Tujikumbushe hawa watangazaji wa redio free RFA

Namba 17 amefariki leo

Steve Moyo Mchongi
 
Redio free wakikuwa na ushirikiano na DW ndio maana redio yao ilikuwa inatamba sana. Na hata watangzaji wake ulikuwa unaweza kuwasikia wiki 2, dw wiki 2 rfa.

Sasa hivi limebaki gofu tu pale.
 
Nimepiga hesabu kati ya watangazaji wote hapo 9 wameshafariki sawa na 14.06. Siku za kuishi ni chache sana.
 
Sahara Ni Sehemu Nzuri sana upande wa Practical na experience wako vizuri
 
RFA ilikuwa na vipindi vizuri na vilivyopangika sambamba na watangazaji waliokuwa wakitangaza vipindi vyao kwa weledi mkubwa. Kila msikilizaji alipata kipindi chakd na hakika alikifurahia.

Walikuwa na coverage kubwa sana nchi hii kwani walisikika sehemu nyingi ambazo redio nyingine hazikufika. Sijui nini kilitokea mpaka asilimia kubwa ya watangazaji kuondoka. Ila walipata attention yetu kwa kweli.

Nimeusoma uzi wote hakika nimekumbuka mbali.

1. Sindano 5 za moto
2 Sitasahau
3. Uliza ujibiwe
4. Showtime
5. Weekend Fever
6. Mambo mambo
7. Je, huu ni uungwana
8. Ushauri wako
9. Uliza Ujibiwe
10. RFA Bonanza
11. Hakuna kulala
12. Masimulizi ya kihindi Jumapili
13. Search Line
14. Kile kipindi cha makabila
15. Je, wajua ?
16.


Hakika vizuri havidumu.
 

Hakuna Kulala aka usiku wa Millenium na Faustine Stephano ,Jazila Mshana
 
asante sana kwa kumbukizi nzuri mheshimiwa..ulikuwa ni wakati mzuri sana
 
Kuna Radio ipo Kenya ime copy almost vipindi vyote vya RFA inaitwa Radio Jambo
 
RFA bado ipo ipo vizuri. Sema wameanza kuiga mambo ya promosheni za pesa sijui ushinde pesa n.k. Ila bado naikubali sana vipindi vyake, hususani Jumapili saa 11 asbh hadi saa 7 mchana
J2 wana vipindi vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…