Courtesy of CTV and Jugo Media
01 September 1990
Dar es Salaam, Tanzania
Ziara ya Papa Yohane Paulo II alipofanya ziara mwaka 1990 na kupokewa na Mh. Rais Ali Hassan Mwinyi.
Mh. Rais Ali H. Mwinyi akimkaribisha Papa Yohane Paulo II (Pope John Paul II) alisema ni heshima kubwa na taadhima kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Dunia kuitembelea Tanzania.
Mbali na mheshimiwa rais Ali Hassan Mwinyi pia alikuwapo Rais wa Zanzibar Mh. Idris Abdul Wakil
Kwanini Idris Abdul Wakil alikuwa Rais wa muhula mmoja? Cardinal Laurean Rugambwa wa Tanzania kadinali wa kwanza muafrika Afrika
Laurean Cardinal Rugambwa [Catholic-Hierarchy] , spika wa Bunge chifu Adam Sapi Mkwawa, Benjamin W. Mkapa akiongozana na Anna Mkapa, Brigedia Moses Nnauye, Getrude Mongella na maaskofu mbalimbali na wananchi wa Tanzania uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
Papa Yohane Paulo II (Pope John Paul II) aliandika historia kuwa kiongozi wa kanisa la Katoliki asiye mtaliano baada ya miaka 400 kupita hapo 1978. Papa Yohane Paulo mzaliwa wa Poland alihudumu mpaka mwaka 2005.
Alizaliwa na kubatizwa jina la Karol Józef Wojtyla hapo mwezi Mei tarehe 18, 1920, katika kijiji cha Wadowice, Poland
Alijiunga na chuo kikuu Jagiellonian University kilichopo Krakow mwaka 1938 alipoonesha kupendelea digrii ya sanaa ya maonesho na ushairi.
Akiwa jijini Dar es Salaam alihudhuria misa katika kanisa la St. Joseph cathedral na kutoa salamu.
Source: Jugo Media