, ikambidi afanye kazi ya ziada ya kusoma kila siku mambo ambayo yanamfanya mtu kuwa mkurugenzi bora. Alisoma kuanzia sa 3 hadi sa 5 asubuhi mkurugenzi anatakiwa afanye nini, baada ya sa 5 hadi anavyoondoka anabidi afanye nini, pia alisoma uhusiano wa mkurugenzi na wafanyakazi na mambo mengi. Jambo ambalo lilimjenga hadi akiwa na miaka 39 akaanzisha Netflix sasa ambayo aliiongoza hadi 2003
Jambo muhimu katika hadithi hii, tusipuue ushauri wa wazazi. Tunaona hadi wenzetu wanaandika. Bwana Marc hakuachiwa mali wala fedha aliachowa kikaratasi tu cha sheria za mafanikio 8. Ila hiyo karatasi ikampelekea kupata utajiri. Pia ushauri na jitihada zinazaa mafanikio. Palipo jitihada na Mungu anaweka baraka zake
Nawatakia mafanikio mema katika kazi yeyote unayofanya. Usikate tamaa, changamoto zipo ila kumbuka palipo jitihada kuna baraka za Mungu pia. Sheria hizo 8 za mafanikio nimeambatanisha chini ili msome au mkiweza nenda google andika Marc Randolph utapata hadithi yake