Tujuzane. Wataalamu wa kutibu meno wanapatikana wapi?

Tujuzane. Wataalamu wa kutibu meno wanapatikana wapi?

Setin

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2020
Posts
649
Reaction score
906
Habari wakuu,

1.Tujuzane hapa kama unawajua waganga wa asili wanaotibu meno,hasa fizi kuvimba na maumivu makubwa ya meno.

2. Dentists wazuri.

3.Hospitali nzuri za meno.

4. Dawa nzuri ya meno.

5. Njia zilizokusaidia.

Mawasaliano yao na bei zao.

Dogo hapa ana shida ya haraka.
 
@ Bsyotyo, skyEclat Jino tayari limeharibika, amengoa machache sasa anataka ayatunze yaliyobaki. Maji yamemwagika.

Wazee, mababu zetu walitumia mbinu gani, dawa gani za asili Hospitali gani, Dentist gani wazuri za uhakika?

Wengi nafikiri tayari kuna wakati mliumwa meno mlitumia mbinu gani?
 
Ukikutana na hawa dentists, utaambiwa dawa ya jino ni kung'oa, sasa utang'oa mangapi? Tambua safari moja huanzisha nyingine, ukiling'oa, utang'oa,utang'oa, utang'oa, hadi mwishowe mashavu yawe kama Kingunge au Bi Kidude.

Itafika mahali hadi ukijiangalia kwenye kioo, uwaze kuumbwa upya,maana kama ukija kufufuliwa na meno huna, utalia sana, bora uumbwe upya. Kidding.
 
@ Bsyotyo, skyEclat Jino tayari limeharibika, amengoa machache sasa anataka ayatunze yaliyobaki. Maji yamemwagika.

Wazee, mababu zetu walitumia mbinu gani, dawa gani za asili Hospitali gani, Dentist gani wazuri za uhakika?

Wengi nafikiri tayari kuna wakati mliumwa meno mlitumia mbinu gani?
Kwa meno yaliyotoboka na kuharibika huna ujanja nenda kwa dentist kuna tiba nyingi mfano root canal, crown, feeling pia unapata tiba kama umepata maambukizi.
 
Ukikutana na hawa dentists,utaambiwa dawa ya jino ni kung'oa,sasa utang'oa mangapi?.Tambua safari moja huanzisha nyingine,ukiling'oa,utang'oa,utang'oa,utang'oa,hadi mwishowe mashavu yawe kama Kingunge au Bi Kidude.
Itafika mahali hadi ukijiangalia kwenye kioo,uwaze kuumbwa upya,maana kama ukija kufufuliwa na meno huna,utalia sana,bora uumbwe upya.Kidding.

Huko vijijini kusipokuwa na Hospitali walikuwa wanafanyaje. Watu kama jamii ya Wamasai wanatibuje meno yao kiasili. Dawa gani wanatumia za mswaki?
 
Kwa meno yaliyotoboka na kuharibika huna ujanja nenda kwa dentist kuna tiba nyingi mfano root canal, crown, feeling pia unapata tiba kama umepata maambukizi.

Unaweza kutoa majina unayoyajua ya Hospitali, Dentist wazuri sio wababaishaji.
 
Huko vijijini kusipokuwa na Hospitali walikuwa wanafanyaje. Watu kama jamii ya Wamasai wanatibuje meno yao kiasili. Dawa gani wanatumia za mswaki?
Ndo hao tunataka majibu yao,siyo hawa madentists wa kisasa.
 
Ndo hao tunataka majibu yao,siyo hawa madentists wa kisasa.

Wote wakitupa majibu itakuwa vizuri zaidi. Wote wanakaribishwa.

Wamasai chakula chao kikuu ni nyama kuliko
mboga za majani. Huwa wanakabiliana vipi na hizi changamoto za meno.
 
Kama meno yashaoza ni option mbili.

Kwanza afanye root canal (hii ni kukata misuli/mishipa ya meno) so unakua hausikii maumivu.

Then ziba kwa risasi.

Hospital zipo nyingi inategemea na bajeti yako.

Serikali wapo mwananyama/muhimbili/temeke n.k

Binafsi

Agha khan
Sanitas
Regency
Dr. Meno pale moroco

Etc etc....

Dawa nzuri ya kutunza meno ni sensodyne ya pink imeandikwa for sensitive teath....

Njia za kienyeji wafuate wamasai ila at your own risk...
 
Mhandisi Mzalendo, Hospitali kama Muhimbili unaweza kwenda tu bila rufaa.

Hizi za private, unaweza kupata appointment siku hiyohiyo? Kwa maoni yako ipi ni nzuri kuliko zote MM? Sababu ameishaenda mbili, tatu dentist wanasema dawa ni kungoa tu.
 
Habari wakuu,

1.Tujuzane hapa kama unawajua waganga wa asili wanaotibu meno,hasa fizi kuvimba na maumivu makubwa ya meno.

2. Dentists wazuri.

3.Hospitali nzuri za meno.

4. Dawa nzuri ya meno.

5. Njia zilizokusaidia.

Mawasaliano yao na bei zao.

Dogo hapa ana shida ya haraka.
Kwa hali ya meno yako uliyotaja pamoja na tiba ifuatayo, unapaswa kuacha matumizi ya vyakula na vunywaji vya viwandani ikiwa ni pamoja na sukari.

Mahitaji:
(i) Unga wa mdalasini vijiko vitano vya chai
(ii) Unga wa karafuu vijiko vitano vya chai
(iii) Unga wa pilipili manga vijiko viwili vya chai.
(iv) Asali 250 mls (robo Lita).

Matayarisho:
Changanya vitu vyote vilivyokutajwa hapo uu na ukoroge vizuri kabisa.

Matumizi
Pigia mswaki dawa hiyo kutwa mara 2. Ikiwa meno yako ni mabovu sana basi mchanganyiko huu ndio uwe dawa yako
ya meno. Ikiwa jino lako limetoboka basi chukua dawa hii na uiweke kwenye tundu hilo.

Kila la kheri na utoe mrejeshonyuma
 
Mhandisi Mzalendo, Hospitali kama Muhimbili unaweza kwenda tu bila rufaa.

Hizi za private, unaweza kupata appointment siku hiyohiyo? Kwa maoni yako ipi ni nzuri kuliko zote MM? Sababu ameishaenda mbili, tatu dentist wanasema dawa ni kungoa tu.
Mimi nilienda Sanitas wakanirekebisha meno ya kibarazani.....

Muhimbili kuna private pale haihitaji rufaa.
 
mwengeso, @ Mhandisi Mzalendo, Asante.

Smart911, hata wewe unaweza kutoa muongozo, maoni yako. Ni mjadala huru, utakaosaidia wengi, kama wengi tutaweka michango yetu pamoja.
 
Watu wengi hudanganywa na waganga wa kienyeji pale jino linapouma kwa kuoza ama kutoboka, Yale maumivu Mali kama Kuna kitu kinatoboa kwa ndani huota ni mdudu.

Hata, baadhi ya madaktari wa meno huita general kuwa ni bacteria.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya kutosha kwa meno wanakokuita kuoza husabanishwa na asidi Kali izalishwaya tumboni( HCL) hiyo , ndio ikifanikiwa kuja mdomoni kwa sababu yoyote kama regurgitation au ruminant disorder ndio hu react na meno na kuyayeyusha ama kuanzia juu au pembeni. Hivyo mishipa ya fahamu ikishakuwa exposed ndio hayo maumivu Makali ambayo unsyasikia yanachoma kama msumari ndio huita mdudu, hivyo utafanyiwa mazingaombwe eti wanamtoa mdudu
 
Back
Top Bottom