Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
MBOLEA zinazotumika Katika kilimo ni moja ya kemikali zinazozalishwa kwa kuibadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA katika nchi zilizo endelea. Hivyo kilimo cha Tanzania kinaweza kufaidika sana kama tukianzisha kiwanda kikubwa cha kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2013, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo kwa zaidi ya robo moja ya Pato la Taifa (27-32%). Kilimo kinatoa 85% ya bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi na kinaajiri 80% ya nguvukazi nchini.
Tanzania huaagiza 90% ya MBOLEA kutoka nje ya nchi, 10% iliyobaki huzalishwa ndani. Lakini pia, MBOLEA inayozalishwa ndani inafaa kwa udongo wenye tindikali (asidi) tu.
MBOLEA YA UREA ndio mbolea inayotumika zaidi nchini ikichukua zaidi ya 33% ya jumla mbolea zote nchini. Na matumizi ya mbolea yanazidi kupanda kila mwaka.
Kama tukianzisha kiwanda cha kuzalisha tani 2300 za AMMONIA kwa siku na tani 4000 za UREA kwa siku (sawa na tani milioni 1.3 za urea kwa mwaka), kiwango hiki kitaweza kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kiasi cha mbolea inayobaki katika masoko ya kikanda na kimataifa. Mradi wa mbolea unaweza kufanikiwa katika uwekezaji mdogo tu.
Prosesi za kuibadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.
Hatua ya kwanza kabisa gesi asilia (CH4) itabadilishwa kuwa AMMONIA hapo kuna miungano mbalimbali ya kikemikali itafanyika kwa kutumia vichocheo. AMMONIA yenyewe ni mbolea tayari.
Baada ya hapo AMMONIA itabadilishwa kuwa MBOLEA YA UREA kwa kutumia miungano ya kikekimali.
Lakini pia kutoka kwenye AMMONIA tutafanya miungano mingine ya kikemikali kupata mbolea zifuatazo; AMMONIUM NITRATE (NA), AMMONIUM SULPHATE (SA), AMMONIUM PHOSPHATE (PA).
Kutoka kwenye AMMONIUM NITRATE (NA) tutafanya miungano ya kikemikali na kutapata mbolea ya CALCIUM AMMONIUM NITRATE (CAN).
Kutoka kwenye AMMONIUM PHOSPHATE (PA) tutapata mbolea ya MONOAMMONIUM PHOSPHATE (MAP), na DIAMMONIUM PHOSPHATE (DAP).
Jedwali hili hapa chini linaonyesha matumizi ya mbolea mbalimbali Tanzania.
Mchoro huu wa chini unaonyesha hatua za kuibadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA ya AMMONIA.
Mchoro huu wa chini unaonyesha mbolea tutakazo zipata kutoka kwenye AMMONIA baada ya kufanya miungano mingine ya kikemikali.