Tujikumbushe majina maarufu ya utani ya baadhi ya wachezaji wa zamani

Ni goalkeeper! Pia alidakia RELI Morogoro!
Unachanganya dancun mwamba aliyekuwa nyanda wa wagosi wa kaya na dancun butinini mshambuliaji wa reli ya moro ambae ukoo wao wa kimichezo alikuwa na dada yake jeni butinini hodari sana wa mpira wa pete mpaka akaimbwa na tancut almasi waqt umekwenda wapi!
 
Sijachanganya Mkuu. DUNCAN MWAMBA na DUNCAN BUTININI wote wamechezea RELI Morogoro kwa wakati mmoja! DUNCAN BUTININI alikuwa WINGER - anakimbia VIWIKO JUU, Mabeki walipata tabu sana kumkaba! BUTININI alicheza RELI sambamba na Baba Mkubwa wa Kelvin Yondan (Mbuyi Yondan)

DUNCAN MWAMBA alidakia RELI akiwa goalkeeper namba 2 baada ya ATHUMAN MSOMALI (kwa sasa ni staff YONO AUCTION)

Mabeki wa RELI walikuwa Bakari Tutu, Gaspar Lupindo, Mohammed Mtono, Madundo Mtambo (Prof. SUA), Fikiri Mohammed Magoso na Habib Kondo!

Sad story ni kwamba BUTININI alishafariki!

 
Duncan mwamba alikua kipa namba mmoja wa African Sports ya Tanga, Jamaa akiwa uwanjani anavaa tracksuit full juu anavaa kapelo, alikua na mbwembwe na ata Peter Manyika alivyokua Yanga nadhani uvaaji wake na mbwembwe zake alikua kakopi kwa Duncan Mwamba. Sina uhakika kama baadae alichezea reli. Maana Duncan kadaka Sports miaka ya mwishoni mwa 80 na Reli imepanda manzoni mwa miaka ya 90.
 
Alidakia timu zote 2! alianzia AFRICAN SPORTS kisha RELI!
 
Athman msumali nyanda mrefu maji ya kunde mbavu zilikuwa za mkali abdallah na mohamed mtono chembamba hivi hapo kati kama ulivyosema huko mbele ndo akina njohole na hamad said masenga mbui na david mihambo ali malilo aah waqt umekwenda wapi?
 
Leo nimekutana na ALLY MALILO "loketo"

Hakika nimefurahi sana na tumekumbushana mengi ua miaka ya mwanzoni ya 90......

LONG LIVE BONGO SOKA
 
Fred Katarahiya Minziro "Majeshi" - Baba Isaya.
 
Fred Katarahiya Minziro "Majeshi" - Baba Isaya.
 

Wakati ni ukuta, asilimia kubwa hawa nimewashuhudia live!! Sahau Kambi hakuwa na nick name??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…