Nakubali 100 kwa 100. Hawa wanaojiita manabii na mitume wamegeuza dini kuwa biashara. Hakuna kuhubiri neno la mungu ila ni kukusanya sadaka na mafungu ya kumi. Tena yanakusanywa mabilioni kila siku bila ya risiti wala kodiNashindwa kuelewa kwanini TRA wanashindwa kuiga kwa Ruto wa Kenya na kuongeza mapato kutoka katika wimbi hili la mitume na manabii walioanzisha biashara ya Maji, chumvi, vitambaa nk wakiviita vya upako na kupata fedha nyingi sana kama biashara isiyo kodi wala cost of production. Msome Rais Ruto alivyoamua.
"Nimeongea na watendaji wa serikali yangu kuhusu baadhi ya wahubiri kucheza na imani za wakenya. Kuanzia sasa yule anataka kuuza maji asajiliwe na mamlaka ya maji, yule anataka kuuza mafuta asajiliwe na food and drugs authority, na yule anataka kuuza mbegu asajiliwe wizara ya kilimo. Watambulike kama wafanyabiashara, na serikali ijue wanauza ngapi kwa siku na walipe kodi. Huku kwa kanisa wabaki wanaoeneza neno la Mungu, sio wafanyabiashara. Hatuwezi kuruhusu imani za wakenya kuchezewa na wakora wachache, wanaotaka kujitajirisha kupitia shida za waumini wetu" William Samoei Ruto, Rais wa Kenya.
Je TRA inalijua hili au ni kuwakamua wananchi kwa tozo na VAT
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi ni msemo usio na maana yeyote wakati hawa manabii uchwara wanatajirika bila ya kulipa kodi
Tujifunze kutoka Kenya