TRA na Bunge kama posho zao hawakatwi kodi it is wrong same kwa mapadre ,masista na mabruda wa kanisa katoliki kama hawakatwi kodi posho zao it is wrong
Acha kuwa kipofu na Mwalimu na Kiongozi Wa Vipofu mwana Wa uasi na wakili Wa Shetani katika nyakati hizi za Kuelekea kujifunua Kwa yule Mwasi na mpinga Kristo.
Mapadri na wachungaji na Hao masister uliowataja wanalipwa Kwa pesa ambazo ni Sadaka za waumini Wao au wanachama Wao. Ningeingia madarakani Taasisi zote za Dini ningezipa ruzuku kama vyama vyama vya siasa na NGO nyingine KWENYE jamii . Lakini sifa ni lazima Dini zijiendeshe kama taaisisi SIO Mali ya MTU na familia yake Huku AKIWA anafanya Biashara ya kuuza bidhaa za viwandani Kanisani.
Mishahara ya watumishi Wa makanisa yanayojiendesha kitaasisi inatokana na sadaka.
Sadaka ni Kile wanachotoa waumini kutokana na vipato vyao ama ni mishahara au ni faida kwenye biashara zao . Wakajinyima Kwa misingi ya Imani na maelekezo ya Biblia na Kwenda KUTOA Sehemu Kwa ajili ya KAZI ya MUNGU hapa Duniani na Kwa ajili ya kupata tahawabu Mbinguni Kwa misingi ya Imani ya Kikristo au Hata kiislam na karibu Imani zote .
Wanachokipata kutoka Kwa watumishi Hao wanawatumikia ni mafundisho ya KIROHO na kurudi Nyumbani Wakiwa na Imani rohoni na SIO kurudi Nyumbani Wakiwa wameuziwa bidhaa na kuwa ndicho walichokipata KWENYE Ibada Kanisani. Ajabu ZAIDI inakua ni bidhaa inayouzwa Kila Siku ya Jumapili na kurudi nayo Nyumbani mikononi Huku rohoni pakiwa pamejaa Chuki,uongo,tamaa mbaya , uadui, tamaa ya Fedha na roho mbaya.
Sasa Sadaka hizo zinapatikanaje Kwa Waumini ?
Kwama ni waajiri au Mabwana wakubwa na waajiriwa au watumwa Wa umma wanaoitwa watumishi Wa Umma ni Baada ya mishahara Yao kuwa imeshakatwa Kodi na Kwenda SERIKALINI ,Sasa wanakwenda Kanisani kumshukuru Mungu Kwa Sehemu ya Kile kiasi kilichobaki Ili KAZI ya Mungu ifanyike.
Kama ni matajiri au wafanyabiashara nao ni hivyohivyo. Wanaangalia faida Yao na Kwenda Kanisani kumshukuru Mungu Kwa Kutoa Sadaka . Kweye hizo Sadaka Bado Kuna Sehemu ya kusaidia yatima na wajane Kama Dini yeyewe Kama taasisi inavyoelekeza na Mungu alivoelekeza SIO matakwa ya MTU kujitajirisha mwemyewe na familia yake Huku AKIWA amesajili kanisa mama Mali yake na MKE wake.
Tofauti na Biashara ya Kwenda Israelí au Uarabuni na Kununua majivu au mafuta yanayotumika KUTOA majini au Kununua makontena ya vitambaa vya hengachifu na Kwenda kuviuza Kwa Bei ya juu kuliko iliyoko kwenye soko la wafanyabishara Wa mitaani.
Vitambaa tiba au Maji tiba au Chumvi na sabuni tiba hizo zinaletwa Kama bidhaa ya MTU na kuuzwa Kwa Bei ya faida Kwa wazi kabisa Kwa maelfu ya pesa na wanapopata faida wahusika wanajiingiza kwenye maisha ya Anasa na ufahari mkubwa kama kuliko wafanyabishara wanaolipa Kodi kwenye Biashara za bidhaa kama hizo.
Hiyo SIO Sawa tuache kushabikia uovu na kulinajisi kanisa la Kristo na nguvu zilizoko damuni mwa mwanakondoo Wa Mungu.
Damu ya Yesu ilipomwagika na kuingia ardhini ilitakasa vitu vyote kama ilivyokuwa mwanzo wakati Wa uumbaji na Yesu akawa mzaliwa Wa kwanza alipofufuka.
Hivyo hakuna bidhaa yoyote inayoweza kumsaidia Kristo kuondoa magonjwa Wala laana Wala mikosi ZAIDI ya Damu yake ,Neno na roho Mtakatifu. Yeye ni Chakula Cha úzima,yeye ni kafara ya Kila kitu,yeye ni Maji ya úzima yeye ni njia , yeye ni kweli , yeye ni Jehova Rafa Yaana mponyaji ,yeye ni mwokozi Wa kuokoa katika shida zote za wanadamu.
Tuwafundishe wanadamu mambo haya makuu yanayopatikana ndani ya Krsto YESU na SIO vitambaa vinavyotengenezwa kwenye viwanda vya wachina na shabuni za viwanda vya wahindi na chumbu za kuokota kwenye Maji ya baharini.
Tuondokane na mafundisho manyonge ya vitambaa na Sasa tuhubiri nguvu za Damu ya Yesu Kristo mwanakondoo Wa Mungu aliyeichukua dhambi ya Ulimwengu .Sadaka ya milele.