Tujikumbushe moja ya matukio ya kusisimua World Cup 1998

Tujikumbushe moja ya matukio ya kusisimua World Cup 1998

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
SHUTI LILIKOKIUKA KANUNI ZA MWENDO ZA KISAYANSI

Kuelekea Kombe la Dunia la 1998, wenyeji Ufaransa waliandaa mashindano maalumu ya kupima maandalizi yao.
Wakati huo Kombe la Mabara lilikuwa halijaanza kutumika kupima maandalizi ya Kombe la Dunia. Lilikuja kuanza 2001.

Mashindano hayo yaliyoitwa Tournoi de France yalifanyika 1997 na kushirikisha timu 4; wenyeji Ufaransa, Brazil, England na Italia.

Mechi zilichezwa kwa mtindo wa ligi, kwamba mwenye pointi nyingi ndiyo bingwa. England wakawa Mabingwa.

Mechi ya ufunguzi ilifanyika Juni 3, 1997 dimbani Stade de Gerland mjini Lyon, na kuwakutanisha wenyeji na Brazil.

Ni kupitia mchezo huu uliomalizika kwa sare ya 1-1, ndipo Roberto Carlos alifunga bao la mkwaju wa adhabu ndogo, linalosemekana kukiuka kanuni za mwendo za kisayansi na hadi sasa wanasayansi duniani bado wanaendelea na utafiti kujua mpira uliwezaje kwenda kama ulivyoenda.

Wanasayansi wanne wa Ufaransa; Guillaume Dupeux, Anne Le Goff, David Quere na Christophe Clanet wa taasisi ya utafiti wa kisayansi ya Ecole Polytechnique, walifanya utafiti ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la New Journal of Physics la Septemba 2010.

Wanasayansi hawa walifanya uchambuzi wa majaribio kadhaa ya kimaabara yaliyozaa mlinganyo unaofafanua mwendo wa mpira na nguvu zilizokuwemo ndani yake katika muda wa kitendo.

Wakahitimisha kwa kusema endapo hesabu zitapigwa vizuri, katika umbali ule ule na nguvu ile ile ya shuti, mtu yeyote anaweza kurudia na mpira ukaenda vile vile.

Lakini mwanasayansi wa Brazil, Prof. Luis Fernando Fontanari anasema hiyo haiwezekani. "Hali ya wakati wa tukio kama nguvu ya upigaji, kishindo cha makutano ya mguu wa Roberto Carlos na mpira, na umbali hadi golini, vilikuwa vya nadra sana kiasi kwamba tunaweza kuita miujiza", anasema Profesa huyo wa chuo kikuu cha Sao Paulo -- kinachoheshimiwa zaidi Brazil.

Fontanari ni mmoja wa wahariri wa majarida ya "Physics of Life Reviews" na "Theory in Biosciences," ambayo ni miongoni mwa majarida muhimu zaidi ya kisayansi duniani.

Mwanasayansi mwingine kutoka Israel, Erez Garty, alifanya utafiti wake na kuhitimisha kwa kusema alichofanya Roberto Carlos ni mazingaombwe. Kazi yake iko YouTube.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani umenikumbusha Davor suker.Sasa hapo zikaja tokea Big G zina picha za wachezaji. Nakumbuka nilikuwa primary school. Yaani ilikuwa Ronaldo,Zidane.

Duh, kwa jinsi ambavyo huwa unatetea CCM huku ukikandia watu wanaonyanyaswa na serikali nilijua utakuwa ule umri wa miaka 45+.

Inaonekana umeanza uchawi ukiwa mdogo sana.
 
Mimi yale mashindano ndio nilimuona zidane kwa mara ya kwanza.akitawala sehemu ya kiungo kama vile anacheza peke yake..

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima uone vile kwa kuwa alifanywa mchezaji huru dimbani (free key player) kutokana na uimara wa viungo waliomzunguka pale kati.
Kwa namna yeyote ile lazima kiwango chake ungekiona bora sana kama unavyosema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom