Tujipime program ya mitihani

Tujipime program ya mitihani

BECKAM

Member
Joined
Feb 23, 2015
Posts
31
Reaction score
12
Kweli teknolojia imekua yaani hawa jamaa wanaendesha mitihani ya kujiandaa ya wanafunzi wa sekondari na shule za msingi kwa njia ya simu.

Leo hii mwalimu wangu aliyenifundisha miaka ya 70 kule chunya alituagiza tuifuate mitihani shuleni takribani kilometa 7 kwa ajili ya kujipima au kujiandaa kwa mtihani wa kitaifa.

Ingekuwa leo hii ningekuambia ''tunaweza kujiandaa hata tukiwa nyumbani mwalimu'' ningeambulia fimbo tu maana ingekuwa nakatisha mianya yake ya kujipatia mlo wa siku na kiasi kilichobakia kwenda gulioni kujipatia kitoweo kwa kweli, shikamoo teknolojia.

Nilikaa juzi usiku nikajaribu na mm kudownload huo mtihani wa hisababti ili nijikumbushe ukokotoaji na nipate majibu nijione kama ntapatia mana tuliamini hesabu ngumu siku zote kumbe ugumu ni sisi wenyewe nikakaa na majibu yangu pembeni nikamuita kijana wangu ameingia kidato cha 4 mwaka huu ili nipambane nae,

nae akaufanya mtihani ule ule kisha nikalipia nikautuma nikapata majibu nilipatia baadhi ila kijana wangu alinipita.

Ni programu nzuri hongera kwao waliofanikisha zoezi hili kwa vijana wa kitanzania wanaosoma kipindi cha sasa maana elimu imeletwa mikononi kwao kabisa tofauti na kipindi cha nyuma sie tukisoma mambo hayakuwa rahisi namna hii.

Nawasilisha...Bravo
 

Attachments

  • tujipime.jpg
    tujipime.jpg
    3.2 MB · Views: 86
Back
Top Bottom