Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hata hivyo, tarehe 14 Novemba, 1968, Baraza la EAMWS la Tanzania liliitisha mkutano wajumbe kutoa mikoa yote ya Tanzania kujadili ‘’mgogoro.’’
Pamoja na waliohudhuria ni wajumbe kutoka mikoa ambayo tayari ilikuwa imekwishajitenga na EAMWS.
Mkutano huu ulifanyika katika shule ya Kiislam ya Kinondoni.
Hapajatokea katika historia ya Uislam Tanzania mkutano kama ule.
Uongozi ulikuwa unaingia katika chumba cha mkutano tayari umeshajeruhiwa vibaya sana na propaganda za magazeti ya TANU na radio ya serikali.
Katika moja ya shutuma ambazo zilikuwa zikiandama uongozi wa EAMWS ilikuwa ni matumizi mabaya ya fedha za jumuiya.
Akifungua mkutano ule Tewa aliwatahadharisha wajumbe kuwa makini katika lolote watakaloamua kwa kuwa endapo wajumbe watashindwa kuafikiana basi matokeo yake ni kuvunjika kwa EAMWS, umoja wa Waislam na mwisho ya miradi yote ya elimu pamoja na ujenzi wa Chuo Kikuu.
Hisia kali zilitawala mkutano huu na baadhi ya wajumbe wanawake walikuwa wakilia hasa pale baadhi ya wajumbe walipokuwa wakitoa michango yao katika mjadala walipokuwa wakisoma aya za Qurían Tukufu na kueleza fadhila za kupigana jihad dhidi ya madhalimu na wanafiki.
Hisia hizi kali zilitokana na ukweli kuwa wajumbe walikuwa wanafahamu kuwa wale wenzao waliokuwa wakidai kujitenga walikuwa wakitumikia Ibilis tu na wala msimamo waliokuwanao haukuwa wao wala hawakuwa wanayafanya yale kwa mapenzi ya Allah na Mtume wake.
Mwenyekiti wa mkutano Tewa Said Tewa aliahirisha mkutano hadi siku ya pili ili wajumbe wapoe na watoe mchango wakiwa katika hali ya utulivu.
Katika wajumbe ambao walisimama kidete kutetea umoja wa Waislam walikuwa Sheikh Issa Mchowera kutoka Mtwara, Bilali Rehani Waikela, Hassan Johari na Sheikh Abdallah Said kutoka Kigoma.
Mkutano uliamua kuunda Tume ya Uchunguzi ya watu saba kuchunguza chanzo cha ‘’mgogoro’’ na kisha itoe taarifa.
Mussa Kwikima kijana mwanasheria alichaguliwa kuwa katibu wa tume ile ya uchunguzi.
Wakati huo mikoa tisa ilikuwa tayari imeshajitenga na EAMWS na magazeti ya TANU yakawa tayari yamejenga ‘’mgogoro’’ ule kufikia hali ya kuonekana kuwa ni ‘’mgogoro’’ wa taifa zima ambao kila mtu anaweza kuuingilia na kusema atakalo.
Magazeti ya TANU yakawa yanaandika na kuchapisha mambo ya EAMWS kama wanavyotaka, wakizidi kutia chumvi katika ugomvi ambao tayari ulikuwa umeshaleta hofu na farka kubwa katika jamii.