Tujikumbushe Mashairi tuliyoyapenda shule ya msingi

Baba na mama salamau, nyumbani nawatumia
Siwezi kupiga simu, nipo mbali na dunia
Bila shaka mwafahamu, jela ninatumikia
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe




Hiiii shairi naitafuta sana!!! Natamani niipate tena niirudie!! Hakika kazi ilkuwa nzurii sana...
 
Hakika fasihi simulizi hutunza amali za jamii, tuwatengenezee watoto wetu misingi ya kupenda kujisomea vitabu itakua na manufaa maishani mwao.
 
Nitafanya kazi Gani nikimaliza kusoma,hili lilikuwa shairi Bomba Sanaa na mashuhuri mno
 
Baba na rafiki zake, walikwenda kutembea
Wakafika kwa Mnyake, hodi wakamgomgea
Wakapata jibu lake, karibu ndani ingia
Watu wale ni wangapi, viti vile vingapi?

Wakakaribishwa viti, ukumbini kuongea
Wakajaribu kuketi, nao hawakuenea
Rafiki yao Japhet, hakupata pa kukaa
Watu wale ni wangapi, viti vile ni vingapi?

Wakaona afadhali, wakae wawiliwili
Kila kiti kuchangia, kwa hii njia ya pili
Kiti kimoja kikabakia
Watu wale ni wangapi, na viti vile vingapi?
 
Baba na mama salamu, nyumbani nawatumia,
Siwezi kupiga simu, nipo mbali na dunia,
Bila shaka mwafahamu, jela ninatumikia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Vipi hapa nimefika, bila shaka mnajua,
Nitakaa kwa miaka, gereza likinilea,
Tayari nimeshachoka, tabu zinanisumbua,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Nilipofika mjini, nadhani nilikosea,
Nikaingia kundini, watu nisiowajua,
Wakanikalisha chini, elimu kunipatia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Tukaingia sokoni, wakaniongoza njia,
Nikaenda kwa imani, wao watashambulia,
Nikiwekwa hatarini, wao watasaidia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Hatua nikahesabu, mbili tatu nikafika,
Fedha bila kuhesabu, haraka nikanyakua,
Mambo yaliponisibu, wenzangu wakakimbia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Meno saba yalinitoka, pale bila kukawia,
Kwa hakimu nikafika, shitaka kanisomea,
Hatimaye katamka, jela nitatumikia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.

Haikimbii misimu, jela ukitumikia,
Naishi kama sanamu, sina la kufurahia,
Najihisi marehemu, kucha kutwa ninalia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe,

Ndugu nisalimieni, wote mnaowalea,
Karamu andalieni, nyumbani nikirejea,
Sheria ziheshimuni, mimi nimeshuhudia,
Sina wa kumlaumu, niliyataka mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…