Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

Pascal Mayalla, mimi ni mwanachama mkongwe wa JF, ingawa siku hizi si mchangiaji sana.

Nimekufahamu siku nyingi tangu wakati unaandaa vipindi vya kitimoto, na daima nimekuona mtu unayejua vema kazi yako ya uandishi wa habari, wakati huo huo ukiwa na mang'amuzi ya kina katika mambo ya kisiasa na kijamii. Mpaka sasa nakufuatilia makala unazoandika humu JF.

Leo umenifanya nirudi hapa kidogo kuchangia. Wengi waliochangia wamechukua upande mmojawapo au kukuballiana nawe au kupingana nawe huku wakitoa hoja zao (kama kawaida wengine wamekutukana). Mimi ninachangia bila kuchukua upande.

Nimesoma michango yote ya waliochangia Mpaka sasa, na kitu kimoja nimegundua ni kwamba unafuatilia michango ya wana JF kuhusu swala hili kwenye uzi huu uliouanzisha, kwa kuwa nimeona kila post kwenye thread hii ume like. Soon uta like na hii ya kwangu, nina hakika na hilo.

Mimi ninachangia kukushauri kama mtafiti. Hapa JF kwenye thread hii, mimi ninaona ni kama umeenda field kufanya utafiti wa suala la kijamii na kisiasa na umeuliza swali la kitafiti, ambalo mimi ninaliweka namna hii:
"Je hali ya chuki ya kisiasa na kijamii miongoni mwa Watanzania hivi sasa imesabishwa na nini?"

Swali lako hilo, ambalo halikutamkwa, limegusa wengi, na wengi wametoa maoni yao yenye hoja za kukubaliana na hypothesis yako, na wengine hoja za kutofautiana na hypothesis yako.

Ukitumia thread hii na kukusanya pande mbalimbali za maoni na sababu walizotoa, unaweza kuandika makala nzuri sana, (ingawa inaweza kukuweka matatani katika nia yako, kama ukiamua kuandika bila kupika habari).

Najua pia wako waandishi wengi wabobezi kama Akina mwanakijiji. Mtu yeyote anayetaka kuandika makala inayowakilisha maoni ya wananchi katika swali hilo, ana pahala pazuri pa kuanzia.

Kwa kuchokoza maoni hayo, nakushukuru sana ndugu yangu Paskali, ambaye nakuheshimu sana.

Mwanaukweli
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya tunayoyaona mitandaoni ni matokeo ya kupokea utandawazi bila tahadhari na kuangalia kipi chema tuchukue na kipi hakitufai tukiache. Tumekuwa na kizazi chenye akili nyingi za biskuti ambazo haziwezi kuhimili situations ngumu na zenye kuamua mustakabali wa nchi.

Ukiona mtu anaombea flani naye augue ili afe unajisikia aibu kwani ni sawa na kuona marehemu anayeongea. Na kama wasemavyo, kichwa kitupu ni karakana ya shetani hivyo usitegemee hekima na busara kutoka kwenye vichwa vitupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal, you are part of the problem,
a) Unalalamikia matokeo wakati chanzo chake unakijua, ulipaswa kushughulika na chanzo, reaction ya corona ni matokeo na chanzo chake ni dhuluma ambazo wananchi wengi wamefanyiwa, mifano unayo mingi.

b) Timing yako ni mbovu, kichekesho, na unafiki wa hali hali juu, siku zote watu wengi wamefanyiwa dhuluma umekaa kimya, leo ghafla umekuwa mtu wa kujali? Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

Kutokana na mwendendo ulivyokuwa unaenda watu walitabiri haya kutokea, tena hapo wananchi walio wengi wala hawana nguvu, ila wanaona timing ya corona kama mkombozi wao, je wangekuwa na nguvu, si ingekuwa hatari zaidi?

Ni kwei kwamba 'dua la kuku halimpati mwewe' lakini nilitarajia hili lingechukuliwa kama somo la kujifunza, kwamba kuna kitu mahali hakiko sawa, ili wahusika wajirekebishe, kwa kuuona ukweli, badala ya kuleta ubabe.

Hii iwe kama ujumbe kwamba kwanini watu wawaombee na wafurahie kuona viongozi wao wapendwa kutaabika
 
Happ mtoe Mwanakijiji ....!
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Kuwa mstaarabu,wewe ni mtu mzima na haya unayofanya ni utoto!Nani amekwambia tunataka kuona nyuzi zako ukurasa mzima wa JF?Unakera bhana,umeshafungua uzi ukatoa habari inatosha!Huu ni uhuni
 
Na Wewe pia mleta mada ni shetani,tena shetani mwenyewe rangi nyekundu na nyeusi kwa sababu ya kutetea watu wenye mikono yenye damu.
Nataman wafe hao unaowatetea sana.kwani na wao ni wauaji wakubwa tena ni mashetani wakubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

It’s time to stop the argument and:

- Protect your family and loved ones.
- Try to have some savings.
- Stop stress by reading articles like this.
- Turn to your faith and stay there.
 
Ndugu Pascal unahitaji utulivu na sisi sote. Kipindi ni kigumu, uzalendo haujengwi kwa bunduki kamwe. Mungu atupe hekima, tena sana. Wanasiasa hapa wamegawanyika kwenye makundi mawili, watawala ambao katiba inawalinda, na bunduki iko mikononi, wana uwezo wa kufanya chochote hata kama sheria haitawaruhusu. Wapinzani, katiba inawalinda hawana bunduki, hawa machozi yao huishia kwenye kuandika na kusema.Mungu wetu ailinde amani ya Tanzania na kumpa raisi wetu nguvu na hekima ya kuivusha nchi yetu salama.
 

Mkuu Pascal Mayalla una maoni yoyote kuwahusu hawa ndugu wanaosemekana kuhusishwa moja kwa moja na hawa makomando kwenye viroba?



Mung mkubwa, washukiwa wa haya sasa wanajulikana kwa majina na hata sura zao, mapema almaarufu - wasiojulikana.

Wasiojulikana Sasa Wajulikana kwa Majina ma Sura

Ama kwa hakika washukiwa hawa na vinara wao wote hai na wafu sasa wanajulikana.
 
Point tupu, bora anayeombea kuliko anayeua wenzake na kubambika kesi za kipumbafu
 
Pascal wewe ni mnajimu. Ulitabiri hili na likatokea kama ulivyolisema!! Ukijifanya jiwe, kuna wadudu wadogo wadogo wasioonekana kwa macho wanakufanya jiwe kweli lisilosikia kitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…