Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Huyo jamaa yuko hai na nnadhani anaishi maeneo ya UKONGA,maana mara nyingi nakutana nae maeneo ya Banana-Uk.
Kwasasa anarusha kipindi cha "YAKALE NI DHAHABU"
 
Saa nne asubuhi ilikuwepo taarifa ya habari kama sikosei,saa kumi alasiri pia ilikuwepo<hata kifo cha sokoine kilitangazwa wakati huo,saa moja usiku habari kutoka sauti ya tz zanzibar

...Kuanzia saa Mbili asubuhi had Saa Tano kamili RTD ilikuwa inarusha vipindi vya Masomo ya shule za Msingi.Kumbuka 'A Thousand Miles to Tanga'. Kuanzia Saa Tano Kamili hadi Saa Sita ilikuwa ni Kipindi cha Wakati wa Kazi. Saa Sita Kamili hadi Saa Saba ilikuwa ni kipindi cha Salmu cha Mchana Mwema na Saa Saba Kamili Taarifa ya Habari.

Baada ya Hapo, Vipindi ambavyo vingefuata vilitegemea Siku gani ya Wiki lakini vingekuwa ni Pamoja na 'Karibu RTD', 'Mgeni wa Wiki' 'Baraza/Ukumbi wa akina Mama' nk.

Hizi taarifa za Habari za Saa Nne na Saa Kumi zilikuja baadae Sana Mkuu.Taarifa ya Habari Kutoka Visiwani ilikuwa ni Saa 12 Jioni, Nadhani.


Taarifa za Kwanza kabisa za Kifo cha Sokoine hazikuwa kwenye Taarifa ya Habari ya Saa Kumi bali Matangazo ya Kawaida yalisimamishwa na Ikulu inakunganishwa moja kwa moja hewani na ndipo Tukamsikia Mzee wetu Nyerere akitangaza kwa Masikitiko Kifo cha Sokoine.

 
Watangazaji wazuri waliobaki TBC ni, Shaban Kissu, Sued Mwinyi, Agnes Mbapu na Kingalame. Walio wengi vimeo wanajifanya wajuaji sana wawapo hewani. Hakuna nidhamu kama iliyokuwepo enzi za akina Nyaisanga. Wananiuzi sana wanapotumia maneno kama Mwalyego 'ameweza' kufeli masomo.4 au Tino (aliweza) kukosa penati!!!


Acha uongo kama wewe ukiwa unaisikiliza hii redio 24/7 huwezi kuandika ushuzi kama huo uliouandika...
nidhamu ndo msingi wa TBC.
Na Still kuna watu kama Acheli Shilewa, Masoud Masoud, Aloisia Maneno, Al anisa Shida Masamba na wengine weengi wanafanya vizuri still.
Pia kuna chipukizi kwa mfano Betty Tesha Mwinuka anafanya vizuuri mno kiasi kwamba hutachoka kumsikiliza akiwa anatangaza...

Njoo na uharo sasa...maana huo ushuzi haujabamba
 
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.

Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.


Aboubakar Liongo hayupo Ujerumani tena...
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!


Still yupo TBC mpaka leo...
 
Nimemkumbuka Hassan Mgumba kama sijakosea jina na kipindi chake cha matukio ya wiki
enzi hizo kwa sisi wa mpakani tunaipata RTD usiku pekee tena kwenye shortwave
Tulitegemea zaidi raidio za Kenya.
Kuna mwingine anaitwa Mrekoni alikuwa na kipindi chake kizuri cha karibu mgeni au mgeni wetu alifariki majuzi
He was talented.


Ni Hassan Mkumba...sio Mgumba
 
Mama Debora Mwenda
Unakumbuka zile hadithi? jumamosi ikifika saa nane mchana watoto wote tuko kwenye radio, na mashuleni tulikuwa na club za mama na mwana

Nakumbuka sana kipindi kiliitwa mama na mwana....na hadith kama ADILI NA NDUGUZE...
I wish i could turn back the hand of time
 
Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo
  25. Hassan Mkumba
  26. Khadija Said
  27. Ally Saleh
  28. Kwegier Munthali
  29. Leonard Mtawa

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.

Sarah Dumba, sijui yuko wapi?
 
Sio Chaguo la msikilizaji, bali kilikuwa kinaitwa Ombi lako, na pia hakikuwa siku zote, siku zingine tulikuwa tunatupiwa mashairi (Malenga wetu),

CC: jazba

Acha uongo Kipindi Cha chaguo la msikilizaji kilikuwepo tena kama sikosei saa nane mchana siku ya jumamosi
 
Chilambo...chilambo...unaniskia..?..nakuskia Charles..?hapa Uwanja wa Taifa kumekucha Zamoyon Mogela anawainua wapenzi wa Simba...Simba 1 Maji Maji toka Songea hawajapata kitu ....haya Chilambo endelea..!! asante sana Charles hapa Mwanza mambo bado si Pamba wala Ushirika toka moshi waliojipatia bao..lala laal laaa goooooo!!!wakati napokea toka kwako Charles mshambuliaji wa Pamba John Makelele alipata krosi safi sana toka kwa Hamza Mponda anaukwamisha mpira wavuni Pamba 1 Ushirika hawajapata kitu....Daaah ni mengi sana ya kukumbuka sijui kama zile enzi za RTD zitarudi.
YANGA wamevaa jezi za rangi ya kijani na bukta za njano hawa simba wametia UZI nikisema UZI nafikili mmeshanielewa huyo CHARLES HILARY akitangaza mpira SIMBA na YANGA
 
Duh umenikumbusha mbali, kile kipindi cha mama na mwana nilikuwa sikosi; kulikua na hadithi za kusisimua sana, mfano UA JEKUNDU (ambapo kuna stori ya msichana aliyependwa na zimwi lililokuwa na bonge za jumba zuri msituni etc etc..ilikuwa inasisimua enzi hizo za utoto


kiukweli radio tz kipindi hicho ilikuwa radio bana sio ss ivi.. hii mama na mwana ilikuwa kiboko aisee, nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nasoma madrasa ambapo jumamosi na jumapili tulikuwa tunaenda asubuhi na jioni, sasa siku ya jumamosi ilikuwa ni lazima nichelewe kwenda madrasa mchana maana hadi kwanza nisikilize mama na mwana....YAANI ilikuwa ni tamu hatari...nakumbuka ustadh wetu alikuwa mkali kupita kiasi yaani ukichelewa madrasa hata dakika tano ni fimbo lakini siku ya jumamosi wanafunzi wengi tulijitolea kuchapwa na ustadh kwa kuchelewa kuliko kukosa mama na mwana.......yaani sitasahau..

sijui siku hizi watoto wanafurahia nini jamani, ivi wana cha kukumbuka ukubwani kweli zaidi ya facebuku?..dunia imechange sana
 
Acha uongo kama wewe ukiwa unaisikiliza hii redio 24/7 huwezi kuandika ushuzi kama huo uliouandika...
nidhamu ndo msingi wa TBC.
Na Still kuna watu kama Acheli Shilewa, Masoud Masoud, Aloisia Maneno, Al anisa Shida Masamba na wengine weengi wanafanya vizuri still.
Pia kuna chipukizi kwa mfano Betty Tesha Mwinuka anafanya vizuuri mno kiasi kwamba hutachoka kumsikiliza akiwa anatangaza...

Njoo na uharo sasa...maana huo ushuzi haujabamba


...Ni Asheli Chilewa kama sikosei.
Mkuu unafanya kazi huko nini?
Mbona umepaniki mno Brother/Sister? :smile-big:
Maana kama unafanya kazi huko halafu majibu yenyewe ndiyo haya, Mkuu atakuwa amedhibitisha alichosema.
Naamini pointi yako ineweza kueleweka tu bila hayo maneno yanayokarahisha!

 
..Wakuu, Kuna huyu Dada mmoja mtangazaji jina limenitoka kidogo ambaye alifariki kama sio mwaka jana ni juzi tena alikuwa amekwenda kazini na Akaanguka huko na kufariki! alikuwa anaitwa nani vile...??
 
Back
Top Bottom