Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV


Mkuu Pasco nakupata vilivyo. Kipindi fulani niliwahi kuuza mafuta kwenye kituo cha njia panda ya kwenda Tanga na Morogoro Chalinze ulikuwa unapita na LIPIKIPIKI lako kuuubwa. Nimekuuzia sana wese ukawa unasema unakwenda na pikipiki South Africa ukawa unabeba totoz za chalinze kwa kasi ya kutisha. Ulikuwa best yangu sana
 
Last edited by a moderator:

Hahahahaaaaa....ntakula ban kwa name calling
 
Huyu Salama Mfamao alikuwa ni balaa.....kachangia sana ...............
 

Pascal, hebu ongezea na hawa:

26. Tido Muhando (Mzee wa Mwananchi) - Pia nafuatilia sana simulizi zake za kila Jpili - Mwananchi Newspaper.
27. Deborah Mwenda
28. Sarah Dumba
29. Charles Hiral ( Mzee wa BBC)
30. Ishe Muhidin
31. Frolian Kaiza
32. Halima Kiemba
33. Betty Mkwasa ( Mwanasiasa kwa sasa)
34. January Constatine
35. Lando Mabula
36. Abubakar Lyongo
37. Sued Mwinyi
38. Nswima Elnest
39. Malima Ndelema
40. Richard Leo
41. Mohamed Kisengo
42. Christina Chokunogela
43. Shaban Kisu
44. Salim Bonde
45. Sekion Kitojo
46. Ahmed Kipozi
47. Fatma Kipozi
48. Ezekiel Malongo
49. Abdul Ngalawa
50. Hendrick Maiko Libuda
 
Safi sana, hata nyuso zao tu zinaonyesha Waandishi wazalendo - wale makanjanja walikuwa bado hawajazaliwa zama hizo- ha ha ha

 

nafikiri ninayemtafuta ni yule wa itv enzi hizo na kipindi cha kitimoto yuko wapi yule bwana?
 

Nilipenda kipindi hiki,ilikuwa saa 7 mchana i think !
 


Hata hamuelewani, nadhani Pascal amaweka waloptangulia mbele za haki? wewe unaweka na walio hai
 
Mkuu Mzito K, japo mabandiko yako humu, hayaonyeshi muuza wese, unless ni kusaidia tuu kama kazi ya home!, Pikipiki ni kweli, ila hilo la kubeba totoz za Chalinze kwenye pikipiki sio kweli, kwa sababu bike yangu ile, haikuwa na kiti cha abiria!.

Halafu hizo totoz za hapo Linze, mtu ubebe upeleke wapi?, wakati ni za kujiokotea tuu, hata nyuma tuu ya malori, mtu unamaliza shida zako!.
 
siku hizi kuna nondo inaitwa Betty Tesha Mwinuka...ni balaa
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!

Haswaa mkuu,sasa hivi tunasikilizishwa taarab,vijembe vya watangazaji bila kupenda,vipindi vya kuelimisha hasa watoto kama kile cha mkoa kwa mkoa kilikuwa kizuri sana mtoto anakuwa anajua nchi yake ina makabila gani na utamaduni wao ni upi,kupitia redio tu.
 
naongeza:
26. ALLY SALEHE - MBILI KASOROBO NA MIDUNDO SAUTI YAKE ILIKUWA KAMA YA MASOUD MASOUD NGULI WA MUZIKI
27. KWEGIER MUNTHALI
hawa walikufa kwa ajali ya gari la Kwegier Munthali likigongwa na treni hapo gerezani /shaurimoyo?? waliopona ni pamoja na HILDA MWAIPOPO - sijui yu wa wapi - nilisikia aliolewa Kenya??
28. KHADIJA SAID - MWANAMKE WA KWANZA MTANGAZAJI - SIJUI KAMA YU HAI - KIPINDI CHAKE CHA WATOTO - MAMA WA KIGOMA HUYU.

umenigusa sana juu ya Salama Mfamao - kuna siku alipiga wimbo do you remember wa phil collins na kamvua kalikuwa kananyunya mahala fulani hadi wa leo ukipigwa wimbo huo huikumbuka sauti yake iliyokuwa nzuri.

29. DEBORAH CHIHOTA badae MWENDA.
30. RAY CHIHOTA
hawa walikuwa mtu na dada yake na mzee wao Chihota alikuwa maarufu Temeke na Serikalini. Ray alikufa kwa ajali ya gari Zimbabwe alikoamua kufuata roots. Ray alikuwa kwenye idhaa ya Kiingereza akiendesha kikundi cha vijana wakiimba Pop. Vijana kama kina Hussein Shebe nk. Pia alikuwa anasoma Taarifa za habari kwa Kiingereza
 

mkuu ilikuwa inasikika sana kuwa watu wa Tanga wanamaliza wenzao!!! mambo ya uvumi dar ikiwa ndogo!!
 
Mkuu Bala,

Rosemary Mkangara... kwa sasa ni mjasiliamali, yupo kwao Gongo la Mboto-

Nathan Rwehabura-Mara ya mwisho alikuwa Sahara comm....bado yuko Sahara ndiye Mhariri Mkuu

Othman Matata....ni nduguye Chama Omar Matata-Ni mhadhiri wa mihadhara ya kidini.

Kassim Mikongoro...bado yuko TBC ni mwakilishi wa Mtwara, alichomewa nyumba yake kwenye zile vurugu.

Daniel Msangya....

Wilson Malosha....Ni PRO Viwanda na Biashara

Geoffrey Erneo....ni PRO-Bodi ya Utalii

Abdallah Mlawa.....ni retired anaishi Ilala Bungoni.

Yusuph Omar Chunda (mzee wa methali na nahau huyu)....STZ -retired yuko Zanzibar

Makame Abdallah...STZ

Nkwabi Ng'wanakilala - Alikuwa Director wa RTD huyu....Nadhani hata wewe ulikuwa chini yake....ni kweli, kwa sasa ni mhadhiri mkuu wa media chuo kikuu cha Tumaini.

Pascal.
 
Sala dumba nae sijui yupo wapi?

Mkuu wa wilaya mojawapo ya wilaya za mkoa wa Njombe. Hawa walitanguliwa na mama mmoja mtangazaji ambae alikuwa wa kwanza kuukwaa ukuu wa wilaya (dodoma??) kwa jina la Thecla-clara Gumbo - inasemekana kutokana na umahili wake wa kutangaza matukio ya siku ya uhuru wa Msumbiji wakati mate wake akiwa chakari na pombe za kireno!!!

Huyu Gumbo aliwahi pata ajali siku hizo pale Salenda (Surrender) bridge alfajiri moja - dar bwana ilikuwa ndogo sana enzi hizo!!

sijui yu wapi mama huyu mcheshi na mtangazaji mahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…