Tujuzane kuhusu Trafiki na faini za elektroniki

Tujuzane kuhusu Trafiki na faini za elektroniki

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
5,818
Reaction score
5,555
Wanabodi, unasimamishwa na askari wa trafiki Kariakoo hana kitabu wala mashine ya elektroniki, anakukagua na kukwambia utalipia kosa fulani na kuwa kesho ukikutana na trafiki mwambie aku-printie risiti ukalipie. Unapofuatilia unakuta kweli umepigwa faini kwa kosa fulani, tiketi inasoma eneo la kosa ni Ubungo! Hivi hili liko sawa kweli kisheria na kimaadili ? Kwanini unapokamatwa na kutuhumiwa kosa akiwa hana mashine asikupeleke kituo cha karibu cha Polisi?

Vv
 
Back
Top Bottom