Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
Salaamu wanajamvi,
Imekuwa ada kuanzisha hata kusajili vikundi vya kusaidiana mambo ya kijamii kama vile msiba na sherehe. Sio jambo baya kwa vile linakuza ushirikiano na ustawi wa jamii.
Ila huwa najiuliza kwanini huwa tunatumia nguvu kubwa mno kuanzisha vikundi vya kuzikana na shughuli za harusi? Je, tumezidiwa na hofu ya matatizo? Au ndio tumefika katika ukomo wa kufikiri?
Nafikiri itakua aula zaidi watu wakijikita katika kuungana na kutafuta nguvu ya kiuchumi zaidi. Fikra hii naamini italeta tija katika nyanja mbalimbali za kimaisha hata kuwawezesha wahusika nguvu ya kipato cha kukabiliana na kadhia za maradhi mbalimbali au hata kujikatia bima za afya.
Hamkani kuhamasishana mchango wa kwenda kumzika mtu ilhali hakukuwepo na jitihada kama hiyo wakati wa maradhi yake?
Sikatishi moyo wa watu kusaidiana ila nahamasisha jamii yetu ( ikiwemo mimi binafsi) kuishi katika fikra za kutafuta na kumiliki nguvu za kiuchumi na maendeleo jumuishi.
Nawasilisha.