Tujikumbushe vituko vya kisiasa vya 2020

Tujikumbushe vituko vya kisiasa vya 2020

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Mimi nitawapatia vituko vitatu tu.

Mosi, kuna waziri mkuu wa taifa fulani alijivika umasihi eti kaliponya taifa lake dhidi ya korona. Akaitumia hii kama kiki kujipa umaarufu wa kisiasa ktk nchi ile.

Uchaguzi ulipofika wananchi hawakumwelewa. Alikuwa hoi sana kisiasa. Akapiga magoti ktk state moja inaitwa Njombhehl ili kubembeleza wananchi wampigie kura lkn wapi. Ikabidi atafute mabegi meusi na kuyasambaza nchi nzima yakiwa na kura zake.

Mbili, kuna mtawala aliwauzia wanyonge wa taifa lake vitambulisho kwa hela nzuri tu. Ikawa lazima kwa kila mnyonge wa nchi ile kuwa nacho.

Uchaguzi ulipofika, akakana kwamba haikuwa lazima kwa kila mnyonge kukinunua. Mwanasheria mmoja nguli sana akambana kwamba kama haikuwa lazima rudisha hela. Akagalauka tena.

Tatu, huko Ulaya kuna mwanasiasa mwingine anakijenga kijiji cha Chateuax alikozaliwa kwa fedha za umma. Kajenga bonge la international airport na anasomba wanyama toka kila kona ya dunia kupeleka Chateuax.
 
Tatu, huko Ulaya kuna mwanasiasa mwingine anakijenga kijiji cha Chateuax alikozaliwa kwa fedha za umma. Kajenga bonge la international airport na anasomba wanyama toka kila kona ya dunia kupeleka Chateuax
Naona kaamua kufanya yale ya gharika la Nuhu
 
Kuna mtu alienda kujificha kijijini kusikilizia madhara ya Corona huku akiwaambia wengine wapige kazi!Alipoona ngoma haina madhara sana ukanda huu akajitokeza na kusema tufanye maombi!Baadaye akasema Mungu kajibu!Akafanikiwa kucheza na akili za wadanganyika mpaka viongozi wa dini!
 
Kuna mzee mmoja wa makamo alishikilia mama mbele ya hadhira ili tu kumfurahisha farao bila kujali yeye anajiacha utupu.
 
Back
Top Bottom