Tujuzane!! Benki ikifilisika au kuungua moto wateja waliohifadhi hela zao inakuwaje??

Tujuzane!! Benki ikifilisika au kuungua moto wateja waliohifadhi hela zao inakuwaje??

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
3,192
Reaction score
5,743
Wadau kwenye nchi kila siku bank zimekuwa zikiongezeka kila siku. Hali hii ni nzuri maana inaongeza ushindani na kumfanya mteja kupata huduma nzuri zaidi tofauti na bank ilivyokuwa chache. Kwa mfano hakuna mtu anayependa kwenda kwenye bank zenye utitiri mwingi wa watu maana kama unataka kupata huduma lazima itakuchukua kupoteza karibia siku nzima ukiwa bank. Hakuna anayependa kupoteza muda mwingi namana hii kwa siku. Cha ajabu zaidi utakuwa ukipokea majibu ya kiburi kutoka kwa wahudumu ya kutokumtosheleza/kumridhisha mteja pale unapohitaji huduma kutoka kwao.

Katika hali kama hii watu tunakimbilia sehemu ambazo tunaweza kupata huduma nzuri na kuhudumiwa kwa haraka. Ila kuna jambo lingine ambalo linaniogopesha kwenye huu utitiri wa bank. Ikitokea bank IKIFILISIKA au KUUNGUA MOTO, Je, kuna uwezekano wa mteja kupata hela yake aliyohifadhi katika bank hiyo?

Wakuu naomba tusaidiane kupeana taarifa juu hili ili wakati wa kuchagua bank ya kuhifadhi madafu yetu tuwe makini zaidi.
 
Wadau kwenye nchi kila siku bank zimekuwa zikiongezeka kila siku. Hali hii ni nzuri maana inaongeza ushindani na kumfanya mteja kupata huduma nzuri zaidi tofauti na bank ilivyokuwa chache. Kwa mfano hakuna mtu anayependa kwenda kwenye bank zenye utitiri mwingi wa watu maana kama unataka kupata huduma lazima itakuchukua kupoteza karibia siku nzima ukiwa bank. Hakuna anayependa kupoteza muda mwingi namana hii kwa siku. Cha ajabu zaidi utakuwa ukipokea majibu ya kiburi kutoka kwa wahudumu ya kutokumtosheleza/kumridhisha mteja pale unapohitaji huduma kutoka kwao. Katika hali kama hii watu tunakimbilia sehemu ambazo tunaweza kupata huduma nzuri na kuhudumiwa kwa haraka. Ila kuna jambo lingine ambalo linaniogopesha kwenye huu utitiri wa bank. Ikitokea bank IKIFILISIKA au KUUNGUA MOTO, Je, kuna uwezekano wa mteja kupata hela yake aliyohifadhi katika bank hiyo? Wakuu naomba tusaidiane kupeana taarifa juu hili ili wakati wa kuchagua bank ya kuhifadhi madafu yetu tuwe makini zaidi.
Umesoma hadi darasa la ngapi? kwa faida yako - Bank huweka dhamana BOT(BANK KUU YA TANZANIA) - Hawaruhusiwi kua na hela inayozidi kiwango hicho cha dhamana Tofauti kati ya bank zawa na ya kigeni ni gharama unazotozwa za kuhudumiwa bank Mfano: Eco-Bank wameingia na wamecut market price kwa huduma mbali mbali wanazotoa ili wateja kama ww mkimbilie huko -
 
Kwani kutoa maoni ni lazima kutoa kashfa? Watu wangine mmekaa kidharau dharau tu. Unafikiri wewe unajua kila kitu kinachoendelea huku ulimwenguni? Hata hilo unalolifahamu pia hukulijua wewe mpaka ulipopata taarifa sehemu fulani. Ukitaka kumsaidia mtu au kumpanua ufahamu wake siyo lazima kumkashfu, ndo maana tunaelimishana kila siku.
 
kwani kutoa maoni ni lazima kutoa kashfa? Watu wangine mmekaa kidharau dharau tu. Unafikiri wewe unajua kila kitu kinachoendelea huku ulimwenguni? Hata hilo unalolifahamu pia hukulijua wewe mpaka ulipopata taarifa sehemu fulani. Ukitaka kumsaidia mtu au kumpanua ufahamu wake siyo lazima kumkashfu, ndo maana tunaelimishana kila siku.
kuku uliza kiwango cha darasa ni kashafa?
 
Kuwa na heshima japo kidogo,sio kila aliyesoma anaelewa kila kitu,kila mtu ka specialize sehem yake,hata wewe unaejifanya umesoma nikikupa swali huwezi jibu,kwa hiyo jaribu kuwa social na watu,elimu yako isikutie kiburi bado hujafika mahali.
 
Kwa uelewa wangu benk ilyosajiliwa na inatambulika BOT huwa zina bima, kwa hiyo huwez kupoteza chochote. Vile bank znaweka hela kwny masanduku ambayo yanaungua kwa nje lakini ukifungua pesa/notes unazkuta hazjaungua, labda moto uwe unatokana na bomu, barut/explosiv au fataki/detenators ambayo inasambartsha sanduku ktk vpandevpande!
 
Wadau kwenye nchi kila siku bank zimekuwa zikiongezeka kila siku. Hali hii ni nzuri maana inaongeza ushindani na kumfanya mteja kupata huduma nzuri zaidi tofauti na bank ilivyokuwa chache. Kwa mfano hakuna mtu anayependa kwenda kwenye bank zenye utitiri mwingi wa watu maana kama unataka kupata huduma lazima itakuchukua kupoteza karibia siku nzima ukiwa bank. Hakuna anayependa kupoteza muda mwingi namana hii kwa siku. Cha ajabu zaidi utakuwa ukipokea majibu ya kiburi kutoka kwa wahudumu ya kutokumtosheleza/kumridhisha mteja pale unapohitaji huduma kutoka kwao.

Katika hali kama hii watu tunakimbilia sehemu ambazo tunaweza kupata huduma nzuri na kuhudumiwa kwa haraka. Ila kuna jambo lingine ambalo linaniogopesha kwenye huu utitiri wa bank. Ikitokea bank IKIFILISIKA au KUUNGUA MOTO, Je, kuna uwezekano wa mteja kupata hela yake aliyohifadhi katika bank hiyo?

Wakuu naomba tusaidiane kupeana taarifa juu hili ili wakati wa kuchagua bank ya kuhifadhi madafu yetu tuwe makini zaidi.

Mkuu nimepata concern yako;katika mabenki asilimia kubwa vitu viko structured.Kwa kuanzia,kwenye benki kuna kitu kinaitwa SMR,STATUTORY MINIMUM RESERVE,hii huongezeka kadiri BOT wanavyoona.Kwa mfano BOT waliongeza SMR ya bank kwenye government deposits mpaka 30% of the deposits.(Hii ina maana kama benki wanazo government deposits za 10 Mil,wanalazimika kupeleka BOT 3M kama Statutory Minimum Reserve)...Hili ni la kwanza.
Pili,Kuna kitu kinaitwa DEPOSITORS INSURANCE BOARD,hii iko chini ya Mr.Marisa wa pale BOT,lakini so far,Hii insurance board inao uwezo wa ku'refund 1,500,000 flat kwa wahanga wa benki iliyofilisika.The rationale beyond this ni kwamba wanaamini depositors wengi ni wadogo wadogo,na resarch iliyofanyika inadai kwamba ukilipa maximum ya 1,500,000 utaweza kulipa more than 85% ya depositors wote in full....Una swali??
 
benki ikiungua huna chako mkuu,kama uliweka hela zako sahau
 
Kufilisika inaweza kuwa jambo la hatari kwa mteja wa benk husika. Lakini kuungua moto sidhani kama ni hoja au ni jambo la kuogopa sana kwa sababu data zako zote zipo kwenye mtandao na ndio maana hata sasa hivi siyo lazima uchukulie au udeposit hela yako kwenye tawi uliofungulia akaunti. Hela yako unachukua kwenye tawi lolote lile ili muradi data zako zinapatikana. Kwa hiyo tawi moja la benk likiungua una uwezo wa kwenda kuweka au kuchukua hela zako kwenye tawi lingine la benk hiyo hiyo au benk tofauti endapo utakuwa na master au visa card. Hofu ni kwa zile bank (sijui kama bado zipo) ambazo data za wateja zinatunzwa kwenye mafaili au vitabu au benk ambazo tawi moja halina uhusiano na matawi mengine
 
Mkuu majany umejibu vizuri sana, sema umetumia maneno ya kitaalam zaidi. Hoja ya mwanawao inamaana japo wengi wetu huwa hatupendi kuuliza vitu hata kama hatujui kwa kuona aibu.

Kwa uelewa wangu ni kwamba, benki inapopewa kibali cha kuendesha biashara huduma za kibenki nchini na BoT, huwa wanatakiwa kuweka kiwango fulani cha fedha BoT, hii ni pesa ambayo hawawezi kuichukua. Na BoT hufuatilia mwenendo wa benki husika na kuitaka iongeze kiwango hicho kutokana na fedha za wateja wake.

Kwa mantiki hiyo kiwango cha hiyo akiba hutofautiana kutoka benki moja hadi nyingine kutokana na kiwango cha fedha walizonazo na ukubwa wa benki.

Na jambo la pili, benki zinakua insured, na hawatakiwi kuwa na kiwango zaidi ya kile ambacho wamekubaliana na kampuni ya insurance na vilevile BoT wanakagua kuona hivyo viwango vinazingatiwa. Ndio maana kila mara utakuta mabenki yanaenda kuweka na kutoa hela BoT. Ni kosa benki kuhifadhi fedha zaidi ya kile ilichopangiwa au kukiwekea insurance.

Hadi hapo nadhani kama benki itapatwa na majanga, wateja wao wanakuwa na uhakika wakupata fedha zao.

Nadhani imeeleweka hata kama sio kwa kiwango ambacho muuliza swali alikitarajia, nadhani wadau wengine wataongezea.

Be blessed
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo benki inaweka hela BOT, au inakata BIMA ya wateja wake?
 
Umesoma hadi darasa la ngapi? kwa faida yako - Bank huweka dhamana BOT(BANK KUU YA TANZANIA) - Hawaruhusiwi kua na hela inayozidi kiwango hicho cha dhamana Tofauti kati ya bank zawa na ya kigeni ni gharama unazotozwa za kuhudumiwa bank Mfano: Eco-Bank wameingia na wamecut market price kwa huduma mbali mbali wanazotoa ili wateja kama ww mkimbilie huko -

Nadhani siyo sahihi kuhamua kutoa ushauri huku ukiwa umetanguliza kashfa. Aliyeuliza alitaka kujua na pengine kwa faida ya wasomaji wengine pia. mtu unaweza kuwa umesoma kwa kiwango ambacho wewe unaamini kuwa ukiitishwa mkutano wa wasomi na wewe utakuwa moja wao, lakini pamoja na hayo bado unaweza kuwa uko gizani kabisa kwenye nyanja nyingine na hivyo kuhitaji msaada wa mtu mwingine. Tubadilishe mitazamo hasi kwa jamii inayotuzunguka
 
Kwa hiyo benki inaweka hela BOT, au inakata BIMA ya wateja wake?

Soma kuhusu depositors insurance board....Maximum amount ambayo wanaweza kukurudishia ni 1,200,000/=,kwa hiyo at the moment benki ina collapse,let say ukiwa na sh.5m benki,hii bodi itakurudishia only 1,200,000/=....Hata hivyo mpaka benki ifilisike kuna kazi sana....Hebu soma historia ya Azania bank......!!
 
Kuungua moto-bank inakitu wanaita back up inakua different from HQ,so kila information za customer zitakuepo.
Bancrupt-am not sure
 
Soma kuhusu depositors insurance board....Maximum amount ambayo wanaweza kukurudishia ni 1,200,000/=,kwa hiyo at the moment benki ina collapse,let say ukiwa na sh.5m benki,hii bodi itakurudishia only 1,200,000/=....Hata hivyo mpaka benki ifilisike kuna kazi sana....Hebu soma historia ya Azania bank......!!

Mkuu, kwahiyo kama max ni 1.2M, na wewe uli deposit 5M.. imekula kwako? au wana uwezo wa kurefund the whole amount?
 
Back
Top Bottom