Tujuzane Je, Mbinu gani mnatumia kuwalipa ulinzi shirikishi mtaani kwenu ili kuepuka upigaji?

Tujuzane Je, Mbinu gani mnatumia kuwalipa ulinzi shirikishi mtaani kwenu ili kuepuka upigaji?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Ulinzi shirikishi ni jambo zuri sana!
Maeneo ya vijijini limeonyesha kufaulu kwa asilimia kubwa kutokana na watu wake kujitolea au kupangwa kwa zamu!

Tatizo kubwa la ulinzi shirikishi mjini una harufu ya upigaji!

Kuna wakati huwa nashawishika kuamini huenda PANYA ROAD ni PROJECT?
Kwasababu iweje kila siku tuwe na jibu moja tu la ULINZI SHIRIKISHI?

Halafu cha ajabu makamanda wa vyombo vya dola wanaoshauri ulinzi shirikishi makwao wanalindwa na polisi/jeshi! BURE

Usalama wa RAIA ambae hana silaha ategemee ulinzi shirikishi wa KULIPIA!

Anyway! Ngoja tujadili huo ulinzi shirikishi wenyewe

Mfano! Kama watendaji wa mtaa au wenyeviti wataamua kuchangisha ulinzi shirikishi mjini kila kaya Tsh 10,000/= kila mwezi uhakika wa makusanyo na matumizi utaonekana wapi?

Chukua mfano kata moja mjini ina kaya 1000 au zaidi maana yake makusanyo ya mwezi ni zaidi ya 10mil

Maswali.
1. Uhalisia wa mapato na matumizi ukoje?
2. Nani anawajibika na usimamizi wa fedha
3. Kama mwananchi atachangia pesa ya ulinzi harafu dirisha lake
likakatwa au kuibiwa je nani mwenye dhamana ya fidia?
4. Endapo mwananchi hana pesa au hawezi kuchangia ulinzi anafanywaje?
5. Mkataba wa uchangiaji una dhamana ipi kwa mwananchi?

HILI SWALA LA ULINZI SHIRIKISHI KINADHARIA NI JEPESI SANA LAKINI KIVITENDO NI CHANGAMOTO!

naomba tupeane mbinu gani mnatumia mtaani kwenu kujilinda!

Mawazo yangu vikundi vya ulinzi shirikishi vingesajiliwa na kulipwa na polisi wenyewe!

Je wewe UNASHAURI NINI?
 
Ulinzi shirikishi pasipo teknolojia ni changamoto pia,mtaa ni mkubwa mno,Ulinzi shirikishi hawana uwezo wa kuumaliza wote nakutoa huduma kwa uharaka ila wanasaidia kupunguza
 
ww toahiyo buku buku mengine hayakuhusu ukiibiwa tu mfokee balozi wako mpk kiekewwke maswala asielipa na anaelipa, sijui bajeti inatumikaje umeeambiwa tuko bungeni? pesa ndogo kazi kubwa unataka kuisakama.
 
Elfu kumi wewe uniona ndogo?
 
waongeze ajira na kuongeza vitengo ndani ya jeshi la polisi.
kuwa na kitengo cha askari kwa ajili mitaa na miji.
mbona wenzetu waliopo nje wanafanya hivi.
yani mimi mwenye familia nianze kuwa mlinzi tena wa mtaa wakati kodi inatafutwa tu
 
basi kusanya hiyo hela halafu weka ccctv camera na electronic door
ccctv kirefu chake nini! Nahisi unaleta kitu ambacho hukijui!
Turudi kwenye hoja
 
waongeze ajira na kuongeza vitengo ndani ya jeshi la polisi.
kuwa na kitengo cha askari kwa ajili mitaa na miji.
mbona wenzetu waliopo nje wanafanya hivi.
yani mimi mwenye familia nianze kuwa mlinzi tena wa mtaa wakati kodi inatafutwa tu
Inaweza kusaidia
 
Back
Top Bottom