Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun

Kweli,waliona mbali sana na pamba zao "gangwe gear" nadhani walikuwa wanasimamiwa na Sebastian Maganga
Yaah! ni kweli Mkuu Seba ndio alikia na mkono wake pale na dili la kusaini ule mkataba Inspector alipiga pesa ndefu sana kwa miaka ile, ilikua ni Milioni moja ya Kitanzania. Sidhani kama kuna msanii aliewahi kupiga dili kubwa kama lile kwakipindi kile
 
Ya kwanza alifanya Nature na KR ikafanya vizuri kiasi, ilipoachiwa Remix ya Inspecta ile OG ikasahaulika kabisa. Ukisikia tu OHoo HOoo... (Sauti ya Inspekta[emoji16]) unajua nini kinafuatia.
Kundi lilikuwa linaitwa "wachuja nafaka" hapo unampata Doro,KR Mura na Nature
 
Hahah!! [emoji119][emoji119]

Watoto wa Temeke hawakua wanastahili kuingia kwenye yale mashindano ila kama Nature angeingia labda angeshinda kwa ifluence ya mashabiki tu...

Mashindano yenyewe kipindi kashinda Afande yaliingia dosari maana wasanii kama Sollo walilalamika sana kua kuna namna imefanyika nakumbuka alitoa hadi ngoma akiongelea hilo swala ililua inaitwa 'kilio changu' kama sikosei
 
Sema nini vingine walikuwa wanatudanganya kwavile wabongo tulikuwa hatuvijui, kuna mistari Inspekta anawema sasa wanapatikana kwenye tovuti 'wwgangwemobb.m', hapo tulikuwa hatuelewi kitu zaidi ya kuwapa respect tu[emoji16][emoji16]
 
Yap alimshirikisha Q Chief, Solo aliumia sana naona ndo akaamua na kulitosa game la bongo na kukimbilia mbele
 
Pia ikumbukwe 'Nje ndani' ilikua album bora ya mwaka 2004 katika tuzo za Tanzania Music Awards ambayo baadae ndio ikawa Kili Music Awards...
 
Title ilitakiwa kutaja jina la juma nature na sio inspectah,mawazo tu.
 
Jose mtambo kaanza kabra ya wote uliowataja apo.
 
Kuna nyimbo moja ya kibabe sana inaitwa "bunda siliga"
japo nimeisahau kidogo.

Chorus:
Bunda siliga kiatu mtu
Hima saka mpira usijitusu
Huu thubutuu
Umo ndani kashilikiswa ommy g luteni wakati anaingiza verse alichemka kama mara kumi ivi adi mastar j akamtaka aje kuludia siku nyingine kwa sababu tulikuwa tunawai kwenye lieso ya summer jum mwaka 2001 ambayo siku izi ndo inaitwa fiesta
 
Mbukwa Tai.
Bye bye
Mtoto wa uswazi.
Nje ndani
Kisa cha baba mkwe.
Vidonge vyao
-------------------
Usafiri choki ndani ya RVR hahahahaa
 
Pengine aliamini ye ndo mkali kuliko wote. Sema binafsi nilikuwa namkubali Solo kuliko Afande
Mimi nilikua mdogo sana nilitekwa na upepo wa darubini ila nilivyopata upeo wa kupambanua mambo nikaona Prof. alistahili kupata ule ushindi...
 
Umo ndani kashilikiswa ommy g luteni wakati anaingiza verse alichemka kama mara kumi ivi adi mastar j akamtaka aje kuludia siku nyingine kwa sababu tulikuwa tunawai kwenye lieso ya summer jum mwaka 2001 ambayo siku izi ndo inaitwa fiesta
"makerere,
Makerere shule aliyosoma Nyerere"

Bunda siliga,kiatu mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…