Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

namkumbuka Ben Kiko (Benedict Kikoti) na kipindi chake cha mambo hayo kutoka kanda ya kati dodoma. bila kumsahau Abdallah Mlawa.

kwa ujumla RTD haikuwa na mchovu hata mmoja. Ndio maana watangazaji wengi wapo ktika radio za mashirika ya nje.

nikikumbuka watangazaji wa mpira akina:
1. Charles Hillary..... Namna gani pale
2. Dominic Chilambo
3. Omary Jongo
3. Ahmed Jongo .... Inakuwa Obstruction pale
4. Na wengineo
5. Wa sasa hovyoooooo...

Mkuu,hao wa mpira walikuwa mashabiki wa timu zetu kongwe. Ungesikia gol gol kumbe mpira upo katikati ya uwanja
 
Namkumbuka Omary Jongo akitangaza mpira Uganda wakati Yanga wakichukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (siku hizi kombe la Kagame) enzi hizo Lunyamila ndiyo anachipukia akiwa na akina maerhemu Saidi Mwamba Kizota,Mohamedi Husein,marehemu Isa Athumani Method Mogella na wengineo,ilikuwa raha sana kumsikiliza.
 
mnakumbuka kipindi cha mikingamo? Wakati huo mafisadi ndo wakitajwa humo ilikuwa noma. Kipindi cha michezo mbili kasoro, hapo mama ndo anapaalia wali kwa kuweka mkaa juu ya mfuniko basi njaa zinauma tunasinzia tu, ikifika mbili kamili ubeche tayari kwenye sina mtu km tano tumelizunguka hapo hasinzii mtu.

Ha ha ha....rafiki yangu aliniambia kwao mpunga walidhani unatengenezwa kiwandani.
 
Tangazo la IPP : Ah! mama Mariam vipi?.....Hizi nguo dadaangu, nimetumia kila aina ya sabuni lakini bado tu hazitakati!!. Si utumie Komesha?....AIPIPII KEAZ FO YUUUU!
 
Aloisia Maneno
Idrissa Sadala


1. Bujaga Izengo Kadago-Michezo lakini alikuwa anakera habari nzuri anaweka mwisho; pia matukio
2. Debora Mwenda-Mama na mwana
3. Sarah Dumba-majira
4. Julius Nyaisanga-DJ Show, sjui pia na kile Starehe na BP
5. Charles Hillary-
6. Eshe Mhidini-Chaguo la msikilizaji
7. Frolian Kaiza-Pia habari za uchambuzi wa nje(not sure)
8. Tumbo Risasi-Huyu sjui Ruvuma vile
9. David Wakati-Mtalaam huyu
10. Halima Kihemba-Morogoro
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula-Chaguo la msikilizaji
14. Ben kiko-Kanda ya Kati/Dodoma
15. Abubakary Lyongo-Michezo sjui na burudan not sure
16. Sued Mwinyi-Nini palee, Penaaaaat, hapana, hapana ni Kona
17. Abisai Stevin-Huyu sjui ni Rukwa au Ruvuma
18. Nswima Ernest-Huyu Mbeya na Rukwa; maarufu Nswima Eeeerrrrnest
19. Malima Ndelema-Mkoa kwa Mkoa, masihara meeeengi
20. Richard Leo-Kanda ziwa/Kigoma
21. Ahmed Jongo-Goooooooooooooooooooooooh, lalaalalala, gooooooooooooh; nini, Goal Kick!
22. Christina Chokunogela-Habari ila hovyo
23. Shaban KIssu-Mazungumzo baada ya Habari na mwenziwe Angaliani Mpendu
24. Jacob Tesha-Habari murua, na External Service
25. Sallim Mbonde-Majira na Matukio
26. Sekion Kitojo-Taarifa ya Habari na Habari za matukio ya nje kama vita ya Kuwait na Iraq
27. Omary Jongo.

Ongeza na Hawa:
28. Fauzia T. Ismail Aboud-Taarifa ya Habari
29. Dominick Chilambo-kwa wana T.P. lindanda
30. Siwatu Luanda
31. Halima Mchuka
32. Titus Philipo
33. Yusuf Omar Chunda-Zanzibar huyu
34. Sjui ni nani alikuwa anaendesha kile cha Club raha leo show; Full uzalendo kipindi hicho,
Haya bwana wacha wajuzi waje wakuchambulie hapa. Ila ilikuwa inapendeza sana, as if uzalendo ulikuwapo kidogo
 
Watu mnakumbukumbu nahisi machoz kunitoka ile ilikuwa TZ halisi kuanzia viongoz had wananchi wake, TZ ya Leo mhh, national timu hoi, simba yanga kutimua makocha tu. Nakupenda RTD popote ulipo
 
RTD sio mchezo kwa kweli waliotangulia waenziwe siku mmoja...ya kale dhahabu
 
1. TANGAZO LA PEDI ZA JESI:
Wanawake kuweni na furahaaa, furahaaa, wakati wote popote na jesi,
Jesi, pedi mpya za kike za njano, ni nyororo raha kuvaa wakati wote......

2. TANGAZO LA DAWANOL
Mgongo wangu waniuma maumivu teleee, dawa ya maumivu dawa yenye nguvu dawa ni dawanol

3. TANGAZO LA SABUNI YA MSHINDI. n.k

MATANGAZO YA VIPINDI:

1. MASHIRIKA YA TAIFA: Mashirika ya taifa Tanzania yapo Mengi... na matangazo mengine mengi. Huwa natamani sana siku moja niende pale RTD nikaombe nipewe hayo matangazo niwe nayasikiliza tu mwenyewe ili niwe nakumbuka utotoni...DA INANIKUMBUSHA MBALI SANA

Pedi mpya, za kike za jesi
Ni nyororo, raha kuvaa na za kupa kinga thabiti wakati wote, popote na hazina mikanda.
 
duuh watanzania wengine mnasikilizaga radio za wapi..? uncle j Nyaisanga . ni marehemu kwa sasa, aifariki dunia mwaka jana huko morogoro, maiti yake ililetwa dsm , ikaagwa kwenye viwanja vya sigara na kisha ikapelekwa musoma kwa ajili ya mazishi.
kweli hata mimi najiuliza wapiyupo anko J? kuna wakati alikuwa radio one na ITV alikuwa akiendesha kipindi cha hizi nazo, labda isac gamba atufahamishe.
 
duuh watanzania wengine mnasikilizaga radio za wapi..? uncle j Nyaisanga . ni marehemu kwa sasa, aifariki dunia mwaka jana huko morogoro, maiti yake ililetwa dsm , ikaagwa kwenye viwanja vya sigara na kisha ikapelekwa musoma kwa ajili ya mazishi.

Mkuu sinafungu uhali gani kaka?
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na Tanzania kuwa na vituo vingi vya redio na televisheni, kuna watangazaji (Radio and TV presenters) wakali na wenye upeo mkubwa kiasi cha kukufanya upate burudani, usichoke msikiliza au kumwangalia.

Taja presenter mkali Bongo au nje anayekuvutia kiasi cha kukufanye usichoke kumsikiliza na sababu za kumkubali kiivyo.

Binafsi namkubali sana Gadner G. Habash. Huyu jamaa enzi za jahazi (kabla ya Kibonde), nilikuwa sichoki kumsikiliza. Masoud Kipanya na Fina Mango, Power Breakfast ilikuwa poa balaa (kabla ya Gerald Hando na PJ) creativity ya hatari enzi hizo.

Pia Sued Mwinyi, Hamed Jongo na Juma Nkamia. Hawa jamaa RTD enzi hizo wakitangaza mpira iwe Simba na Yanga ndo utapenda, gogogogogoooo mpira ukiwa katikati ya uwanja.

I miss those days.

Karibu ujumuike.
 
Back
Top Bottom