CHADEMA walitaka kuwa na Katiba ambayo italeta misingi thabiti kwa taifa letu.
Kuwa na uchaguzi huru na wenye haki.
Kuwa na sheria madhubuti ambazo zingesimamaia uchaguzi huru. Mfano kuwa na nafasi ya kupinga matokeo ya urais ikiwa kuna mizengwe kwenye uchaguzi.
Hili la kusema waliweka mpira kwapani ni upotoshaji.
Makada wengi tu wa CCM akiwemo Diallo walishatamka wazi kuwa wizi wa kura huwa unafanyika nyakati za uchaguzi
Chadema wana hoja nzuri tatizo Bongo tunakuza sana vitu na mifano ni mingi
1. Wananchi wakitaka kuandamana, utasikia "Wanataka kuleta vita vya kisiasa" wakati ni maandamano tu ya amani
2. Wananchi wakitaka serikali ipinduliwe utasikia "Wanataka kuvuruga amani yetu"
Bongo hakuna amani maana watu wanatekwa sana, ila tu kuna uvumilivu"
3. Mtu akiwa mwanaharakati, kupinga tu serikali utasikia wanakuambia ni "Mhaini" mara sijui ni gaidi
4. Media hazipaswi kukosoa serikali, zikikosoa tu zipo hatarini, mfano mzuri Millard Ayo, watu wanamlaumu sana ila mimi namuelewa Millard, analinda career yake
5. Mwananchi ukikosoa serikali unatekwa. Hivi kweli maneno tu ndio yanafanya unateka mtu na kumuua. Kwa hiyo wewe kubaki madarakani kuna umuhimu kuliko maisha ya mtu?
Hii nchi haina demokrasia, na hakuna amani Tanzania ila kuna uvumilivu. Watz wameshazoea kuvumilia shida, ila viongozi wao hawawezi kuvumilia hata "kukosolewa" tu
Hii ipo kote, sio tu serikalini hadi nyumbani au shuleni uhuru wa kuzungumza unaminywa sana Tanzania. Hata shule ukimkosoa mwalimu pale anapokosea anakuambia unadharau walimu, sijui nini. Hata wazazi pia hawapendi watoto wao wawakosoe hata kama wanakosea, tunapenda sana ubabe na kukuza vitu Watanzania
Hata uongozi wa leo ni matokeo ya jamii yetu. Mkitufanya wananchi tuwe waoga wa kuexpress maoni yetu inakuwa si haki. Mnafanya tuendelee kuishi na maumivu moyoni, it's so tough to be in this position