Tujikumbushe Taifa Stars ya 1980s na miamba ya soka Afrika

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
5,818
Reaction score
5,555
Wanabodi, nawaomba radhi wenzetu ambao mko chini ya miaka 40 maana hamuwafahamu sana wachezaji hao, lakini kwa kuwa JF ni kisima cha maarifa, mtaweza kupata historia ya miaka hiyo.

Nakumbuka Taifa Stars ya mwaka 1980, ndio pekee ambayo iliyofika mbali zaidi ktk michuano ya AFCON.

Tukumbushane wachezaji wa kikosi hicho, na ambacho hakijawahi kutokea kwa maana ya kufika mbali ktk mashindano hayo.

Baadhi ya wachezaji hao ni:-
1. Juma Pondamali (Mensah)
2. Leopard Mukebezi (Tasso)
3.
4. Leodgar Tenga (T Captain)
5. Jella Mtagwa
6. Mohammed Rishard (Adolf)
7.
8.
9. Augustino Peter (Peter Tino)
10. Mohammed Salim
11. Thuwein Ali

Wakongwe wenzangu, Baba Enock na wengine wachezaji tukumbushane niliowasahau.

Vv
 
Hivi mkuu wangu, Daudi salumu, Kajole Mohammed, Nico Njohole, Kulagwa, Omari Hussein hawakuwemo ktk 1st eleven hii ya Taifa!?
 
Nico Njohole alikuja baadaye pamoja na Ahmed Amasha, Athumani Juma Chama, na Yusufu Ismail Bana. Daud Salum na Kajole sikumbuki kama waliwahi kuwa ktk first eleven ya T Stars.

Kumbukumbu yangu Stars ya 1981iliyopigwa na Harambee Stars Uwanja wa Taif ilikuwa na:Hamis Kinye,Yusuf Bana, Ahmed Amasha, Athumani, Juma Chama, Jella Mtagwa, Nico Njohole, Peter Tino.

Harambee Stars ilikuwa
Mahamoud Abas (Kenya One), Hussein Heri, Josephat Mulira, Bob Ogolla, Wilberforce Mulamba Francis Kadenge, Peter Otieno 'Basanga' na wengine.

Vv
 
enzi za vipaji mpira ulikuwa ziada,enzi za magalasa mpira unahela kweli
 
Nico Njohole alikuja baadaye pamoja na Ahmed Amasha, Athumani Juma Chama, na Yusufu Ismail Bana. Daud Salum na Kajole sikumbuki kama waliwahi kuwa ktk first eleven ya T Stars.

Kumbukumbu yangu Stars ya 1981iliyopigwa na Harambee Stars Uwanja wa Taif ilikuwa na:Hamis Kinye,Yusuf Bana, Ahmed Amasha, Athumani, Juma Chama, Jella Mtagwa, Nico Njohole, Peter Tino.

Harambee Stars ilikuwa
Mahamoud Abas (Kenya One), Hussein Heri, Josephat Mulira, Bob Ogolla, Wilberforce Mulamba Francis Kadenge, Peter Otieno 'Basanga' na wengine.

Vv

kwa Stars nadhani golini alikuwa Pondamali, na ushambuliaji Zamoyoni Mogella ndio alianza kuichezea taifa stars.

Ninakumbuka ilikuwa fainali ya Cecafa Challenge Cup, tulipigwa 1 bila na Harambee goli likifungwa na 'Charles Ouma'

Huku marehemu Leonard Mambombotela akisaidiwa na Juma Njuguna wakiitangaza mechi kupitia KBC
 
Kaka miye, wewe ni mkongwe maana hilo jina ni la enzi za katuni za Chakubanga, Polo, na Bushiri, enzi za Uhuru na Mzalendo pekee.

Bila shaka hiyo mechi ndiyo ile Peter Tino alifungwa bandeji kichwani baada ya kugongana na beki mmoja wa Harambee Stars.

Matokeo ya ile mechi yalituuma sana, maana ktk mechi za makundi tuliwapiga goli moja bila.

Vv
 
kwa Stars nadhani golini alikuwa Pondamali, na ushambuliaji Zamoyoni Mogella ndio alianza kuichezea taifa stars.

Ninakumbuka ilikuwa fainali ya Cecafa Challenge Cup, tulipigwa 1 bila na Harambee goli likifungwa na 'Charles Ouma'

Huku marehemu Leonard Mambombotela akisaidiwa na Juma Njuguna wakiitangaza mechi kupitia KBC

Bao hilo lilifungwa na James Ouma "Jacaranda". Direct Free kick
 
huwa najiuliza hawa mnaowasifu walishirii mara ngapi michuano ya mataifa huru Afrika? mimi naona ni yaleyale hakuna lolote
 
Haijalishi mkuu, lkn T Stars ya wakati huo ilikuwa inaogopwa hata na nchi za Kiafrika zilizopiga hatua ktk soka. Stars ya wakati huo ilikuwa kiwango cha Zambia na Malawi, siyo hii inayopangwa na Botswana, Lesetho na Swaziland ktk preliminaries.

hizo ni hadithi tu.walikuwa wanaogopwa? kuna makombe waliyopata ya kuogopwa. mataifa huru walienda kutolewa mwanzo kabisa ndo ikawa nitolee halafu leo tunawasifu utafikiri walikuwa nguli na chanzo cha kuamini walikuwa bora hakukuwa na tv na watangazaji wa redio walikuwa waongo tofauti na leo mtu unaona uhalisia wa mpira wa timu ndo maana tunawaponda sana.
 
Hivi unajua kuwa kuna wachezaji wawili wa Stars waliwahi kuchaguliwa kwenye kombaini ya Timu ya Afrika? Kwa mantiki hiyo, unaweza kufananisha Stars iliyotoa wachezaji kwenye Timu ya Afrika na hii ya leo?

hatuwezi kupima ubora wa timu ya taifa kwa kutumia kigezo cha kuwa na wachezaji wawili au zaidi kwenye kikosi cha Africa. timu ya taifa inapimwa on collective terms so nitajie kuwa walicheza mataifa huru mara ngapi na walishinda kikombe hicho hata mara moja, vinginevyo ni kutiana moyo kwa kitu ambacho hakijawahi kutokea.
mfano wako ni sawa na kusema mchezaji wa slovenia akichaguliwa kwenye kikosi cha ulaya eti ni ushaidi tosha wa Slovania kuwa timu tishio
 
kwa Stars nadhani golini alikuwa Pondamali, na ushambuliaji Zamoyoni Mogella ndio alianza kuichezea taifa stars.

Ninakumbuka ilikuwa fainali ya Cecafa Challenge Cup, tulipigwa 1 bila na Harambee goli likifungwa na 'Charles Ouma'

Huku marehemu Leonard Mambombotela akisaidiwa na Juma Njuguna wakiitangaza mechi kupitia KBC

Kumbe mambo mbotela kashafariki.
R.I.P
 
hatuwezi kupima ubora wa timu ya taifa kwa kutumia kigezo cha kuwa na wachezaji wawili au zaidi kwenye kikosi cha Africa. timu ya taifa inapimwa on collective terms so nitajie kuwa walicheza mataifa huru mara ngapi na walishinda kikombe hicho hata mara moja, vinginevyo ni kutiana moyo kwa kitu ambacho hakijawahi kutokea.
mfano wako ni sawa na kusema mchezaji wa slovenia akichaguliwa kwenye kikosi cha ulaya eti ni ushaidi tosha wa Slovania kuwa timu tishio

Mkuu, inaonekana unapenda 'ligi' na una ubishi wa Simba na Yanga.

Nimekueleza kuwa kuna wachezaji wa T stars waliwahi kuteuliwa ktk Kombaini ya Afrika ili kulinganisha na ubora wa wachezaji wa T Stars ya sasa; wewe unaongeza vigezo vingine.

Jaribu kupima kwa kutumia mafanikio ya T stars ya nnayoizungumzia Vs T Stars ya sasa; hata kama T Stars ya 1980s haikuwa na mafanikio makubwa, lkn itoshe (kwa vigezo hivyo vichache na rahisi) kusema Stars ile ilikuwa bora zaidi kuliko hii; kwa hiyo wewe tumia vigezo hivyo kupiga mafanikio ya time hiyo kwa vipindi tunavyozungumzia hapa.

Vv
 
View attachment Taifa Stars.mp3

Majina ya wachezaji wanaotajwa kwenye wimbo wa Taifa Stars

Iddi Pazi
Kiwelo Mussa
Said George
Athumani Maulidi
Athumani Chama
Ahmed Amasha
Ramadhani Lenny
Mohamed Adolf
Octaviani Mrope
Makumbi Juma
Peter Tino
Charles Borniface
Lila Shomari
Hillary Hemed
Selestine Mbunga
Zamoyoni Mogela

Abdul Wakati Juma
Joel Bendera

Hao wawili wa mwisho nadhani walikuwa makocha
 
Mkuu, inaonekana unapenda 'ligi' na una ubishi wa Simba na Yanga.

Nimekueleza kuwa kuna wachezaji wa T stars waliwahi kuteuliwa ktk Kombaini ya Afrika ili kulinganisha na ubora wa wachezaji wa T Stars ya sasa; wewe unaongeza vigezo vingine.

Jaribu kupima kwa kutumia mafanikio ya T stars ya nnayoizungumzia Vs T Stars ya sasa; hata kama T Stars ya 1980s haikuwa na mafanikio makubwa, lkn itoshe (kwa vigezo hivyo vichache na rahisi) kusema Stars ile ilikuwa bora zaidi kuliko hii; kwa hiyo wewe tumia vigezo hivyo kupiga mafanikio ya time hiyo kwa vipindi tunavyozungumzia hapa.

Vv

haya bwana naona wewe una ubishi wa kiulaya ulaya. tukitumia vigezo vya mafanikio ya individual players hata leo wapo ambao klabu kubwa za Africa zimewanunua kutoka tz sasa tuseme timu yataifa imekuwa imara? kwanza hii heading inapotosha eti MIAMBA YA SOKA AFRIKA!!! kwa lipi walilofanya .kujifariji tu
 
Back
Top Bottom