SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kejeli dhidi ya mafanikio ya Simba ya zinakuwaga kubwa halafu pale upande wa pili wanapofikia mafaniko hayo au wanapopata changamoto fulani ambayo Simba waliwahi kupitia ndiyo fahamu zinawajia wanasahau yale waliyowahi kubwabwaja.
Msimu uliopita katika mashindano ya Champions League hatua ya awali round ya pili, Simba walikutana na Jwaneng Galaxy ya Botswana. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Botswana, Simba walishinda kwa goli 2-0. Mechi ya marudiano kwa Mkapa, Jwaneng walishinda kwa matokeo ya 3-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-3. Kwa matokeo hayo, Kanuni za CAF zikaitoa Simba katika Champions League akaangukia Kombe la Shirikisho.
Hapo sijagusia matokeo ya msimu wa nyuma yake kati ya Simba vs UD Songo ya Msumbiji ambapo Simba walitolewa kwa matokeo ya jumla ya 1-1. Kanuni za CAF kwa mara nyingine tena zikaitoa Simba katika Champions League.
Sikumbuki kusikia watu wa Yanga kusema Simba wametolewa KIKANUNI. Zaidi zilikuwa ni kejeli mtindo mmoja ikiwemo kusema Kombe la Shirikisho waliloangukia Simba kuwa ni kombe la losers.
Fahamu imekuja kuwajia sasa baada ya hali hiyo kuwakuta wao.