Roulette
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 5,568
- 5,386
Wana JF,
nimegundua threads nyingi members wanaleta zinahusu matatizo na namna matatizo hayo yanasababisha matokeo katika maisha yao (au jamii, au taifa, ulimwengu etc), zaidi matokeo mabaya (negative impact). Na hili nimelikuta jukwaa karibu zote.
Ni kweli ni muhimu kuzungumzia matatizo na kuyatafutia suluhisho ila itasaidia zaidi kama tutaweza kubadilisha mtazamo wetu kutoka matokeo mabaya kwenda matokeo chanya. Najua Great thinkers wanatakiwa kutafuta suluhisho na ni lazima wajadili the negatives in order to bring the positive, ila nadhani ni muhimu kila mtu binafsi awe na positive attitude, hata kwenye negative circumstance, na hii huhitaji kubadilisha mtazamo wetu wa maisha.
Lengo la thread hii ni kusaidia kubadilika huko.
1. Kuna wakati (na hii hutokea sana) umeamka asubuhi na umepanga "goals" za siku. Ikifika jioni unagundua kuna vitu hukufanikiwa kutimiza na hii inaleta frustration, unaona kama siku hiyo imepotea. Unasahau kama kuna vitu ulitekeleza na kwa utekelezaji huo unastahili kujipongeza. Ukiwa na glass imejazwa nusu, usisemi liko half empty, sema liko half full.
2. Kuna watu wengi sasa hivi wamefikia hatua ya kutojua ni vitu gani wanapenda, ila wanajua na hutaja sana vitu wasivo vipenda. Kutambua vitu vyenye kukuletea furaha nido mwanzo wa kukaribisha furaha. Binafsi napenda sana kucheza na watoto karibu na maji (iwe maji ya mpira wakati wa kuosha gari, iwe beach, swiming pool au hata kwenye bath tube). Kazi yangu ni ya safari kwa hivo mara nyingi nashindwa kufanya hivi vitu ila kila niwezapo, nachukulia nafasi ya kuvifanya sana na baadae nikija kuvimiss nakumbukia na inatosha kurudisha furaha.
3. Kumbu kumbu ni kitu muhimu katika kukaribisha furaha maishani mwetu. Matatizo ni sehemu ya maisha na tunatakiwa kukabiliana nayo tukiwa na nguvu. Nguvu hiyo itatokea kwenye kumbu kumbu ya siku za furaha. Mfano, ukihisi hali ya upweke, kumbu kumbu ya siku ulikua na watu uwapendao inaweza kutosha kurudisha furaha moyoni. Sio kukumbuka na kusema: siku zile nilikua na watu ila leo niko peke yangu, bali nikukumbuka kua wakati ulipata fursa ya kufurahia kuwepo kwa watu uwapendao ulifurahia kwa kiwango kikubwa na furaha hiyo imebaki moyoni mwako ili uweze kuitumia utakapo wakosa karibu yako.
4. Sababu za kufurahi ni nyingi sana. Kuna watu wanasema maisha kwao hayana maana sababu wanahishi tabu tupu. Ukimuuliza ni tabu gani anasema mume wake anatembea nje, au anaumwa ugonjwa usio pona na kadhalika. Anasahau hicho kitu kinacho mnyima raha ni sehemu moja tu ya maisha, na wala sio maisha yenyewe. Uhai ni chanzo cha furaha. Kuona mbingu, ardhi na chochote ilicho kati ya mbingu na ardhi ni furaha. kua na afya ni furaha, kua na watoto ni furaha. Kula chakula, kulala ndani ya nyumba, kazi, marafiki, familia, imani nakadhalika, vyote vinaweza kua vyanzo ya furaha, kama utavitambua kua vinakufurahisha na kama utaamua kukaribisha furaha maishani mwako.
5. Kukaribisha furaha ni rahisi na hakuhitaji kua msomi, haihusiani na hali ya uchumi, jinsia, kabila au miaka, haichukui muda wako na haitegemei watu wa nje kuhusika (ingawa hii itasaidia). Kama nilivo sema mwanzo ni swala la kujiamulia, kujua ni vitu gani vinakuletea furaha na kutenda hivyo vitu kila uwezapo, ni kukumbuka vitu vinavyo kuletea furaha zaidi na kujifunza namna ya kuona positive zaidi ya negative katika maisha.
Vitu hivi vitasaidia kuanza kubadilisha mtazamo wako wa maisha na kukaribisha furaha maishani mwako, ila kuna mengine mengi unahitaji kufanya kwa kuimarisha furaha... Natumai kuna member atapost zaidi kuhusu kuimarisha furaha. Asanteni