Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Nashindwa kuelewa kwanini TRA wanashindwa kuiga kwa Ruto wa Kenya na kuongeza mapato kutoka katika wimbi hili la mitume na manabii walioanzisha biashara ya Maji, chumvi, vitambaa nk wakiviita vya upako na kupata fedha nyingi sana kama biashara isiyo kodi wala cost of production. Msome Rais Ruto alivyoamua.

"Nimeongea na watendaji wa serikali yangu kuhusu baadhi ya wahubiri kucheza na imani za wakenya. Kuanzia sasa yule anataka kuuza maji asajiliwe na mamlaka ya maji, yule anataka kuuza mafuta asajiliwe na food and drugs authority, na yule anataka kuuza mbegu asajiliwe wizara ya kilimo. Watambulike kama wafanyabiashara, na serikali ijue wanauza ngapi kwa siku na walipe kodi. Huku kwa kanisa wabaki wanaoeneza neno la Mungu, sio wafanyabiashara. Hatuwezi kuruhusu imani za wakenya kuchezewa na wakora wachache, wanaotaka kujitajirisha kupitia shida za waumini wetu" William Samoei Ruto, Rais wa Kenya.
 
Hao jamaa ni wafanyabiashara waliojificha kwenye kivuli cha imani, tena ni wafanyabiashara wakubwa tu wanaotakiwa kulipa kodi.

Kwenye makanisa yao wanauza maji, mafuta, biskuti, TRA kazi kwenu, sasa Ruto ameshawaamsha usingizini.
 
Hali peke yake hiyo hela. Kuna wakubwa kibao nyuma ya utapeli huo.

Unajua sababu ya nabii Suguye kufungiwa? Nitafute inbox nikujuze.
Haya mambo uliyoandika yanahitaji ushahidi, na wala hakuna sababu ya kutafutana inbox, kwani hii ndio JF - A place where we dare to talk..

Huko kutafutana inbox ni kuendelea kukuza tatizo, kwasababu mnapeana taarifa za uozo kwa siri ambapo mamlaka husika hazitaweza kuziona na kuzifanyia kazi.
 
Kodi inatozwa kwenye mapato ya:
1. Business
3. Employment
3. Investment

Sasa tukija kwenye tafsiri business income as per Income Tax Act (ITA) unakuta akina mwamposa and co, wako nje ya wigo wa hiyo tafsiri ( out of scope)

Kodi haitozwi kwa hisia...Kodi inatozwa kwa sheria ambazo ziko challenged mpaka kwenye court of appeals kama kuna mzozo.

Sasa wakati wa utunzi na utafsiri wa sheria ya Kodi words must strictly construed and clearly stated.nje ya hapo hiyo sheria haitafanya kazi.

SASA NIAMBIENI MODALITIES YA HIYO SHERIA ITAKAAJE KIASI KWAMBA ITAMKAMATA MWAMPOSA IACHE SADAKA ZA KAWAIDA KANISANI na Msikitini
 
Haya mambo yanahitaji ushahidi, na wala hakuna sababu ya kutafutana inbox, hii ndio JF a place where we dare to talk..

Huko kutafutana inbox ni kuendelea kukuza tatizo, kwasababu mnapeana taarifa za uozo kwa siri ambapo mamlaka husika hazitaweza kulifanyia kazi.
..."we dare talk openly"..!
 
Kodi inatozwa kwenye mapato ya:
1. Business
3. Employment
3. Investment

Sasa tukija kwenye tafsiri business income as per Income Tax Act (ITA) unakuta akina mwamposa and co, wako nje ya wigo wa hiyo tafsiri ( out of scope)

Kodi haitozwi kwa hisia...Kodi inatozwa kwa sheria ambazo ziko challenged mpaka kwenye court of appeals kama kuna mzozo.

Sasa wakati wa utunzi na utafsiri wa sheria ya Kodi words must strictly construed and clearly stated.nje ya hapo hiyo sheria haitafanya kazi.

SASA NIAMBIENI MODALITIES YA HIYO SHERIA ITAKAAJE KIASI KWAMBA ITAMKAMATA MWAMPOSA IACHE SADAKA ZA KAWAIDA KANISANI na Msikitini
Sheria hushuka au hutungwa na kurekebishwa kulingana na uhitaji?Sijajua unataka kukwepesha nini?
 
Sheria hushuka au hutungwa na kurekebishwa kulingana na uhitaji?Sijajua unataka kukwepesha nini?
Hoja iko hivi?
Kodi hutozwa kwenye mambo matatu tu yaan, business, investment, employment. Chochote nje ya hapo hakitozeki Kodi (out of scope)
Sasa unatakiwa uje na sheria itakayosema na iwe strictly construed ili inmase mwamposa.
No intendment in tax laws, words must clearly be stated.
SASA EBU NISAIDIE HIYO SHERIA ITAKAAKAJE KIASI KWAMBA SADAKA AU MICHANGO kanisan itofautishe na mambo ya mwamposa?
Utaishia kutunga sheria mfu kwan haitaweza kufanya kazi.

Inatakiwa hivi unapowashtaki mwamposas useme ni kivipi arrangement ya transactions zake za maji na mafuta namna ambavyo fall within tax laws na sio kihisia.

Sasa mwamposa si atasena toeni sadaka nitawagawia maji MUNGU alioniruhusu niwagawie...
Wale wa 5,000 watapewa maji , chin ya hapo hatawapo ...hajairuka sheria yeyote
 
Back
Top Bottom