Tujikumbushe aliyekuwa Waziri wa Afya, Dr Gwajima akiwabana watumishi wazembe

Kuna kipindi niliwahi kusikia aidha akijiita ama akiitwa "Field Mashall" wakati akiwabananisha watumishi wazembe na wababaishaji akiwa Wizara ya Afya na akawaeleza kuwa hawawezi kumdanganya kitu kwakuwa amekulia humo kiutendaji kwahiyo anaijua Wizara 'nje-ndani'. Hakika she desrve hiyo tittle.
Ni aina ya Viongozi wachache sana wanaoitendea haki kodi ya Wananchi na anakula mshahara anaoufanyia kazi ipasavyo.
Najaribu kuvuta picha vile nchi itachangamka kiutendaji na nidhamu ya watumishi kurejea kwa viwango vya juu pale atakapokabidhiwa kuwa Waziri Mkuu wa JMT na akaruhusiwa na mamlaka ya uteuzi kufanya kazi zake bila kuathiriwa na fitina za kisiasa, hakika nchi itanyooka sana.
Ni moja ya hazina za kutunza sana na anaweza kutumika kama karata ya turufu pale wakati unaofaa utakapofika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…