Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Umeandika mengi kitaalamu,sawa.Kumbuka hapo tujikite kwenye kuuza bidhaa.Hayo mengine baki nayo tu.Auze for free?Bila tozo?Kwa nini uiweke akili yako kuwa stugnant kwamba sheria ya kumtoza kodi haitungiki?Umekwama kabla ya kujishughulisha kutafuta aina ya kodi?Na usijikite kwamba kuna kodi fulanifulani tu.Zinaweza kuongezwa muda wowote
 
Yale maji, chumvi au vitambaa ni sadaka au biashara?
Na unadhani kule Kenya mpaka katamka vile (mind you jamaa ni mlokole) hakuifahamu sheria ya kodi kama wewe unayefahamu zaidi?
 
Yale maji, chumvi na vitambaa ni Business na watapaswa waombee leseni ya kuuza
 
Kafungue na wewe uuze na utoe kodi kama ni rahisi. Kuwa weka watu na kuwa na furaha ya moyon ni zaid ya kodi
Akili ya mwafrika ndio tatizo lake. Na huu umaskini unatumiwa na hao wahubiri wa dini kwa kujitajirisha.

Kagame alitumia akili kubwa sana kuwapa masharti ili makanisa yao yakubaliwe Rwanda.

Wanautumia ujinga wa wengi wetu kujitajirisha hawana msaada wowote katika kuleta afadhalii ya kimaisha ni wapigaji tu.
 
Yale maji, chumvi au vitambaa ni sadaka au biashara?
Na unadhani kule Kenya mpaka katamka vile (mind you jamaa ni mlokole) hakuifahamu sheria ya kodi kama wewe unayefahamu zaidi?
Rais SAMIA alisema msidai mkokotoo audit & examination za miaka zaidi ya miwili nyuma.
TRA mpaka leo wanafanya miaka mitano. Kisa haipo kwenye sheria.
Ruto mlokole ni kweli, ametamka ni sawa, sasa Kodi inahitaji Sheria na ndicho kinachosubiriwa ili Tanzania nayo iige.
IGUMU NI MODALITIES YA HIYO SHERIA ili isigeuke Sheria hewa.
Mfano:
Mwamposa akisema nagawa maji bure ila njoo na sadaka ya kuanzia 5,000
Nagawa komunyoo bure ila njoo na sadaka
Sasa hapo utatofautishaje sadaka sadaka na sadaka biashara kisheria?
 
Sacraments pia za wakatoliki nk wawe wanalipa kodi huwa makanisa yananunua kwa wanaotengeneza hizo sakrameni
Sacraments ni tofauti na huo utapeli wa wachungaji feki, huuziwi sacrament kanisani unainunua kwa kutoa sadaka mbalimbali. Mapadre wanaishi kwa sadaka zetu za kila misa.

Padre akitaka kununua laptop au kifaa chochote anayo haki ya kuwaambia waumini na wakamnunulia ndio maisha ya useja hayo.

Tofauti na haya makanisa yanayotumia ujinga na ufukara wa waumini katika kutajirisha wachache.

Ni kanisa katoliki lina nidhamu ya uendeshaji na usimamiaji wa kila kinachofanyika huwezi kulinganisha na hayo makanisa ambayo ni mali za watu binafsi.
 
Uongo yanalipiwa kodi

Hatengenezi nyumbani kwake ujue
YEHODAYA hebu ngoja kidogo, viwanda vya maji vinalipa kodi kama kawaida na yeye ananunua huko.
Lakini kifuatacho naye anauza nasikia yale maji ya elfu moja anauza elfu 5 mpaka 10. That's where tunasema faida hiyo iwe taxed.
Tupo pamoja mkuu? Hata maduka yetu ya mtaani faida yao ya kuuza maji inatozwa kodi.
 
Sacraments pia za wakatoliki nk wawe wanalipa kodi huwa makanisa yananunua kwa wanaotengeneza hizo sakrameni
Umeona ugumu wa modalities ya hiyo sheria utakavyokuwa?
Watu wanatoa sadaka wanapewa komunyoo, je hiyo utatofautishaje na watoa sadaka kwa maji?
Ndio maana mamlaka za mapato zinashindwa kuwa na sheria kwenye hili
 
Sasa mwamposa si atasena toeni sadaka nitawagawia maji MUNGU alioniruhusu niwagawie...
Wale wa 5,000 watapewa maji , chin ya hapo hatawapo ...hajairuka sheria yeyote

Hapo maana yake ni pure biashara,maji yatakuwa yanauzwa kwa 5,000.Sadaka huwa haina kiwango.Kwanini kama ni sadaka basi asiwape hayo maji hata waliotoa shs 100 maana zote ni sadaka.
 
Umeona ugumu wa modalities ya hiyo sheria utakavyokuwa?
Watu wanatoa sadaka wanapewa komunyoo, je hiyo utatofautishaje na watoa sadaka kwa maji?
Ndio maana mamlaka za mapato zinashindwa kuwa na sheria kwenye hili
Kanisa lina utaratibu wa uendeshaji wenye kueleweka kumbuka kanisa katoliki limekuwepo kabla ya uhuru hapa Tanzania huwezi kulinganisha na hayo makanisa yenye anwani za watu binafsi.

Fungukeni akili ili mpige vita huo wizi unaofanywa na hao wachungaji.
 
Hiyo transaction haina business value, it is not a transaction of business nature. MAJI YA 1000 kwenye jua la Kawe unayanunua 10,000 is it a business arrangements? Kwa nin nisinunue kibanda jiran kwa buku.
Kikodi hiyo transaction haina mashiko, the same to mtu ananihubiria Kisha natoa sadaka ya 1000,5000 au laki .

Kwa kutumia Kodi huwezi kuwazuia mwampsa and co, labda upige marufuku kama rwanda
 
Sacraments pia za wakatoliki nk wawe wanalipa kodi huwa makanisa yananunua kwa wanaotengeneza hizo sakrameni
Sacraments haziuzwi.Utauzaje Sacrament ya Kipaimara ,ubatizo au Komunio? Kama ulimaanisha ile ekarist wanayokula hizo zinatengenezwa Kanisani na masister,huwezi zikuta ziko zinauzwa dukani kama maji,chumvi na mafuta.
 
Mnasukumwa na chuki tu dhidi ya Mwamposa hamna zaidi ya hilo.
 
Mwamposa akisema nagawa maji bure ila njoo na sadaka ya kuanzia 5,000
Nagawa komunyoo bure ila njoo na sadaka
Sasa hapo utatofautishaje sadaka sadaka na sadaka biashara kisheria?

Biashara iko hapo kwa hiyo kauli.Kwanini uwapangie watu sadaka kiasi flani kama siyo kusema hiyo ndiyo bei ya maji,mafuta na komuniyo? Ulishaona Wakatoliki wanapangiwa watoe kiasi flan kwanza cha pesa ili wapewe komuniyo au waumini wote huwa wanapewa na haichaguwi umetoa sadaka ama hukutoa.
 
Ndugu mim mwenyewe ni mkatoliki charismatic.

Napinga uuzwaji wa nguvu za MUNGU.
NACHOELEKEZA NI UGUMU WA MODALITIES YA HIYO SHERIA UTAKAVYOKUWA

Kwa mfano schools, University zinalipa Kodi ambazo ni cooperate income tax, PAYE kwa employees wake and most of indirect taxes?

Sasa mapadre na masister wanalipishwa PAYE? Sio waajiriwa na hii taasisi ...hawana kipato ambacho ni sadaka zetu?
Hatutoi sadaka kwenye jumuiya, kanisan kwa ajili ya hawa masister na fathers? Je wenyewe sio wakaazi wa hii nchi mbona hawakatwi PAYE? Kama hawana wapatacho wanaishije, wanavaaje, wanakunywaje?wanakazi au biashara gan za ziada kuwawezesha kuishi?
 
Hao jamaa ni wafanyabiashara waliojificha kwenye kivuli cha imani, tena ni wafanyabiashara wakubwa tu wanaotakiwa kulipa kodi.

Kwenye makanisa yao wanauza maji, mafuta, biskuti, TRA kazi kwenu, sasa Ruto ameshawaamsha usingizini.
Tra ya Tsz sijui walisomea shule wap? Vyanzo vyao vya Kodi Ni vilevile miaka yote. Hata hili la makanisa hawatalifanyia kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…