Tujulishane kuhusu Kilimo cha Coriander/Giligilani: Mbegu bora, Utaalamu, Magonjwa, Mazingira na Masoko

1800

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
2,215
Reaction score
604
Wadau nakuja tena jukwaani kwa mara nyingine kutaka kujifunza zaidi kutoka kwenu!

Leo ningependa kupata elimu toka kwenu juu ya kitu kinachoitwa Giligilani au Coriander kwa lugha ya kigeni!

Ningependa kujua tu je zao ili linalimwa wapi hasa na juu ya hali ya hewa inayohitajika kulima zao hili!

Zao hili ni kiungo(Recipe) na linauzwa sana kwenye masoko hasa ya ndugu zetu wenye asili ya bara la Asia na hata kusafirishwa zaidi nje!

Kwa mdau yeyote mwenye uelewa zaidi juu ya zao ili naomba atupe shule zaidi

Natumaini wadau wa kilimo chakula na kilimo biashara hamjambo,

Ninalo hitaji la kulima zao la giligilani kuanzia mwezi wa 2 mwaka huu, hivyo basi naomba majibu juu ya aina ya mbegu bora ya giligilani ya kuvuna mbegu pia na upatikanaji wake kwa mikoa ya kanda ya ziwa,

Pia naomba kujua kuhusu soko la giligilani za mbegu kwa kanda ya ziwa na Tanzania nzima ama Afrika mashariki.
 
Wadau nakuja tena jukwaani kwa mara nyingine kutaka kujifunza zaidi kutoka kwenu!leo ningependa kupata elimu toka kwenu juu ya kitu kinachoitwa GILIGILANI au CORIANDER kwa lugha ya kigeni!ningependa kujua tu je zao ili linalimwa wapi hasa na juu ya hali ya hewa inayohitajika kulima zao ili!zao ili ni kiungo(Recipe) na linauzwa sana kwenye masoko hasa ya ndugu zetu wenye asili ya kiasia na hata kusafirishwa zaidi nje!kwa mdau yeyote mwenye uelewa zaidi juu ya zao ili naomba atupe shule zaidi
zao hili lina sitawi katika maeneo yote ya tanzania,maeneo kama mbeya na iringa ni mazuri zaidi maana halihitaji joto kali.zao hili linasitawi katika maeneo yenye joto lisilozidi nyuzi 20-25
maeneo mengine ya tanzania yaliyosalia yenye joto zaidi ya nyuzi 20-25 ni vizuri ulime wakati wa msimu wa mvua maana joto linakuwa sio kali
linasitawi vizuri katika udongo wa tifutifu na kichanga.hekta moja ukiwa na kilo 40 za mbegu zinatosha kupanda.ukipanda mbegu inaanza kuota siku ya 8-15.mbegu zinapandwa moja kwa moja shambani sio kitalu.
angalia unapo funika mbegu usifunike udongo mwingi,tabaka la udongo lisizidi nusu sentimita.hakikisha siku ya kwanza hadi 12 toka umepanda mbegu uzimwagie maji kila baada ya siku 2 baada ya kuota unaweza ukamwagilia mara 2 au tatu kwa wiki.
umbali wa shina hadi shina inategemea na ulichokusudia kuvuna,kama umekusudia kuvuna majani sia mdegu kama unavyo sia mbegu za mchicha usirundike mbegu sana.tunza baada ya siku 40 toka kuota zitakuwa tayari kuvunwa.kama unavuna majani uvune kabla hajijatoa maua au zikifikia urefu wa sm 20 ziko tayari kuvunwa.unapo vuna vuna asubuhi ng'oa mche na mizizi yake osha mizizi kutoa udongo funga matitamatita kutegemeana na soko lake.usikate mizizi
kama unakusudia kuvuna mbegu,umbali wa shina hadi shina liwe sm 10-15 na kutoka msitari hadi msitari umbali ni huo huo.ni vizuri ukasia mbegu baada ya kuota ndo ukaachanishia umbali huo.uvunaji wake ni mpaka pale utakapoona mbugu zake zimekomaa na kubadirika rangi na kuwa kahawia.kuvuna ng'oa miche irundike baada ya siku 7 piga polepole mbegu zitoke pepeta tayari kwa kuuza
yapo magonjwa yanayo shambulia zao hili ila ni machache sana.magonjwa haya ni kushambuliwa na wadudu dawa za kuua wadudu wa mimea inamaliza tatizo.ugojwa mwingine ni ukungu/fangasi tumia dawa za ukungu tangu miche inapoota hadi kuvuna dawa utakayonunua maana siku hizi dawa ni nyingi ila utayonunua itakupa maelezo utumie vipi
ANGALIZO 1/ Kuna aina kuu mbili za giligilani,giligilani fupi na ndefu.giligilani fupi ni nzuri kwa yule anaekusudia kuvuna mbegu inatoa maua ikiwa fupi sana na inawahi kukomaa.aina hii mbegu zake ni nyingi na ndo unazoziona masokoni sio nzuri kabisa kwa kuvuna majani.
2/giligilani ndefu ambayo ni maalum inafaa hasa kwa anae taka kuvuna majani ingawa mbegu zake hufaa pia kwa viungo.hii inalefuka zaidi kabla ya kutoa maua.aina hii ya giligilani mbegu zake ni chache sana sio rahisi kuzipata masokoni.ila nakifahamu kikundi fulani wao huzalisha mbegu za giligilani ndefu ya majani.ukihitaji mbegu hizi ndefu au msaada zaidi wowote juu ya kilimo cha bustani ebu ni PM
 
Asante sana mkuu!thats why i love JF,ni zaidi ya shule!kila kitu unapata na kujifunza hapa!nadhani idea tuzipatazo humu JF tukiwa effort na kuzi implement,angalau suala la ukali wa maisha litapungua kiasi!mkuu nitaku PM maana ninahitaji kujifunza mengi juu ya kilimo cha bustani!leo niko safarini hapa na ninatumia simu,ila niki settle nitaku PM,ila labda kwa faida ya wadau wengine,je soko la ili zao la GILIGILANI likoje?kwa maana demand yake ni kubwa au ni zao linalosumbua kuuzika sokoni?na vipi kuhusu maeneo ya mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilosa je naweza kufanya kilimo cha GILIGILANI na zao likakubali?Ahsante!
 
zao hili soko lake ni kubwa kwa DAR wala halisumbui.heka moja ninatoa sio chini ya gunia 15 za debe 7 na gunia moja lina kilo 70 bei kilo moja tsh 4500/=.huko kilosa zao hili linasitawi sana
 
Mkuu nina ku PM
 
Nakushukuru sana kwa kuuliza swali hili kwani limekuwa msaada kwangu pia kutokana na majibu/maeolezo yaliyotolewa na ndg.ehee kumbe
 
zao hili lina sitawi katika maeneo yote ya tanzania,maeneo kama mbeya na iringa ni mazuri zaidi maana halihitaji joto kali.zao hili linasitawi katika maeneo yenye joto lisilozidi nyuzi 20-25
maeneo mengine ya tanzania yaliyosalia yenye joto zaidi ya nyuzi 20-25 ni vizuri ulime wakati wa msimu wa mvua maana joto linakuwa sio kali
linasitawi vizuri katika udongo wa tifutifu na kichanga.hekta moja ukiwa na kilo 40 za mbegu zinatosha kupanda.ukipanda mbegu inaanza kuota siku ya 8-15.mbegu zinapandwa moja kwa moja shambani sio kitalu.
angalia unapo funika mbegu usifunike udongo mwingi,tabaka la udongo lisizidi nusu sentimita.hakikisha siku ya kwanza hadi 12 toka umepanda mbegu uzimwagie maji kila baada ya siku 2 baada ya kuota unaweza ukamwagilia mara 2 au tatu kwa wiki.
umbali wa shina hadi shina inategemea na ulichokusudia kuvuna,kama umekusudia kuvuna majani sia mdegu kama unavyo sia mbegu za mchicha usirundike mbegu sana.tunza baada ya siku 40 toka kuota zitakuwa tayari kuvunwa.kama unavuna majani uvune kabla hajijatoa maua au zikifikia urefu wa sm 20 ziko tayari kuvunwa.unapo vuna vuna asubuhi ng'oa mche na mizizi yake osha mizizi kutoa udongo funga matitamatita kutegemeana na soko lake.usikate mizizi
kama unakusudia kuvuna mbegu,umbali wa shina hadi shina liwe sm 10-15 na kutoka msitari hadi msitari umbali ni huo huo.ni vizuri ukasia mbegu baada ya kuota ndo ukaachanishia umbali huo.uvunaji wake ni mpaka pale utakapoona mbugu zake zimekomaa na kubadirika rangi na kuwa kahawia.kuvuna ng'oa miche irundike baada ya siku 7 piga polepole mbegu zitoke pepeta tayari kwa kuuza
yapo magonjwa yanayo shambulia zao hili ila ni machache sana.magonjwa haya ni kushambuliwa na wadudu dawa za kuua wadudu wa mimea inamaliza tatizo.ugojwa mwingine ni ukungu/fangasi tumia dawa za ukungu tangu miche inapoota hadi kuvuna dawa utakayonunua maana siku hizi dawa ni nyingi ila utayonunua itakupa maelezo utumie vipi
ANGALIZO 1/ Kuna aina kuu mbili za giligilani,giligilani fupi na ndefu.giligilani fupi ni nzuri kwa yule anaekusudia kuvuna mbegu inatoa maua ikiwa fupi sana na inawahi kukomaa.aina hii mbegu zake ni nyingi na ndo unazoziona masokoni sio nzuri kabisa kwa kuvuna majani.
2/giligilani ndefu ambayo ni maalum inafaa hasa kwa anae taka kuvuna majani ingawa mbegu zake hufaa pia kwa viungo.hii inalefuka zaidi kabla ya kutoa maua.aina hii ya giligilani mbegu zake ni chache sana sio rahisi kuzipata masokoni.ila nakifahamu kikundi fulani wao huzalisha mbegu za giligilani ndefu ya majani.ukihitaji mbegu hizi ndefu au msaada zaidi wowote juu ya kilimo cha bustani ebu ni PM

Habari..
nataka kulilima zao hili, je kwa Bagamoyo litasitawi?na kwa heka moja inaweza ikagharimu sh.ngapi?
asante
 
habari,
ninahitaji mbegu za giligilani ndefu na fupi ..nimejaribu kwenye maduka ya pembejeo hazipatikani kabisa.
Tafadhali kwa mkulima,
muuzaji wa mbegu ama mtu yeyote mwenye kufahamu upatikanaji wa hizi mbegu na bei zake anisaidie.
ninahitaji kwa ajili ya kupanda.
ahsante.
 
mkuu uko wapi zipo nyingi sana hapa arusha kg 10000
 
mamseri nipo Dar es salaam
Ngoja niangalie hapa nikikosa unisaidie Tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Hapo Dar si umesema umeshakosa?

Sijazunguka Dar es salaam yote.
Inawezekana Kuna mahala zinapatikana hapa hapa na sijapafahamu.
Nikikosa nitakuwa sina budi kumtafuta mkuu hapo juu.
 
Habari wanajukwaa,

Mimi ni mkulima mchanga kabisa. Naomba msaada wa kujua soko zuri la giligilani.

Nimelima giligilani ndefu kwa ajili ya kuvuna majani.
 
Giligilani, samahani mkuu nifahamishe please... ndio zao gani hilo? Linatumika vipi? Lina limwa pande zipi?
 
Habari mankwe11. naomba unisaidie kujua wapi napata mbegu ndefu ya giligilani na bei yake. Ningependa pia kujua uzoefu wako kuhusu soko ulipovuna.
 
Natumaini wadau wa kilimo chakula na kilimo biashara hamjambo,

Ninalo hitaji la kulima zao la giligilani kuanzia mwezi wa 2 mwaka huu, hivyo basi naomba majibu juu ya aina ya mbegu bora ya giligilani ya kuvuna mbegu pia na upatikanaji wake kwa mikoa ya kanda ya ziwa,

pia naomba kujua kuhusu soko la giligilani za mbegu kwa kanda ya ziwa na Tanzania nzima ama Afrika mashariki.
 
Back
Top Bottom