Tujitahidi kujenga chumba cha leseni,vyeti na risiti kwenye majengo yetu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Maisha yanavyokimbia kila Jambo unalofanya linapaswa kuwa kwenye maandishi. Kila jambo unalolipa linapaswa kuwa kuwa na risiti.

Kila kazi unayofanya unatakiwa kuwa na cheti kwa maana umekaa darasani ukasomea na kupata, hata kuchuna ng'ombe na mbuzi utatikiwa kuwa na cheti.

Kila biashara unayofanya leseni lazima,ili utambulike lazima uwe na kitambulisho. Utajikuta una kitambulisho Cha Taifa, Kura, machinga, uchunaji ngozi, ufundi seremala, fundi, nk

Hapo ujaweka vyeti vya shule, chuo, vyakuzaliwa, elimu ya dini, chanjo, bima, leseni, nk

Kwa mtiririko huu wa leseni, risiti na vitambulisho unashauriwa kujenga chumba maalum chakuhifadhi ili mamlaka za serikali zitakapokufikia uwakabidhi ufunguo waendelee na upekizi.

Ila tunapaswa kujiuliza, walioendelea nao wana leseni nyingi hivi? Vyeti vingi hivi? Vitambulisho vingi hivi?

Kwanini taasisi za serikali wasiwe na mfumo mmoja wa utoaji huduma ambao taarifa namba mfano kitambulisho Cha Taifa inaweza kuunganishwa na taasisi nyingine zote?
 
8be7da0c6541986eabf19c4bacb126b2.jpg
 
Nuna vitambulisho zaidi ya 24
Nakusubiri hiki cha tin number na hati ya madeni ya benki
Hii nchi ni ya uchumi wa kati
 
Sound as a pithole country?kitamulisho ni kimoja tu ID inayoongea na system's ya nchi nzima kuanzia mabenki,hospitals,polisi,etc etc
 
Aha haaa
Ni kawaida sana. Ubeberuni kuna kadi ya commuter transport, kazi, makazi, gym, atm, library, passport etc. Maisha ndivyo yanavyoenda.
 
Unauelewa mdogo sana, kadri teknolojia inavyokuwa na ID + documents nazo ndio zinaongezeka.
Kwa wenzetu huko kuna hadi ID kwa ajili ya transport
 
Maisha yanavyokimbia kila Jambo unalofanya linapaswa kuwa kwenye maandishi. Kila jambo unalolipa linapaswa kuwa kuwa na risiti.

Kila kazi unayofanya unatakiwa kuwa na cheti kwa maana umekaa darasani ukasomea na kupata, hata kuchuna ng'ombe na mbuzi utatikiwa kuwa na cheti.

Kila biashara unayofanya leseni lazima,ili utambulike lazima uwe na kitambulisho. Utajikuta una kitambulisho Cha Taifa, Kura, machinga, uchunaji ngozi, ufundi seremala, fundi, nk

Hapo ujaweka vyeti vya shule, chuo, vyakuzaliwa, elimu ya dini, chanjo, bima, leseni, nk

Kwa mtiririko huu wa leseni, risiti na vitambulisho unashauriwa kujenga chumba maalum chakuhifadhi ili mamlaka za serikali zitakapokufikia uwakabidhi ufunguo waendelee na upekizi.

Ila tunapaswa kujiuliza, walioendelea nao wana leseni nyingi hivi? Vyeti vingi hivi? Vitambulisho vingi hivi?

Kwanini taasisi za serikali wasiwe na mfumo mmoja wa utoaji huduma ambao taarifa namba mfano kitambulisho Cha Taifa inaweza kuunganishwa na taasisi nyingine zote?
Huko mbele ndio kabisa!!, ila vyeti vyote huko vinaonekana kupitia namba moja inayotolewa kwa kila raia, inaitwa evidence number kwa baadhi ya nchi. Kwa hapa kwetu, namba zote za vitambulisho zingeweza kuonekana kupitia namba ya kitambulisho cha taifa.
 
Na wale tunao oa kila mwaka tuna lundo la vyeti vya ndoa.
 
Siwezi miliki ma ID mengi kiasi hiki.
ID tano tu zinanitosha NIDA, Passport, leseni, Bank, Kazi.

Na yote haya yanakaa kwenye wallet bila shida.
Just imagine usumbufu wallet ikipotea
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Siwezi miliki ma ID mengi kiasi hiki.
ID tano tu zinanitosha NIDA, Passport, leseni, Bank, Kazi.

Na yote haya yanakaa kwenye wallet bila shida.
Chakupigia kura mkuu umekisahau
 
Back
Top Bottom