Tujikumbushe kidogo Misingi ya Uhasibu:

Tujikumbushe kidogo Misingi ya Uhasibu:

Joined
Apr 10, 2017
Posts
25
Reaction score
18
Misingi mitano ya taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi.
1.Uadilifu (Integrity)
- Mhasibu unatakiwa kuwa muwazi na muaminifu katika maswala ya taaluma na vinavyohusiana na kazi

2.Usawa (Objectivity)- Mhasibu usiruhusu kitu chochote , upendeleo au utashi wako ukahasili kufanya maamuzi yanayohusiana na utendaji wako wa kazi

3.Uhodari na Ustadi (Professional Competence and Due Care )
- Mhasibu unatakiwa kuongeza ujuzi wa taaluma na kujisomea sheria na taratibu ili kuendana na Mabadiliko yanayotokea kila siku katika taaluma na utandawazi.

4. Usiri (Confidentiality )- Mhasibu unatakiwa kuwa msiri kuhusiana na taarifa za biashara au chochote cha mteja kwa mtu mwingine (Third parties) isipokuwa kwa matakwa ya sheria au chombo kinachohusika .

5.Tabia na Mwenendo (Professional Behavior )- Mhasibu unatakiwa kuwa na mwenendo na tabia nzuri katika mazingira yoyote yale hata kama hakiusiani na kazi.
 
Attachments

karibu kuongezea na kuchangia kitu ambacho kitatuwezesha kusonga mbele kwenye taalumu ya uhasibu na ukaguzi
 
Kuna mtu hapa anasema yeye anapenda kucheza na petty cash,kuandaa payroll,salaries&wages ,kuidhinisha&kufanya malipo mbalimbali kasema usimuulize kwa nini
 
Hivi, kwanini tunasema "Kilimo cha kufa NA kupona" na siyo " Kilimo cha kufa AU kupona" au " Profit AND loss" na siyo "Profit OR loss". Kwamba hivi vitu vinatokea pamoja!
 
Hivi, kwanini tunasema "Kilimo cha kufa NA kupona" na siyo " Kilimo cha kufa AU kupona" au " Profit AND loss" na siyo "Profit OR loss". Kwamba hivi vitu vinatokea pamoja!
Hahaha.

Umenimumbusha album moja ya Peter Tosh inaitwa "Wanted Dead And Alive" yani siyo "Dead OR Alive" ni "Dead AND Alive".

Inabidi wamkamate akiwa katika process ya kufa wakati huo huo yupo dead and alive, some Schrodinger Cat experiment type of quantum state.
 
Ngoja nikujibu kitaaluma zaidi.
Unaona bana, kihasibu kuna 'statement' moja hv inaitwa 'Income Statement' imezoeleka zaidi kama 'Profit and Loss Account'

Sasa mzee bana hadi ku ascertain profit ama loss kuna sehemu kuu zinapitiwa.

Kabla ya Net loss ama Net profit kunatangulia Gross losa ama Gross profit.

Sasa mzee baba, unaweza ukawa na Gross profit lakini ikaleta Net loss mwisho wa hesabu, and vice versa. Unasikia eeehhh.

Ila sasa statement ama account ni MOJA, ndio maana wanaita Profit and Loss na wala sio Profit or Loss.

Daka hio itakusaidia kijiweni kwako!

Hivi, kwanini tunasema "Kilimo cha kufa NA kupona" na siyo " Kilimo cha kufa AU kupona" au " Profit AND loss" na siyo "Profit OR loss". Kwamba hivi vitu vinatokea pamoja!
 
Hivi, kwanini tunasema "Kilimo cha kufa NA kupona" na siyo " Kilimo cha kufa AU kupona" au " Profit AND loss" na siyo "Profit OR loss". Kwamba hivi vitu vinatokea pamoja!
Tuje sasa katika kilimo cha kufa na kupona. Eeehhh.

Iko hv: Kwanza, mantiki ama dhumuni zima la hiki ni nini? Ni kuhamasishana tu nothing else.

Sasa, mzee baba eeehh ukisema Kilimo cha kufa au kupona tafsiri yake ni kwamba ama ufe ama upone ila kilimo kisonge mbele. Eeehh mzee baba hapo kuna ubinadamu kweli? Hakuna. Like you burnt the bridge! Hahahahaha

Hivyo, kiuweledi huwezi kusema hivyo mzee baba, maana italeta tafsiri yenye ukakasi.

Nimefurahi sana kupata maswali kama haya. I can see una akili kubwa sana. Atukuzwe Mungu aliyekuumba.
 
  • Thanks
Reactions: bbc
wazee wa CPA hours wekeni mabadiliko yoyote ya ghafla ya "standard" za uhasibu
Uhasibu haina something special and new ya kuleta kwenye society (kwa mtazamo wangu). Nachoona IT iwe integrated na uhasibu ndio itaenda extra level. Now ibaki hv hakina jipya
 
Uhasibu haina something special and new ya kuleta kwenye society (kwa mtazamo wangu). Nachoona IT iwe integrated na uhasibu ndio itaenda extra level. Now ibaki hv hakina jipya
mbona ipo integrated na IT,au sijui maana ya IT
hizi accounting packages sio moja ya integration?
 
Naomba tuendelee kuchangia ni vitu gani vinavyochangia au kutishia kuenenda na misingi ya Uhasibu na Ukaguzi na namna ya kuepukana navyo
 
Back
Top Bottom