Baba na mama salamau, nyumbani nawatumia
Siwezi kupiga simu, nipo mbali na dunia
Bila shaka mwafahamu, jela ninatumikia
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe
Hiiii shairi naitafuta sana!!! Natamani niipate tena niirudie!! Hakika kazi ilkuwa nzurii sana...
Baba na mama salamu, nyumbani nawatumia,
Siwezi kupiga simu, nipo mbali na dunia,
Bila shaka mwafahamu, jela ninatumikia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Vipi hapa nimefika, bila shaka mnajua,
Nitakaa kwa miaka, gereza likinilea,
Tayari nimeshachoka, tabu zinanisumbua,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Nilipofika mjini, nadhani nilikosea,
Nikaingia kundini, watu nisiowajua,
Wakanikalisha chini, elimu kunipatia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Tukaingia sokoni, wakaniongoza njia,
Nikaenda kwa imani, wao watashambulia,
Nikiwekwa hatarini, wao watasaidia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Hatua nikahesabu, mbili tatu nikafika,
Fedha bila kuhesabu, haraka nikanyakua,
Mambo yaliponisibu, wenzangu wakakimbia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Meno saba yalinitoka, pale bila kukawia,
Kwa hakimu nikafika, shitaka kanisomea,
Hatimaye katamka, jela nitatumikia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
Haikimbii misimu, jela ukitumikia,
Naishi kama sanamu, sina la kufurahia,
Najihisi marehemu, kucha kutwa ninalia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe,
Ndugu nisalimieni, wote mnaowalea,
Karamu andalieni, nyumbani nikirejea,
Sheria ziheshimuni, mimi nimeshuhudia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.