Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Mkuu,
Hoja yako ni ipi hasa? Unazungumzia namna ya kikokotoo kinavyofanya kazi (kwa maana ya formula) au unazungumzia Jinsi kikokotoo kinavyowakandamiza wastaafu?

Wapi nimesema kikokotoo kipya ni kizuri?? Kuna shida kubwa sana ya ku comment kwenye comment za mbele bila kujua ilikotoke!
Hoja ni kinavyomuumiza mstaafu, swala la kinavyofanya kazi wala haina maana. Hizo kanuni zinawanufaisha wachache wenye mishahara mikubwa ila wengi wanaostaafu na mishahara midogo ni mateso tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mjinga, ni kweli kabisa kwamba huu ni wizi wa wazi na mauaji ya wazi. The government is dancing to Satan's tune of theft and murder. Ni murder kwa sababu unapomsitishia mtu any income at 72 years old, na huko nyuma ulimnyima uwezo wa kuwekeza unategemea nini, si kufa. To some of us serikali inatembea kwenye mkakati ule ule wa NWO wa depopulation.
 
wakati huo mama anaupiga mwingi kwa safari zake zisizoisha
laiti hii kazi ninayoifanya sasa ingekuwaga kuna mtu alinishauri,
ningelimtafuta na kumpiga shaba.
ni kwamba tu ni kiherehere changu kusomea hii kazi kwa kuvutiwa na mavazi
Afisa kipenyo? 😅
 
kupanga ni kuchagua,
fursa ya kubadilisha sheria na taratibu ipo wazi kabisa....

Hii ni sheria na ni lazima ifuatwe na kutekelezwa kikamikifu inavyostajhili mpaka pale itakavyo onekana kuna ulazima wa kuibadilisha na kua vinginevyo...

hata hivyo, utaratibu wa kuwasilisha mapendekezo ya mabadolilo ya sheria lazima ufuatwe, na maoni na mitazamo ya wadau lazima yakusanywe kwa weledi na kuchakatwa vizuri ili hatimae kuja na sheria mbadala na muafaka kwa maslahi mapana ya watumishi nchini.....

Tuendelee kuwaombea viongozi wetu wa inchi, ili mwenyezi Mungu awajaalie afya njema, hekima na busara katika kazi na majukumu yao mazito ya kuwatumikia waTanzania wote kwa haki, usawa na weledi....

Na sisi wananchi Mwenyezi Mungu atuzidishie hekima na busara tunapowasilisha maoni, mitazamo na malalamiko yetu dhidi ya uonevu au kasoro zilizopo kwenye sheria. Tuyawasilishe kwa upendo na upole ili yaweze kupokelewa vema na kufanyiwa kazi kwa weledi na wahusika...

R.I.P Laigwanan comrade ENL
Umeandika kinafiki kabisa,asante kwa mchango wako
 
Wewe huna elimu ya kikokotoo. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Dah hujui kitu bora ungekaa kimya kuficha ujinga wako
 
Wewe huna elimu ya kikokotoo. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Acha upuuzi wewe chawa. Unaongea kupalilia maslahi ya tumbo lako. Kwanini umpangie mtu mzima matumizi ya pesa yake? Ni lini uliwasikia watumishi wanaomba serikali iwaletee huo utaratibu wa kinyonyaji?
Kama huna cha maana cha kusema hebu funga huo mdomo wako?
Kwa kujiita chawa imedhihirisha ni jinsi gani ulivyojaa ujinga kwenye kichwa chako maana chawa na uchafu ni kitu kimoja. Huwezi kukuta chawa mahala ambapo ni pasafi
 
Acha uongo, mfano ma prof vyuoni walipata mpaka mil 30 tu. Kwa ufupi kila mfuko ulikuwa na fomula yake, ila kwa sasa inatoa fursa sawa. Nimemtukana kwa sababu ni mjinga anapotosha watu. Kikokotoo cha sasa kinamuwezesha mstaafu kuishi bila wasiwasi kwa sababu monthly pension ni kubwa na mstaafu akiiwekeza vizuri lumpsum kwenye miradi mbali mbali inamlipa vizuri hata kama ikitokea lumpsum imeisha anaweza kuishi vizuri. Mleta maada aacha uzuzu
Acha utahira wewe, njaa isikupofushe ikakufanya ukaacha kuuona ukweli na kuukiri kwa kinywa chako
 
Za ndani ndani pesa zimechotwa kwa ajili ya uchaguzi kuna watumishi wa afya huko Shinyanga wameambiwa kweupe.

Malipo yao ya extra duty hayapo kwa vile pesa zimechotwa kwa ajili ya uchaguzi, hapo mkurugenzi alikabwa sana mpaka kaona aseme ukweli ...Yeye hana kosa maana anapokea maelezo kutoka juu.

Ebu angalia siasa wanatumia pesa kibao ila wanajua wataiba tu kura ,kuna haja gani ya uchaguzi!?
Miradi ya Maji ilisainiwa kwa mbwembwe imesimama hakuna fedha, pamoja na Magu kuweka utaratibu mzuri kupeleka pesa RUWASA ndipo miradi inatangazwa mama kupitia Mugulu Walichota pesa zote kupeleka hazina.

Dodoma pekee ilikuwa na B 23 za miradi ilisainiwa miradi 13 mwaka 2021 leo hakuna miradi hata mmoja umeisha kwakuwa fedha hakuna
 
Wewe huna elimu ya kikokotoo. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Wewe mjinga itakuwa ni mtumishi wa psssf.
Mwaka juzi Mzee kastaafu kapewa milioni 100 na ushehe na kila mwezi anapata 600k.
Wenzake waliostaafu baada ya upuuzi wenu huu wanajuta.
Hakuna mtumishi wa umma anayefurahia huu ujinga ukiondoa watumishi wa psssf na nssf. Kingekuwa kizuri Wabunge wangekiingiza kwenye malipo yao.
Mimi ninastaafu 2049, sina hofu najua kitakuwa tayari omitted
 
Inaonekana hujui maana ya kustaafu!

Hiyo nguvu ya kuwekeza kwenye miradi anatoa wapi!?

Mbona unajitoa ufahamu??

Sometimes haya mambo ndiyo yanasababisha wizi kwa watumishi wa umma!

Tsh 46M atawekeza nini kwa age ya 55 or 60 zaidi ya kumtafutia presha na kifo cha mapema??
Yaani miaka 60 mtu ahangahikie miradi?
Hawa wapuuzi ipo siku makalio yao yatafidia huu upuuzi wao.
 
Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.

Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu [emoji2960])
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.

Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu [emoji2960]) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!

Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu [emoji2960])

Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?

Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?

Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?

Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.

Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.
Una IQ ya kutosha Mkuu
 
Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.

Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu 🤭)
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.

Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu 🤭) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!

Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu 🤭)

Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?

Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?

Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?

Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.

Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.
Kila kitu kina faida na hasara zake
 
Back
Top Bottom