Tujuane Wangapi Ambao Tumeshawahi Kupitiwa Na Shetani Hapa...

kiben10

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
613
Reaction score
791
Mshambuliaji mwenye asili ya Guinea kinda Lamine Diaby-Fadiga anayekipiga na klabu ya Nice (Ufaransa) anatuhumiwa kuiba saa ya mchezaji mwenzake nyota aliyesajiliwa kutoka Ajax, Kasper Dolberg.

Saa hiyo inathamani ya Β£62,000 (zaidi ya shilingi million 175 za Tanzania), Diaby amekiri kuchukua saa hiyo iliyokuwa imeachwa na mchezaji mwezake kwenye chumba cha kubadilishia nguo (dressing room).
β€’
Diaby ameshaomba radhi kwa mchezaji mwenzake ambaye alimuibia saa pamoja na kocha wa Nice Patrick Viera.

Jambo hili huenda likamchafua sana Lamine Diaby-Fadiga mbele ya safari kwa kupita na saa ya mchezaji mwenzake.
 
Aiseee jamaa kajiharibia sana aisee hasa kwa wenzetu ulaya itakua doa katika maisha yake yote
 
Mkuu hilo Jina la Fadiga umempa la Utani kutokana na Udokozi wake ukikumbuka Issue ya Msenegali Khaliou Fadiga kule Ufaransa wakati ya World Cup au Majina yao yamefanana. Yote kwa yote dogo kaharibu sana
 
hapo tatizo sio kuiba

tatizo kaiba mwafrika na kaharibia zaidi waafrika..

na alivyo mshamba hakujua kwamba INA GPS... hadi alipofatwa na kukutwa NAYO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…