Tujikumbushe Songea Boys {Box 2}

Tujikumbushe Songea Boys {Box 2}

Kwa wale mliokuwa Luhira miaka ya mwanzo ya tisini mtamkumbuka mwalimu mmoja maalufu wa sayansi naomba nisimtaje jina lake mtamjua tu. Yeye alikuwa mwnafunzi wa arts ukikosea anakataa kukupiga. Utamsikia anasema; ' Sikuchapi. Nimekustukia unataka sifa. Nikikuchapa utajisifu kuwa umepigwa na mwalimu mwenye Bachellors of Science with Honour"

Je Mnamkumbuka mwalimu mwingine mwenye kupenda kufuga nywele ndefu. Yeye alikuwa ananunua dagaa duka la jirani na shule anawatafuna wanaisha kabla hajafika nyumbani.

Maharage ya mbinga mnayakumbuka.

Wale mliokuwa mnatoboa usiku kama mimi mliwahi kukutana na vibwengo?

Choo cha milango saba mnakikumbuka. Sharti moja wapo la kuingia ni kwamba unavua nguo zote hadi za ndani na ukitoka unatoka mbio. Hekima yake ni kwamba ukibaki na nguo ile harufu utaishi nayo wingi nzima.

Weekly Reports mnazikumbuka. Sisi ndio zilikuwa zinatusaidia mitaani kuthibitisha kama ni wasomi. Ukiulizwa unajua kingereza unasema ndio. Ukiambuwa useme unaanza " Ministry of Education, Songea Boys Secondary School, the Weekly Report".

Tuanzisheni mtandao wetu wa box mbili
 
Wakati ule utamskia Mwanyigu akitangaza mbele yake basi la kiswele " wakati wale wa Iringa wanapanda, wale wa Dar Es Salaam wanajiandaa. Wakati huo moshi mtupu. Si fegi hizo.
 
Duh, Wana JF, nyie mlitutangulia. Bifu lenu na tamso lilisababisha tucheze disco mchana kweupeee.. hiyo ni 1991 -93. Dispensary alikuwepo mzee Kidato...(Clinical officer). Nakumbuka ligi ya mabweni, Azimio tuliibuka mabingwa na kuzawadiwa mbuzi. Vijana wa Tunduru (mawia) walikula mpaka ngozi ya mbuzi. Ukiwa na appointment na tamso lazima utunge ugonjwa mkubwa ili uende hospital ya mkoa ukajihudhurishe.

Duh, jamaa kanikummbusha shamba, nusu ya shamba tulikuwa tunalima marejea, hiyo kazi sikuipenda kabisa.. Nilichokipenda ni soft diet kwa sisi mabingwa wa kufoji.

Kiranja wa starehe alikuwa maarufu kuliko kaka mkuu, hasa kwa upande wa Tamso.

Nakumbuka dogo mmoja (form three) tulimkamata darini usiku akiwa Uchi. Hakujua vijana wa kwa Pinda tulikuwa fiti..

Mzee kumbe ulikuwepo?
 
images (1).jpg

Hili jengo lilikua multipurpose hatariii sana kila kitu lawama,huzuni furaha humohumo ndani nikiwa na maana ya:-
  1. PIN (DISCO) na WATAMSO
  2. MITIHANI
  3. KININGA
  4. MENU Hasa Punga na Nyama ilikua balaa
 
Jamani mmenichekesha sana,,, nakumbuka sisi wa miaka ya 2009-2011 tulifanyaga maandamano mwaka 2009 akaja kusuluhisha vizuri aliekuwa Naibu waziri wa elimu wakati ule MWAMTUMU MAHIZA tulikuwa kama tupo jela hivi ilahuyu mama alipokuja alitufungua mwengi tukaanza kula nyama, ndizi na siku za wali zikaongezeka...Sisi ndio tulifanya Songea Boys ikawa kama Seminary nasikia hii hali bado ipo mpaka sasa,,, kisa simu.. Mh Mwamtumu alipokuja akagawana namba zake za simu ili kama kuna mwalim anawasumbua mnapigia au kumbipu then unampa taarifa sasa walimu wakashitukia iikuwa ukikutwa na simu ujue na wenzako woote watakamatwa tu,, wanaanza kuangalia majina yaliyomo,,, tuliposhtukia kila mtu ikabidi mwenye simu awe na A.K.A ili kuthbiti kukamatwa
 
Naikumbuka sana siku ile yule mama alivokuja
 
Na kumbuka Mabweni ya Urafiki, umoja, maendeleo, ujamaa na muungano!

  • Nakumbuka shida ya umeme iliyokuwa itokea na kulazimika kutumia chemli!

  • Kama mtakumbuka Kuna kisima cha kupampu a.k.a Shadufu! Aisee kilitoa msaada wa kutosha katika kutupa maji ila ndo kuoga watu ilikuwa issue passport kama kawa!

  • Pia kulikuwa na huduma ya mihogo "mayau/mayao au makaba" ya kuchemsha kila asubuhi wakati wa uji "pola" ya kiuzwa na wamama wa vijijini toka Mletele!
  • Nakumbuka library yetu ilivyokuwa imechoka ukiingia utakuta vitabu vya hadithi za Abunuasi na adili na nduguze! Vitabu vya taaluma iliku vya enzi zile za 67! Dah ilikuwa shughuli kama kulikuwa na assignment!
  • Kwa wale wapenzi wa disco mnawakumbuka tamsala/ Tamso "Songea Girls" Mwanangu ilikuwa lazima Uoge na Pafyum!

  • Nakumbuka mitaa ya Ulokoni {vijijini} kulikuwa na mama mmoja maarufu kama binti bull huyo mama dah ni noma kila service unapata chakula na vingine pia!

  • Bila kusahau Kuchunga Ng'ombe wa shule na kulima mashamba ya shule dah ilikuwa kazi kwelikweli kwa sisi watoto wa ocean road jembe hatukuwahi kulishika zaidi ya kusomakwenye vitabu!
  • Namkumbuka mwl. mmoja muhohela vijana walikuwa awakimwita maps da alikuwa ni noma ni zaidi ya Feudal wa Tosa Huyu alikuwa capability ya ajabu ya kukutambua akiwa umempa mgongo kisha ukiwa na bifu naye duu utajuta!
  • Bila kusahau umbali uliopo toka mjini hadi shule {4KM} lakini dah wazee tulikuwa tunachapa kwa mguu unaweza kwenda na kurudi mara mbili au zaidi! Lakini leo tunapanda gari fire na kushukia bahkresa kariakoo!
Naomba kama unakumbuka vingine usisite kuchangia napenda kuwasilisha wakuu!
Maji ya shadufu matamu sana kaka mwendo wa kupampu tu..., siku hizi dogo hawakutani na shida hizo za umeme na zingine
 
Kulikuwa na mboga za majani na zingine za kupima katika kijiko zinauzwa na wana ulokoni.Aisee zilitu save sana siku za maharage yani tulikuwa tunamix na maharage siku zinasonga.Ofcourse ni maisha flani ya kukumbuka sana
 
Back
Top Bottom