Mnyonge ni mtu gani? Mnyonge ni mtu anaye nyimwa haki yake. Mnyonge ni mtu ambaye anakandamizwa na utawala akihangaika kulima, mazao yake yanaporwa, au anapangiwa bei ya kuuza, au anapangiwa sehemu ya kuuza. Hayuko huru kufanya kazi zake.
Mfanyakazi mnyonge hapandishwi mshahara. Anatumikishwa. Hana sauti, hawezi kudai haki. Hawezi kuchagua kiongozi anaye mpenda maana kura yake inaporwa. Eneo lake na nyumba yake inachukuliwa na serikali bila kulipwa fidia. Akifikwa na majanga ya asili kama matetemeko au mafuriko serikali haimpi msaada inasema siyo iliyoleta majanga.
Akilalamikia malipo ya choo anaambiwa akae na mavi yake.
Mnyonge hama sauti, hasikilizwi.
JPM alitengeneza wanyonge ili awe kiongozi wa wanyonge. Fundi mkuu akafanya yake.
Serious kiongozi yeyote anayeweza kujisifu kuwa ni kiongozi wa wanyonge anatakiwa akataliwe. Maana kiongozi mzuri anawatoa watu kwenye unyonge.