Tujikumbushe tuliosoma Kibaha Sekondari miaka ya 1993, Mkuu wa Shule akiwa Mwaipaja

iboyamwaka2020

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2020
Posts
725
Reaction score
844
Wakuu,

Nimepata hamu sana ya kuikumbuka shule niliyosoma O Level na kumaliza mwaka 1993 Form Four. Hebu kama kuna mtu alisoma kipindi hicho tubadilishane mawazo; wakati huo Mkuu wa Shule Mwaipaja; Second Master Mainoya, kina Mpalaza na wengine wengi.

Karibuni
 
Moja ya wakuu wa shule peace sana.

Baadaye alikuja master mmoja alikuwa anaitwa sijui Kayenga kama zoba zoba hivi na second wake chizi mmoja hivi anaitwa Kachingwe Kaselenge "KK"
 
Moja ya wakuu wa shule peace sana...

Baadaye alikuja chizi mmoja alikuwa anitwa sijui Kayenga na second wake Kaselenge
Da! Mkuu Kayenga alikuwa mwalimu wa taaluma aisee Kaselenge alikuwa wa kawaida tu nakumbuka Mwaipaja alikuwa mtu poa sana tulikuwa tunamheshimu sana, da!
 
JF raha sana!
Headmaster - kama zoba zoba
Second master - chizi mmoja
Hahah zoba zoba kwa maana kazubaa sana na asiyejiamini hivi, kwa mtazamo wangu hakuwa na hadhi ya kuwa mkuu wa shule, kwa shule kubwa kama Kibaha.

Sasa msaidizi wake naye alikuwa chizi mmoja, usela umemzidi kiasi anaweza hata tukana matusi ya nguoni mbele ya wanafunzi, anatongoza hovyo tu waalimu wa kike na wadada wadada hata wauza vitafunwa.
 
Mwaka jana nilisikia Mwampaja anaumwa sana, sijui hali yake sasa. Unanikumbusha mbali sana, hivi mwalimu mpalaza yupo?.

Sent using Jamii Forums mobile app
MWALIMU MPALAZA ALIHAMIAGA RUVU SEC NAFIKIRI MIAKA MIWILI AU MITATU KUTOKA 1993 AISEE MUNGU AMSAIDIE MWAMPAJA HUKO ALIKO SINA TAARIFA NAYE MUDA MREFU SANA, UNAJUA MWALIMU KAYENGA ALIKUWA MPOLE MNO KIASI KWAMBA MPAKA ALIKUWA ANA BOA YAANI AKISIMAMA KUTANGAZA KITU PARADE DAAA ILE SHULE HAIKUWA SZE YAKE KWA KWELI NA HUYO SECOND WAKE NDIYO KABISAAA MSELA
 
Mkuu mbona unapiga kelele hivi/Kupayuka?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma A-level. One of the best schools in Tanzania. Form 6 wana vyumba vyao kabisa na wengine ni kama walianza "maisha ya ndoa" wakiwa shuleni
 
Nilisoma A-level. One of the best schools in Tanzania. Form 6 wana vyumba vyao kabisa na wengine ni kama walianza "maisha ya ndoa" wakiwa shuleni
du maisha ya ndoa tena? unajua A LEVEL bana walikuwa wako vizuri yaani vyumba vyao vizuri sana watu wawili wawili tu vya chini walikuwa wana enjoy kwa kweli na elimu ya pale kiukweli ni safi sana
 
du maisha ya ndoa tena? unajua A LEVEL bana walikuwa wako vizuri yaani vyumba vyao vizuri sana watu wawili wawili tu vya chini walikuwa wana enjoy kwa kweli na elimu ya pale kiukweli ni safi sana
Kachingwe Kaselenje. Mwalimu wa GS...huyu alikua smart alikua anapaka nakumbuka kidevu sjui mafuta gani aisee...ilikua ngumu kuona chembe ya nywele....vidume njia kuu mwanalugali na Javisco!!haya yalikua maeneo adimu sana kwa vidume vya mbegu!!!hahaa..nakumbuka Dada mmoja alikua anauza chapati da vjana walipga misele sana mwanalugali!!!maisha Yale acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu: Mwampaja, Mbawala, Kaselenge Kachingwe.

Kuna mzee fulani mfanya usafi sijui alikuwa anaitwa Karangaza anaijua historia ya shule tangu enzi za ukoloni.

Bahati mbaya nilikuta Mwampaja ndio anaondoka 2003:.....
2003-2009: One to Six.


Alexander The Great
 
da mwanalugali yaani acha lakini maisha kipindi hicho yalikuwa raha sana kss napakumbuka sana sijui kama mpaka sasa wanafurahia maisha kama kipindi chetu misele kwa sana mwanalugali
 
utakuwa uliifurahia sana kss umekaa muda mrefu yaani katika shule hiyo ni zaidi ya shule mkuu sisi tulimuacha mwampaja mwaka 1993 nikaenda zangu mazengoo dodoma five na six aisee acha tuvery interesting story
 
Na wa Pugu na azania tutakujua na uzi wetu, na mzumbe watakuja na uzi wao na wa iliboru watakuja na uzi wao na tabora watakuja na uzi wao, kisimiri, marians, tosamaganga , minaki hapo itakuwaje sasa.....

Aya tushajua nyie vipanga mmesoma kibaha(vipaji msuli) wakuu[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
karibu na wewe tujikumbushe mkuu yaani ilikuwa full raha tulisoma kwa raha sana sijui kama kuna shule wana enjoy kama kibaha sec halafu tulikuwa vichwa hasa mkuuu
 
mnamkumbuka second master Mainoya basi mkuu mwampaja alisafiri hali ikawa mbaya shuleni wanafunzi wakaandamana usiku mpaka kwake wacha waanze kupiga mawe nyumba yake kunja taa wakatulizwa na mke wa mkuu wa shule mwampaja kwa heshima ya mkuu alikuwa anaheshimika sana
 
Tangu alipopokea ukuu kutoka kwa Msaki tulianza kula vizuri Sana lol Mungu amkumbuke.
wapi Bob Nasongelya?
 
karibu na wewe tujikumbushe mkuu yaani ilikuwa full raha tulisoma kwa raha sana sijui kama kuna shule wana enjoy kama kibaha sec halafu tulikuwa vichwa hasa mkuuu
Sidhani Kama kuna Shule ya Serikali wanakula raha Kama Kibaha A level tulitupwa Tabora boys na jamaa yangu akawa anapambana rule vizuri Kama Kibaha wakamwambia Kibaha iko chino ya shirika la Elimu alipozidi wakampa kiranja wa chakula, ikawa kimia.
 
Tangu alipopokea ukuu kutoka kwa Msaki tulianza kula vizuri Sana lol Mungu amkumbuke.
wapi Bob Nasongelya?
da umenikumbusha mbali sana nasongelya kwakweli mwampaja alikuwa smart sana tuliifurahia shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…