Tujitahidi kulima mpira. Tutakosa kondomu na gloves

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Nchi wazalishaji wakubwa wa kondomu(Malaysia na Thailand) zinapanga kuongeza bei ya kondomu kwa asilimia 20-30 sababu ya kupanda kwa bei za uzalishaji(mafuta). Gloves nazo zitapanda sababu mlolongo wake ni kama wa kondomu tu.

Wakati wa covid nchi kondomu ziliadimika sana sababu ya kuyumba kwa usafirishaji na mpira kutumika kuzalisha gloves. Pia gloves nazo zikaadimika sababu wazalishaji walibania kuuza nje, mahitaji ya ndani kuhudumia wahonjwa yalikuwa makubwa. Na pia nchi tajiri ziliweka maorder makubwa makubwa.

Hapa tusipojiongeza, ikitokea ishu nyingine kama Covid hatutaona cha gloves wala kondomu. Na huku tu kupanda kwa bei zake kutafanya ma STIs yaongezeke. Ni aibu mwanafunzi wa afya kuambiwa anavyoenda field aende na pesa ya gloves!! Moja ya bajeti kubwa kwa mama anayeenda kujifungua ni mipira!

Wajerumani ndiyo walianzisha kilimo cha mpira Tanganyika, huko Tanga. Leo tuna mashamba makubwa mawili ya mpira. Tanga na Kilombero. Ila mashamba hayo yapo yapo tu.

Tufufue hayo mashamba,
tuongeze mengine na tuanze kuzalisha kondomu na gloves. Hizi aibu ndogo ndogo tunaweza ziepuka.







 
Ukilimwa utaota kweli !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…