Tujikumbushe Taifa Stars ya 1980s na miamba ya soka Afrika

Kumbe mambo mbotela kashafariki.
R.I.P

Viol...... naomba nisahihishe na nifute usemi wangu wa awali..... 'LEONARD MAMBO MBOTELA HAJAFARIKI YUPO HAI'. SAMAHANI WADAU KWA KULETA TAARIFA AMBAZO HAZIKUWA SAHIHI!!!!!!
 
Viol...... naomba nisahihishe na nifute usemi wangu wa awali..... 'LEONARD MAMBO MBOTELA HAJAFARIKI YUPO HAI'. SAMAHANI WADAU KWA KULETA TAARIFA AMBAZO HAZIKUWA SAHIHI!!!!!!

Pamoja mkuu,maana huyu jamaa nilimsikiliza mwaka Jana tu,sasa nikashangaa gafla imekwaje hata sikusikia kwenye media.


Pamoja mkuu
 

You are some how right by your heading interpretation, but the heading is not as you claim to be!

Vv
 



Hii ilikuwa kabla hawajaanza bongo fleva (uchawi) kwani walijali sana vipaji vya wachezaji si mvuto wa nguvu za giza. Siku hizi kila mchezaji ni mbongo fleva (fake/mchawi) na ndiyo maana hawafundishiki/hawakocheki. Mtu anaona bora aroge ili apande ndege na kwenda kubadirishana jezi na wachezaji wa Misri, akirudi anajisifia kuwa alimpa mchezaji wa Misri jezi yake. Rais Mwinyi was dead right kuwa Taifa Stars ni kichwa cha mwenda wazimu.
 

Umenikumbusha mbali; huyo ni Freddie Ndala Kasheba (Supreme) akiwa na Orchestra Safari Sound.

Hicho kikosi cha Stars ni cha miaka ya katikati ya 1980.

Wachezaji na Timu zao ni: Idd Pazi 'father', Kiwelu Mussa 'Super Kiwelu', Athumani Maulid 'Big man', Ramadhani Lenny Maufi 'Abega', Lilla Shomari, Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' (Simba SC); Said George, na Hillal Hemed (Coastal Union), Athumani Juma 'Chama', Ahmed Amasha, Makumbi Juma 'Bongabonga', Charles Boniface Mkwasa 'Master', (Yanga SC); Mohammed Rishard 'Adolf', na Peter Tino (Pan Africa), Octavian Mrope, na Celestine 'Sikinde' Mbunga (Majimaji). Abdul Wakati Juma alikuwa kiungo mahiri kutoka Small Simba ya Zanzibar.

Vv
 

Umenikumbusha mbali sana, hiki kikosi kama sikosei ilikuwa 1984, nakumbuka tulicheza na Sudan hapa Dar wakatufunga tuliporudiana Sudan tukashinda, man of the Match akiwa Idd Pazi na ndio kisa cha El-hilal kumsajili mwaka huo. Kwenye benchi upande wa Golini alikuwa Ramadhani Korosheni wa KMKM, jamaa nilikuwa sina imani naye!
 
huwa najiuliza hawa mnaowasifu walishirii mara ngapi michuano ya mataifa huru Afrika? mimi naona ni yaleyale hakuna lolote

Hata mimi nashangaa. Eti "miamba ya Afrika". Na hao Misri wajiite nani kama sisi ni miamba? Tatizo letu Tanzania ni kuwa tuna "low expectations" kwenye kila kitu ndio maana tunaona eti kwenda kwenye AFCON na kutolewa kwenye hatua za awali tena miaka 35 iliyopita ni mafanikio. Shame on us!
 
Zamoyoni Mogella alikuwepo kweli mwaka 1980?
 
Ongezea Mogela na Juma Burhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…