Tujikumbushie vionjo vya nyimbo zetu za shule ya msingi....!!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Wakuu,
Kwa hakika tumetoka shule tofauti tofauti baina yetu kutoka sehemu mbali mbali za hapa kwetu Tanzania na hata kwa wale wenzetu waliopata neema ya kusoma nchi za nje tangu shule za msingi. Naona simbaya tukikumbashana enzi hizo za kaptura/sketi za blue na (baadhi yetu) soksi za pundamilia tukiwa mstalini tunaimba wimbo wa shule.
Mimi nilisoma Lugalo shule ya msingi na hii ni sehemu ya wimbo wetu wa shule:
Hii shule yetu ya Lugalo la kwanza hadi la saba mwaionaaa,
wanafunzi mnchanganyiko wasichana wavulana mwatuonaaa,
iko wilaya ya kinondoni na kata yetu ya kawe tunasemaaaa,
tutunze mali ya shule, majengo mazingira, lugalo iwe mfanooo........


#reminisce
 
Mapinduzi ungali mtoto mdogo nimepewa jukumu la kukulinda wewe
Na hapa naahidi mbele ya chama mapinduzi nitakulinda mpaka kufaaaa!
 
Kijani kibichi cha mpilipili
Shule yetu ina raha mama weeeh
Ilivyo karibu na barabara!
Vyombo vya pwani twapata bila shida (shidaaa)
 
hahaha. huo wimbo wa lugalo una majigambo sana labda kwavile ni mujini.mie nimesoma kijijini shule ya msingi mawanda lario.
wimbo wetu ulikua kama maombi vilee
shule yetu nzuri ya mawanda,
kwa mola twaiombea baraka,
ubariki uongozi wake, na kuuzidishia baraka.
c/o .ibarikiiiii shule yetu nzuriii, ipate mafanikiooo kwa kila fanii(kwa kila fani).
huo ni ubeti 1 tu zipo.beti 5.
duuu nimekumbuka mbaliii sanaaa
 
zaina!zainaaaa.!
(zainaa)
mtoto wa madeko!
(zaina)
mtoto wa kileo.!
(zaina lete raha zaina)
 

Hahah, majigambo kiasi tu mkuu
 
hahahaaaa! nimecheka sana, mi hata siukumbuki vizur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…