Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Michael Katembo kipindi chake cha mkoa kwa mkoa kikianza anaanza na kukuimbia kwanza mwenyewee then anapiga mh mmmh mmmh mmh maana yake hayajui maneno but anafata mdundo athen anakuba BARRR AAABARAAAAA ni Wamakonde wa Mtwara haooo...then kukawa na mmoja nimemsahau anapiga ijumaa kipindi cha KIjaruba sijui alikuwa ni nani...then Mama na mwana na Ma debora mwenda ..au chei chei shangazi jjioni na Aunt Aloiycia Maneno...Then Club ya Leo Shooooooooooooooooo na Julius Nyaisangah....Then Sikiliza Bwna Umemeeeeeeeee na Satarehe na BPPPP...loh natamani na taarifa ya habari msomaji ni Sango Kipozi lloh au mpira sauti ya kike ya Halima Mchuka
 
Kaka Pascal Mayalla naomba ututambulishe wengine kupitia picha hizi:

Watangazaji-wa-Zamani-RTD.jpg
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.

Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.
 
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.

Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.

Mkuu wa pili kutoka kushoto waliosimama siyo Mike Mhagama?
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
 
Nimemkumbuka Hassan Mgumba kama sijakosea jina na kipindi chake cha matukio ya wiki
enzi hizo kwa sisi wa mpakani tunaipata RTD usiku pekee tena kwenye shortwave
Tulitegemea zaidi raidio za Kenya.
Kuna mwingine anaitwa Mrekoni alikuwa na kipindi chake kizuri cha karibu mgeni au mgeni wetu alifariki majuzi
He was talented.
 
Hee humu naona sasa wa miaka ile tunaanza kufahamiana, Dot com wakae kimya kabisaa! Enzi hizo RTD ilikuwa na watangazaji bwana, unapata raha hata kuisikiliza redio yako ya Taifa. Siyo sasa hivi yamejaa ma-mburula tu!! Jamani wapi BUJAGA IZENGO KADAGO? CHRISTINA CHOKUNOGELA (Binti alikuwaga na sauti tamu huyo enzi zile, nikatokea kumpenda kupita maelezo, mpaka home wakaniozesha kwake kila wakisikia sauti yake tu wanalipuka mkeo anatangaza!!). Jamani haya mamburula ya TBC hebu yajifunze kwa hawa watangulizi! PASCAL saidia hivi viumbe mkuu!
 
Mama Debora Mwenda
Unakumbuka zile hadithi? jumamosi ikifika saa nane mchana watoto wote tuko kwenye radio, na mashuleni tulikuwa na club za mama na mwana

Duh umenikumbusha mbali, kile kipindi cha mama na mwana nilikuwa sikosi; kulikua na hadithi za kusisimua sana, mfano UA JEKUNDU (ambapo kuna stori ya msichana aliyependwa na zimwi lililokuwa na bonge za jumba zuri msituni etc etc..ilikuwa inasisimua enzi hizo za utoto
 
PASCO,

Ili tuelezane ukweli; tangu enzi hizo nimekuwa nikisikia from many different sources kuwa RTD ndio sehemu iliyokua inaongoza kwa fitina, uchawi na kurogana kazini...na hata ufuska...!
Could it not be that this high death rate ya wafanyakazi hapo RTD ilichagizwa na hizo factors??
 
Back
Top Bottom