Tukikamilisha miradi ya Stiegler's Gorge na SGR pekee. Ona habari hii na fanya hesabu kuhusu sisi kuendelea kukopesheka na utathimini tunaelekea wapi

Tukikamilisha miradi ya Stiegler's Gorge na SGR pekee. Ona habari hii na fanya hesabu kuhusu sisi kuendelea kukopesheka na utathimini tunaelekea wapi

Chanzo cha habari yako ndiyo tatizo
Problem ya nyie mnaopenda kusifia hivi vitu, mnapita hata ile element ya stupidity, kwa hiyo nimekudanganya, haya soma hii

Egypt’s Elsewedy, Afreximbank ink USD 500 mn loan agreement
Elsewedy, Afreximbank ink USD 500 mn loan agreement: Elsewedy Electric signed a USD 500 mn loan agreement with the African Export-Import Bank (Afreximbank) to finance its projects in Africa, Elsewedy marketing director Ahmed Hassouna said, according to Youm7. The funds will go toward the USD 3 bn hydroelectric dam in Tanzania, for which the final contracts will be signed today. Prime Minister Moustafa Madbouly is heading to Tanzania for the project’s signing ceremony, while Tanzanian President John Magufuli announced he will sign the Tanzanian dam project this week. Elsewedy will also direct the funding to an electricity generation equipment factory in Uganda, on which it is set to break ground next year. Elsewedy Electric and partner Arab Contractors will sign the USD 3 bn agreement today, Hassouna add
 
  • Thanks
Reactions: ffn

Jibu umeleta mwenyewe, kumbe wanakuja na financing yao wenyewe.
 
Again level ya stupidty inaendelea usd 500 against 6.5 trillion means equal
Partial.

Unafikiri mradi mkubwa kama huo financing inatoka sehemu moja tu au yote kwa moja?

Hivi hizo shule huwa mnaenda kufanya nini? Kusomea ujingaaaaaaa?
 
Tayari el sewedy jusi wamekopa usd 500 million kuanza huu mradi, unless serikali ya egypt huko mbele watakusamehe, angekuwa mzungu ningekuwa na uhakika , deni liko pale pale acheni uongo
Thibitisha , sio kuleta porojo hapa
 
Hilo ndiyo jibu. Madeni yatakuwepo na umeme utakuwepo na malipo yatafanyika.

Life goes on.

Ushindwe kulipa deni la chini ya 2t kwa miaka kibao, ndio uweze kulipa 6.5t? Kibaya zaidi hawa marais wetu huwa wanakopa kusaka sifa za kisiasa bila kujali huko mbele wanaokuja kama wataweza kulipa. Mfano halisi ni huo mradi wa gas, kakopa JK kwa Madaha, saa hii deni haliijalipwa na Magufuli kaamua kuachana na gas kaenda kukopa mradi wa umeme wa maji!
 
Mradi huu utakuwa na mkataba wa uendeshaji na usimamizi. Nahisi hivyo.
 
Kama kweli Magufuli atajenga SGR yote niko tayari akope ata trillion 100. Katika kitu ambacho nataman kikamilike ni hii SGR. Pia akiboresha na reli ya Tanga-Arusha na mwendelezo wake toka Arusha hadi mara niko tayari kutoa sadaka ka hela kangu nilikokusanya PPF.
Ila akifanya ununuzi wa wapinzani sitamwelewa...
Unatumia makwapa kufikiri?
 
Hilo ndiyo jibu. Madeni yatakuwepo na umeme utakuwepo na malipo yatafanyika.

Life goes on.

Ushindwe kulipa deni la chini ya 2t kwa miaka kibao, ndio uweze kulipa 6.5t? Kibaya zaidi hawa marais wetu huwa wanasaka sifa za kisiasa bila kujali huko mbele wanaokuja kama wataweza kulipa. Mfano halisi ni huo mradi wa gas, kakopa JK kwa Madaha, saa hii deni haliijalipwa na Magufuli kaamua kuachana na gas kaenda kukopa mradi wa umeme wa maji!
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Mradi huu utakuwa na mkataba wa uendeshaji na usimamizi. Nahisi hivyo.

Endelea kuishi hivyo hivyo kwa kuhisi. Kilichoshindikana kwa miradi mingine ni nini, na sasa malaika wanatoka wapi ndio hapo. Wenzio wanataka mitaji ya kisiasa kulipwa au kutokulipwa haipo kwenye vichwa vyao kwani watakuwa wamestaafu hivyo haiwahusu, anayekuja atapambana na hali yake.
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Jumatano iliyopita, Kampuni ya Arab Contractors ya Misri na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), walisaini mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme kwenye Mto Rufiji, maarufu kama Stiegler’s Gorge. Utilianaji huo wa saini ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, walikuwa mashuhuda wa utilianaji huo wa saini. Kukamilika kwa Stiegler’s Gorge kutaifanya Tanzania kuwa na umeme mkubwa, wenye kutosheleza nchi na zaidi tena kwa bei nafuu.

Mradi wa Kinyerezi ulipokamilika mwaka juzi, taarifa ya Tanesco ilieleza kuwa mahitaji ya umeme yalitimia kwa asimilia 100. Ilielezwa kwamba Kinyerezi inazalisha megawati 150, hivyo kufikisha megawati 1,500 ambazo ndizo mahitaji ya nchi kwa sasa.

Hata hivyo, hali halisi ya umeme kwa sasa, jinsi umeme unavyokatika mara kwa mara, huku nishati hiyo ikionekana kuwa si ya uhakika, ni dhahiri kuwa kiwango cha umeme kilichopo hakitoshelezi. Ama uwezo wa mitambo ya ufuaji ni mdogo au njia za upitishaji wa umeme zimezidiwa.

Stiegler’s Gorge ikikamilika, itaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2,100. Kwa hesabu ya Tanesco mwaka juzi kuwa mahitaji ya nchi ni megawatt 1,500, maana yake, mradi huo ukikamilika, itawezekana hata kuzima mitambo mingine yote na kutumia umeme wa Stiegler’s Gorge na mwingine utabaki.

Mantiki hapo ni kwamba nchi itakuwa na umeme mwingi wa ziada. Itaweza kuuza hata nje umeme mwingine. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), unaendelea awamu ya kwanza kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro. Matarajio ni kupitisha treni za umeme. Stiegler’s Gorge inaielekeza nchi kwenye umeme unaokidhi mahitaji.

Tuuhoji uhakika

Pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake njema pamoja na uthubutu wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu, ukizingatia kuwa Stiegler’s Gorge ni mradi ambao upo kwenye mipango ya Serikali tangu miongo minne iliyopita.

Novemba mwaka jana, wakati Bunge lilipokuwa kwenye mjadala wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017-2018, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye aliikosoa Serikali kwa uamuzi wake wa kutoishirikisha sekta binafsi katika miradi inayoweza kujiendesha kibiashara.

Alikosoa utaratibu wa Serikali kujenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani, wakati kiuhalisia inakopa na kuipa nchi mzigo mkubwa wa madeni. Nape alisema, kuishirikisha sekta binafsi kuna nafuu kubwa kuliko kuendelea kukopa, kitu ambacho alionya kwamba kitakuja kusababisha athari kubwa kwa nchi.

Jambo la kwanza Nape alisema kuwa Serikali inakopa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mikubwa ambayo ukamilikaji wake unachukua muda mrefu, wakati mikopo husika marejesho yake yanafanyika ndani ya muda mfupi. Kutokana na hali hiyo, alitahadharisha kwamba marejesho yataathiri miradi mingine.

Nape alisema kwa vile miradi itachelewa kukamilika, wakati wa marejesho ya mikopo, itabidi kuchukua fedha kwenye miradi ya huduma kama elimu, afya na kadhalika ili kuwalipa wadeni wa nchi. Katika hili Nape alisema anatilia shaka uzalendo wa wachumi ambao wanamshauri Rais Magufuli.

Tahadhari ya Nape

Upande wa pili, Nape alionya kuwa nchi inapiga hatua kwenda kuwa isiyokopesheka ikiwa itakopa kwa ajili ya miradi miwili tu; wa kwanza ni ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) dola 15 bilioni (Sh33.8 trilioni) na wa ufuaji umeme wa Stiegler’s Gorge megawati 2,100 dola 5 bilioni (Sh11.27 trilioni), jumla dola 20 bilioni (Sh45 trilioni).

Nape alisema taarifa za mpango zinaeleza Deni la Taifa lilifikia dola 26 bilioni (Sh58.6 bilioni) sawa na asilimia 32 ya uhimilivu wa deni. Kwamba ili Tanzania ifikie kikomo cha kukopeshwa, deni lake linapaswa kufikia dola 45 bilioni (Sh101.4 trilioni).

Kutokana na hoja hiyo ya Nape, endapo Serikali itaongeza mkopo kwa miradi miwili tu ya Standard Gauge na Stiegler’s Gorge, deni lingefikia dola 46 bilioni (Sh103.7 trilioni), yaani ongezeko la Sh2.3 trilioni kutoka kwenye kiwango chake cha mwisho cha kukopa.

Hata hivyo, hesabu ya Nape kuwa Stiegler’s Gorge ingegharimu Shi11 Trilioni haipo sawa, kwani wakati wa utiliaji saini kati ya Tanesco na Arab Contractors, Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, alisema kuwa mradi gharama yake jumla ni Sh8 Trilioni.

Nape pia alikosoa kutelekezwa kwa mradi wa gesi ambao uligharimu maisha ya watu kuhamishwa makazi. Mipango ya awali ilikuwa nchi ije kuwa umeme wa gesi. Hata hivyo, Rais Magufuli mwaka huu alizungumzia sababu ya kupuuza mradi wa gesi, kwamba ulishaandaliwa mazingira ya kifisadi.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amekuwa akipigia kelele mkataba wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge, kuwa unaminya fursa zilizopo nchi. Nchi ina chuma, makaa ya mawe na kila kitu chenye kutumika kujenga reli, lakini mkataba uliopo unafanya Waturuki waliopewa zabuni watoe malighafi nje ya nchi, badala ya kuwabana kutumia zilizopo nchini.

Wadau wa mazingira wanadai Stiegler’s Gorge ni hatari kwa mazingira, lakini wanapuuzwa. Haya ndiyo mambo ya kutazama kipindi hiki furaha ikiwa imetanda. Je, kila kitu kinakwenda safi au upo wakati majuto yataibuka. Hoja za akina Nape na Zitto hazina maana au utafika wakati itakuwa majuto mjukuu? Watu wa mazingira je? Vema kusikiliza hoja za kila upande, kwani hiyo ndiyo mantiki ya kujenga nchi moja.

Chanzo:Mwananchi
     
Mada fikirishi na uandishi mzuri sana
 
Ndugu yangu nataka kukupa elimu tuu angalia tazara, ni mradi ulikuwa mkubwa juu ya uwezo wa ncni mbili , zambia na tanzania, leo unasua sua kwa sababu hatukuwa na uwezo wakuumiliki na kuutunza, ukienda vituo vya tazara, au workshop ya maghula, au hata dar workshop utalia, hakuna kitu, sababu kubwa ni kuwa chumi zetu ni ndogo hatuna uwezo kuhimili repair and maintenance ya miradi mikubwa, nenda national stadium mpya watu wamevunja machoo, umeme bulb haziwaki etc etc, kitu gani kinChokupa tumai, kuwa SGR itakuwa tofauti? Tofauti iliyotakiwa na endelezo la uchumi watu wawe na ajira, wakulima waweze kupata kipato kikubwa etc etc, tunavyofanya ni kinyume kabisa actually mnatusomesha halafu nyie mnatumia primitive thinking kuendesha nchi hatuendi
Mkuu ingekua vizuri ungefanya stadi ya reli ya kati ukaangalia utendaji kazi wao. Usipende kukata tamaa kabla hujajaribu...suala la ustaarabu ni changamoto kwetu Watanzania ila sio kila kitu tunaharibu angalia treni ya Deluxe hii inayotoka Dar hadi Kigoma iko vizuri na inafanyiwa maintainance vizur. Matatizo ya TAZARA yasitumike kama study ya Central corridor railway.. Reli ya kati inahudumia watu wengi na maintainance yake ni ya kiwango cha juu. Bado nna imani tunaweza
Unatumia makwapa kufikiri?
Sina uhakika kama kwapa linaweza kufikiri labda lako
 
Tufunge mkanda ndg zangu watanzania... tupo katika safari ya kuelekea Uchumi wa kati...! mataifa mengi haya pendi kutuona tukielekea huko hata wakenya hawa pendi hahahahahaaa...

hasa baada ya kutamka tuna pesa... tuna jenga kwa pesa zetu wenyewe... wana tuonea wivu sana...

hivi karibuni tutaacha matumizi ya haya maneno tuna... kwa pesa zetu wenyewe
Bwawa la Ethiopia limeongezewa muda 4yrs zaidi baada ya miaka 7 kushindwa kukamilika kampuni hii ya Arab ilijenga bwawa huko kwao Misri kwa miaka 10 Nawaza tu kama 36months zinatosha
 
Mkuu ingekua vizuri ungefanya stadi ya reli ya kati ukaangalia utendaji kazi wao. Usipende kukata tamaa kabla hujajaribu...suala la ustaarabu ni changamoto kwetu Watanzania ila sio kila kitu tunaharibu angalia treni ya Deluxe hii inayotoka Dar hadi Kigoma iko vizuri na inafanyiwa maintainance vizur. Matatizo ya TAZARA yasitumike kama study ya Central corridor railway.. Reli ya kati inahudumia watu wengi na maintainance yake ni ya kiwango cha juu. Bado nna imani tunaweza

Sina uhakika kama kwapa linaweza kufikiri labda lako
Mkuu jamaa ana point ya msingi TRL ni shirika ambalo kuanzia mabehewa mpaka vichwa vyake ni teknolojia za zamani kingine tumerithi toka kwa wakoloni. so si sahihi sana kulinganisha TRL na hii treni ya umeme, kingine tazara ilikuwa ni mradi mkubwa sana ulioanza from scratch kama ambavyo itakuwa hiyo treni ya umeme so nadhani kuna usahihi fulani kulinganisha. Kuna ukweli kuwa watz tunashindwa kuendeleza vitu vyetu vikawa katika ufanisi unaokubalika kimataifa mf mdogo tu ATCL imewahi kuchelewesha safari kisa inamsubiri waziri! na sasa ina kashfa ya ufaulisha ticket!! yaani full uswahili, mabasi ya Mwendokasi si umeona changamoto zake zilivyo kubwa!! Kwa anayejua TAZARA kweli inasikitisha sanaaaaaaaa. Hili shirika lilikuwa na best ever railway workshop ambapo walikuwa wanachonga mpaka matairi ya traini, leo hii imebaki historia!! shirika lipo busy kuuza ardhi yake!!! shirika lina madeni ya kutisha kwa wastaafu wake mpaka wazabuni wa huduma na bidhaa, mishahara kuna wakati inatoka tarehe 90! Sasa ndipo inapaswa serikali ijiulize imeshindwa changamoto hizi je imejiandaa na changamoto za treni ya kisasa ya umeme!! kumbuka kenya karibia itatwaliwa na mdeni wake ambaye ni china!!!!
 
Back
Top Bottom