Tujikumbushe Songea Boys {Box 2}

Kwa wale mliokuwa Luhira miaka ya mwanzo ya tisini mtamkumbuka mwalimu mmoja maalufu wa sayansi naomba nisimtaje jina lake mtamjua tu. Yeye alikuwa mwnafunzi wa arts ukikosea anakataa kukupiga. Utamsikia anasema; ' Sikuchapi. Nimekustukia unataka sifa. Nikikuchapa utajisifu kuwa umepigwa na mwalimu mwenye Bachellors of Science with Honour"

Je Mnamkumbuka mwalimu mwingine mwenye kupenda kufuga nywele ndefu. Yeye alikuwa ananunua dagaa duka la jirani na shule anawatafuna wanaisha kabla hajafika nyumbani.

Maharage ya mbinga mnayakumbuka.

Wale mliokuwa mnatoboa usiku kama mimi mliwahi kukutana na vibwengo?

Choo cha milango saba mnakikumbuka. Sharti moja wapo la kuingia ni kwamba unavua nguo zote hadi za ndani na ukitoka unatoka mbio. Hekima yake ni kwamba ukibaki na nguo ile harufu utaishi nayo wingi nzima.

Weekly Reports mnazikumbuka. Sisi ndio zilikuwa zinatusaidia mitaani kuthibitisha kama ni wasomi. Ukiulizwa unajua kingereza unasema ndio. Ukiambuwa useme unaanza " Ministry of Education, Songea Boys Secondary School, the Weekly Report".

Tuanzisheni mtandao wetu wa box mbili
 
Wakati ule utamskia Mwanyigu akitangaza mbele yake basi la kiswele " wakati wale wa Iringa wanapanda, wale wa Dar Es Salaam wanajiandaa. Wakati huo moshi mtupu. Si fegi hizo.
 

Mzee kumbe ulikuwepo?
 
Mlipita box2 but bado cc 2nakomaa. Pola na mayao kama home vile
 


Hili jengo lilikua multipurpose hatariii sana kila kitu lawama,huzuni furaha humohumo ndani nikiwa na maana ya:-
  1. PIN (DISCO) na WATAMSO
  2. MITIHANI
  3. KININGA
  4. MENU Hasa Punga na Nyama ilikua balaa
 
Jamani mmenichekesha sana,,, nakumbuka sisi wa miaka ya 2009-2011 tulifanyaga maandamano mwaka 2009 akaja kusuluhisha vizuri aliekuwa Naibu waziri wa elimu wakati ule MWAMTUMU MAHIZA tulikuwa kama tupo jela hivi ilahuyu mama alipokuja alitufungua mwengi tukaanza kula nyama, ndizi na siku za wali zikaongezeka...Sisi ndio tulifanya Songea Boys ikawa kama Seminary nasikia hii hali bado ipo mpaka sasa,,, kisa simu.. Mh Mwamtumu alipokuja akagawana namba zake za simu ili kama kuna mwalim anawasumbua mnapigia au kumbipu then unampa taarifa sasa walimu wakashitukia iikuwa ukikutwa na simu ujue na wenzako woote watakamatwa tu,, wanaanza kuangalia majina yaliyomo,,, tuliposhtukia kila mtu ikabidi mwenye simu awe na A.K.A ili kuthbiti kukamatwa
 
πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Naikumbuka sana siku ile yule mama alivokuja
 
Maji ya shadufu matamu sana kaka mwendo wa kupampu tu..., siku hizi dogo hawakutani na shida hizo za umeme na zingine
 
Kulikuwa na mboga za majani na zingine za kupima katika kijiko zinauzwa na wana ulokoni.Aisee zilitu save sana siku za maharage yani tulikuwa tunamix na maharage siku zinasonga.Ofcourse ni maisha flani ya kukumbuka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…