Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tetee uko vizurii aiseee umenikumbusha mbaliii [emoji4] [emoji4]
 
Kwanza nakumbuka Ezekiel malongo akiwa studio. Mbwe mbwe kibao. Anatamka saa dakika hadi sekunde. Kweli. Mm huwa naburudika sana akiwa yeye hasa kipindi cha mchezo.
 
duuuu jamani nimecheeeeeka kweli kweli yaani unayakumbuka yoooooote hayo aisee wee hatari mimi nilikuwa napenda kipindi cha Mama na Mwana cha Sara Dumba, kipindi cha salamu cha jioni njema... taarifa baada ya habari ilikuwa ikisimuliwa na SS Nkamba siku akisoma mtangazaji mwingine nilikuwa nazima radio au nabadilisha stesheni
 
Nakumbuka tangazo la dawa ya meno Aha..linda meno yako kwa saa ishirini na nne aha aha
Pia nikitoka shulen saa kumi nafungua redio ya baba panasonic nyeusi ina mshale flani ukiiwasha unapoint upande mwingne nakutana na kipindi cha harakati na ile jingle daah namiss sana mambo ya enzi zile
 
Kipindi cha ngoma za asili na Mkoa kwa Mkoa navikumbuka sana na natamani hata leo nipate fursa ya kuzisikiliza nyimbo za makabila mbali mbali
 
Hizo mbona za juzi juzi tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…