Tukiibadilisha Gesi Asilia (CH4) iliyopatikana Tanzania kuwa Mbolea za kilimo tutainua uchumi wa nchi

kuanzisha kiwanda kama hiki maana yake ni kuua mrija wa watu hapo,tuache kuagiza mbolea nje? harafu wapigie wapi mbwa gizani? mambo hayahaya ndio yapo kwenye sukari na mafuta ya kula kwenye hivyo vitu vitatu ndio mahali mbwa huwa anapigiwa gizani.
 
Hii sahau chini ya serikali ya CCM
 
Kulikuwa na mwekezaji toka Ujerumani kwenye mradi huo wa mbolea na hiyo gesi, naona kampuni hiyo ilikwishajiondoa baada ya kutoonekana maendeleo yoyote kuhusu gesi yenyewe.
Dangote anajenga kiwanda cha mbolea , kuna uwezekano atatuma gesi kama malighafi ya kuzalishia maana sasahivi anapata gesi kwa ajili ya kuzalishia nishati
 
Dangote anajenga kiwanda cha mbolea , kuna uwezekano atatuma gesi kama malighafi ya kuzalishia maana sasahivi anapata gesi kwa ajili ya kuzalishia nishati
Sioni tatizo na hilo ili mradi tu maslahi ya nchi yetu yazingatiwe kiweledi kabisa.
 
kuanzisha kiwanda kama hiki maana yake ni kuua mrija wa watu hapo,tuache kuagiza mbolea nje? harafu wapigie wapi mbwa gizani? mambo hayahaya ndio yapo kwenye sukari na mafuta ya kula kwenye hivyo vitu vitatu ndio mahali mbwa huwa anapigiwa gizani.
Tukifanikiwa vyema kuwaminya matapeli waliomo kwenye bidhaa hizo na nyingine kadhaa tutafanikiwa vyema kuijenga Tanzania yenye neema.

Hili kundi ndilo sumbufu sana katika kuhujumu juhudi za wananchi.
 
Muda mrefu sana dangote alipanga kujenga kiwanda cha mbolea wakati wa awamu ya nne , ilikuwa akimaliza kujenga kiwanda cha saruji ajenge cha mbolea
Viongozi tuliowachagua wajitahidi kuyaona haya.
 
Tukifanikiwa vyema kuwaminya matapeli waliomo kwenye bidhaa hizo na nyingine kadhaa tutafanikiwa vyema kuijenga Tanzania yenye neema.

Hili kundi ndilo sumbufu sana katika kuhujumu juhudi za wananchi.
Matapeli ni wengi sana na hao ndio wanao kwamisha maendeleo.
 
Professor wa msoga alikula cha juu akawagawia wachina!

Je, wakulima wetu wa kipato cha chini wataweza kumudu bei ya mbolea zitakazozalishwa?
Wataweza kumudu kwasababu zitazalishwa hapahapa nchini hivyo zitauzwa kwa bei ya chini.
 
Kwa nadharia ni wataalamu lakini vitendo ni ziro inawezekana hatukiamini tulicho jifunza tulishinda mitihani tupate vyeti
 
Wataweza kumudu kwasababu zitazalishwa hapahapa nchini hivyo zitauzwa kwa bei ya chini.
Inabidi kufanya analysis ya kutosha kujua kweli kama gharama za uzalishaji zitakuwa chini compared to imported fertilizers ili kuwezesha kitakachozalishwa kushindana kwenye soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…