Tukikamilisha miradi ya Stiegler's Gorge na SGR pekee. Ona habari hii na fanya hesabu kuhusu sisi kuendelea kukopesheka na utathimini tunaelekea wapi

Mkuu jamaa ana point ya msingi TRL ni shirika ambalo kuanzia mabehewa mpaka vichwa vyake ni teknolojia za zamani kingine tumerithi toka kwa wakoloni. so si sahihi sana kulinganisha TRL na hii treni ya umeme, kingine tazara ilikuwa ni mradi mkubwa sana ulioanza from scratch kama ambavyo itakuwa hiyo treni ya umeme so nadhani kuna usahihi fulani kulinganisha. Kuna ukweli kuwa watz tunashindwa kuendeleza vitu vyetu vikawa katika ufanisi unaokubalika kimataifa mf mdogo tu ATCL imewahi kuchelewesha safari kisa inamsubiri waziri! na sasa ina kashfa ya ufaulisha ticket!! yaani full uswahili, mabasi ya Mwendokasi si umeona changamoto zake zilivyo kubwa!! Kwa anayejua TAZARA kweli inasikitisha sanaaaaaaaa. Hili shirika lilikuwa na best ever railway workshop ambapo walikuwa wanachonga mpaka matairi ya traini, leo hii imebaki historia!! shirika lipo busy kuuza ardhi yake!!! shirika lina madeni ya kutisha kwa wastaafu wake mpaka wazabuni wa huduma na bidhaa, mishahara kuna wakati inatoka tarehe 90! Sasa ndipo inapaswa serikali ijiulize imeshindwa changamoto hizi je imejiandaa na changamoto za treni ya kisasa ya umeme!! kumbuka kenya karibia itatwaliwa na mdeni wake ambaye ni china!!!!

Shida kubwa ya hii miradi mikubwa ni capacity ya nchi kuiendesha, kikweli kuwapata proper managers watanzania wanoweza na wanexperience ya hivyo sio kuwa hawapo, bali wengi wapo nje ya nchi, kikwete alianza kuwaita mmoja mmoja kwa uwezo wake, akiangia jiwe akawaperusha mmoja baada ya wengine, wamebaki wale ambao kutwaa wanapokea maagizo, ubunifu zero na kutwa kusifu juhudi, otherwise uwezo zero
 
Jumatano iliyopita, Kampuni ya Arab Contractors ya Misri na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), walisaini mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme kwenye Mto Rufiji, maarufu kama Stiegler’s Gorge. Utilianaji huo wa saini ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, walikuwa mashuhuda wa utilianaji huo wa saini. Kukamilika kwa Stiegler’s Gorge kutaifanya Tanzania kuwa na umeme mkubwa, wenye kutosheleza nchi na zaidi tena kwa bei nafuu.

Mradi wa Kinyerezi ulipokamilika mwaka juzi, taarifa ya Tanesco ilieleza kuwa mahitaji ya umeme yalitimia kwa asimilia 100. Ilielezwa kwamba Kinyerezi inazalisha megawati 150, hivyo kufikisha megawati 1,500 ambazo ndizo mahitaji ya nchi kwa sasa.

Hata hivyo, hali halisi ya umeme kwa sasa, jinsi umeme unavyokatika mara kwa mara, huku nishati hiyo ikionekana kuwa si ya uhakika, ni dhahiri kuwa kiwango cha umeme kilichopo hakitoshelezi. Ama uwezo wa mitambo ya ufuaji ni mdogo au njia za upitishaji wa umeme zimezidiwa.

Stiegler’s Gorge ikikamilika, itaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2,100. Kwa hesabu ya Tanesco mwaka juzi kuwa mahitaji ya nchi ni megawatt 1,500, maana yake, mradi huo ukikamilika, itawezekana hata kuzima mitambo mingine yote na kutumia umeme wa Stiegler’s Gorge na mwingine utabaki.

Mantiki hapo ni kwamba nchi itakuwa na umeme mwingi wa ziada. Itaweza kuuza hata nje umeme mwingine. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), unaendelea awamu ya kwanza kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro. Matarajio ni kupitisha treni za umeme. Stiegler’s Gorge inaielekeza nchi kwenye umeme unaokidhi mahitaji.

Tuuhoji uhakika

Pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake njema pamoja na uthubutu wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu, ukizingatia kuwa Stiegler’s Gorge ni mradi ambao upo kwenye mipango ya Serikali tangu miongo minne iliyopita.

Novemba mwaka jana, wakati Bunge lilipokuwa kwenye mjadala wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017-2018, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye aliikosoa Serikali kwa uamuzi wake wa kutoishirikisha sekta binafsi katika miradi inayoweza kujiendesha kibiashara.

Alikosoa utaratibu wa Serikali kujenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani, wakati kiuhalisia inakopa na kuipa nchi mzigo mkubwa wa madeni. Nape alisema, kuishirikisha sekta binafsi kuna nafuu kubwa kuliko kuendelea kukopa, kitu ambacho alionya kwamba kitakuja kusababisha athari kubwa kwa nchi.

Jambo la kwanza Nape alisema kuwa Serikali inakopa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mikubwa ambayo ukamilikaji wake unachukua muda mrefu, wakati mikopo husika marejesho yake yanafanyika ndani ya muda mfupi. Kutokana na hali hiyo, alitahadharisha kwamba marejesho yataathiri miradi mingine.

Nape alisema kwa vile miradi itachelewa kukamilika, wakati wa marejesho ya mikopo, itabidi kuchukua fedha kwenye miradi ya huduma kama elimu, afya na kadhalika ili kuwalipa wadeni wa nchi. Katika hili Nape alisema anatilia shaka uzalendo wa wachumi ambao wanamshauri Rais Magufuli.

Tahadhari ya Nape

Upande wa pili, Nape alionya kuwa nchi inapiga hatua kwenda kuwa isiyokopesheka ikiwa itakopa kwa ajili ya miradi miwili tu; wa kwanza ni ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) dola 15 bilioni (Sh33.8 trilioni) na wa ufuaji umeme wa Stiegler’s Gorge megawati 2,100 dola 5 bilioni (Sh11.27 trilioni), jumla dola 20 bilioni (Sh45 trilioni).

Nape alisema taarifa za mpango zinaeleza Deni la Taifa lilifikia dola 26 bilioni (Sh58.6 bilioni) sawa na asilimia 32 ya uhimilivu wa deni. Kwamba ili Tanzania ifikie kikomo cha kukopeshwa, deni lake linapaswa kufikia dola 45 bilioni (Sh101.4 trilioni).

Kutokana na hoja hiyo ya Nape, endapo Serikali itaongeza mkopo kwa miradi miwili tu ya Standard Gauge na Stiegler’s Gorge, deni lingefikia dola 46 bilioni (Sh103.7 trilioni), yaani ongezeko la Sh2.3 trilioni kutoka kwenye kiwango chake cha mwisho cha kukopa.

Hata hivyo, hesabu ya Nape kuwa Stiegler’s Gorge ingegharimu Shi11 Trilioni haipo sawa, kwani wakati wa utiliaji saini kati ya Tanesco na Arab Contractors, Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, alisema kuwa mradi gharama yake jumla ni Sh8 Trilioni.

Nape pia alikosoa kutelekezwa kwa mradi wa gesi ambao uligharimu maisha ya watu kuhamishwa makazi. Mipango ya awali ilikuwa nchi ije kuwa umeme wa gesi. Hata hivyo, Rais Magufuli mwaka huu alizungumzia sababu ya kupuuza mradi wa gesi, kwamba ulishaandaliwa mazingira ya kifisadi.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amekuwa akipigia kelele mkataba wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge, kuwa unaminya fursa zilizopo nchi. Nchi ina chuma, makaa ya mawe na kila kitu chenye kutumika kujenga reli, lakini mkataba uliopo unafanya Waturuki waliopewa zabuni watoe malighafi nje ya nchi, badala ya kuwabana kutumia zilizopo nchini.

Wadau wa mazingira wanadai Stiegler’s Gorge ni hatari kwa mazingira, lakini wanapuuzwa. Haya ndiyo mambo ya kutazama kipindi hiki furaha ikiwa imetanda. Je, kila kitu kinakwenda safi au upo wakati majuto yataibuka. Hoja za akina Nape na Zitto hazina maana au utafika wakati itakuwa majuto mjukuu? Watu wa mazingira je? Vema kusikiliza hoja za kila upande, kwani hiyo ndiyo mantiki ya kujenga nchi moja.

Chanzo:Mwananchi
     
Uelewa wako wa uchumi ni zero!! Wewe ujuzi wako ni propaganda za kisiasa tu.
 
Shida kubwa ya hii miradi mikubwa ni capacity ya nchi kuiendesha, kikweli kuwapata proper managers watanzania wanoweza na wanexperience ya hivyo sio kuwa hawapo, bali wengi wapo nje ya nchi, kikwete alianza kuwaita mmoja mmoja kwa uwezo wake, akiangia jiwe akawaperusha mmoja baada ya wengine, wamebaki wale ambao kutwaa wanapokea maagizo, ubunifu zero na kutwa kusifu juhudi, otherwise uwezo zero
Tupo sisi wazalendo achana na hao waliathirika na uzungu!
 
Uzalendo bila skills na capacity , mimi kipimo ambacho hata mimi nilipitia na kwa mfano , miaka ya nyuma niliomba kazi saudia, mimi mkristo mtanzania, nikabomoa miaka mitano nimekaa kenya mitatu, sasa kama capacity ya wewe kununua gazeti kama la economist na ukaapply kazi na ukapata, nitakuvulia kofia, i promise you 99.9% ya watanzania wasomi wanaishia kuomba kazi tamisemi au wakizidi southern sun or the like, wachache utawakuta WB, IMF na hawana hata hamu ya kuja huku
 
Pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake njema pamoja na uthubutu wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu, ukizingatia kuwa Stiegler’s Gorge ni mradi ambao upo kwenye mipango ya Serikali tangu miongo minne iliyopita.
Comrade umekomaa sasa.. Hongera kwa kupevuka..usiwe na shaka tutafika salama
 
Nimeshau capacity ya kuandika na kuongea kiingereza, hii inaanzia juu sana, hahaha, ukimsikiliza graduate wa tanzania, au muambia aandika report utajinyea
 
Jumatano iliyopita, Kampuni ya Arab Contractors ya Misri na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), walisaini mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme kwenye Mto Rufiji, maarufu kama Stiegler’s Gorge. Utilianaji huo wa saini ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, walikuwa mashuhuda wa utilianaji huo wa saini. Kukamilika kwa Stiegler’s Gorge kutaifanya Tanzania kuwa na umeme mkubwa, wenye kutosheleza nchi na zaidi tena kwa bei nafuu.

Mradi wa Kinyerezi ulipokamilika mwaka juzi, taarifa ya Tanesco ilieleza kuwa mahitaji ya umeme yalitimia kwa asimilia 100. Ilielezwa kwamba Kinyerezi inazalisha megawati 150, hivyo kufikisha megawati 1,500 ambazo ndizo mahitaji ya nchi kwa sasa.

Hata hivyo, hali halisi ya umeme kwa sasa, jinsi umeme unavyokatika mara kwa mara, huku nishati hiyo ikionekana kuwa si ya uhakika, ni dhahiri kuwa kiwango cha umeme kilichopo hakitoshelezi. Ama uwezo wa mitambo ya ufuaji ni mdogo au njia za upitishaji wa umeme zimezidiwa.

Stiegler’s Gorge ikikamilika, itaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2,100. Kwa hesabu ya Tanesco mwaka juzi kuwa mahitaji ya nchi ni megawatt 1,500, maana yake, mradi huo ukikamilika, itawezekana hata kuzima mitambo mingine yote na kutumia umeme wa Stiegler’s Gorge na mwingine utabaki.

Mantiki hapo ni kwamba nchi itakuwa na umeme mwingi wa ziada. Itaweza kuuza hata nje umeme mwingine. Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), unaendelea awamu ya kwanza kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro. Matarajio ni kupitisha treni za umeme. Stiegler’s Gorge inaielekeza nchi kwenye umeme unaokidhi mahitaji.

Tuuhoji uhakika

Pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake njema pamoja na uthubutu wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu, ukizingatia kuwa Stiegler’s Gorge ni mradi ambao upo kwenye mipango ya Serikali tangu miongo minne iliyopita.

Novemba mwaka jana, wakati Bunge lilipokuwa kwenye mjadala wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017-2018, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye aliikosoa Serikali kwa uamuzi wake wa kutoishirikisha sekta binafsi katika miradi inayoweza kujiendesha kibiashara.

Alikosoa utaratibu wa Serikali kujenga miradi mikubwa kwa fedha za ndani, wakati kiuhalisia inakopa na kuipa nchi mzigo mkubwa wa madeni. Nape alisema, kuishirikisha sekta binafsi kuna nafuu kubwa kuliko kuendelea kukopa, kitu ambacho alionya kwamba kitakuja kusababisha athari kubwa kwa nchi.

Jambo la kwanza Nape alisema kuwa Serikali inakopa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mikubwa ambayo ukamilikaji wake unachukua muda mrefu, wakati mikopo husika marejesho yake yanafanyika ndani ya muda mfupi. Kutokana na hali hiyo, alitahadharisha kwamba marejesho yataathiri miradi mingine.

Nape alisema kwa vile miradi itachelewa kukamilika, wakati wa marejesho ya mikopo, itabidi kuchukua fedha kwenye miradi ya huduma kama elimu, afya na kadhalika ili kuwalipa wadeni wa nchi. Katika hili Nape alisema anatilia shaka uzalendo wa wachumi ambao wanamshauri Rais Magufuli.

Tahadhari ya Nape

Upande wa pili, Nape alionya kuwa nchi inapiga hatua kwenda kuwa isiyokopesheka ikiwa itakopa kwa ajili ya miradi miwili tu; wa kwanza ni ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) dola 15 bilioni (Sh33.8 trilioni) na wa ufuaji umeme wa Stiegler’s Gorge megawati 2,100 dola 5 bilioni (Sh11.27 trilioni), jumla dola 20 bilioni (Sh45 trilioni).

Nape alisema taarifa za mpango zinaeleza Deni la Taifa lilifikia dola 26 bilioni (Sh58.6 bilioni) sawa na asilimia 32 ya uhimilivu wa deni. Kwamba ili Tanzania ifikie kikomo cha kukopeshwa, deni lake linapaswa kufikia dola 45 bilioni (Sh101.4 trilioni).

Kutokana na hoja hiyo ya Nape, endapo Serikali itaongeza mkopo kwa miradi miwili tu ya Standard Gauge na Stiegler’s Gorge, deni lingefikia dola 46 bilioni (Sh103.7 trilioni), yaani ongezeko la Sh2.3 trilioni kutoka kwenye kiwango chake cha mwisho cha kukopa.

Hata hivyo, hesabu ya Nape kuwa Stiegler’s Gorge ingegharimu Shi11 Trilioni haipo sawa, kwani wakati wa utiliaji saini kati ya Tanesco na Arab Contractors, Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, alisema kuwa mradi gharama yake jumla ni Sh8 Trilioni.

Nape pia alikosoa kutelekezwa kwa mradi wa gesi ambao uligharimu maisha ya watu kuhamishwa makazi. Mipango ya awali ilikuwa nchi ije kuwa umeme wa gesi. Hata hivyo, Rais Magufuli mwaka huu alizungumzia sababu ya kupuuza mradi wa gesi, kwamba ulishaandaliwa mazingira ya kifisadi.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amekuwa akipigia kelele mkataba wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge, kuwa unaminya fursa zilizopo nchi. Nchi ina chuma, makaa ya mawe na kila kitu chenye kutumika kujenga reli, lakini mkataba uliopo unafanya Waturuki waliopewa zabuni watoe malighafi nje ya nchi, badala ya kuwabana kutumia zilizopo nchini.

Wadau wa mazingira wanadai Stiegler’s Gorge ni hatari kwa mazingira, lakini wanapuuzwa. Haya ndiyo mambo ya kutazama kipindi hiki furaha ikiwa imetanda. Je, kila kitu kinakwenda safi au upo wakati majuto yataibuka. Hoja za akina Nape na Zitto hazina maana au utafika wakati itakuwa majuto mjukuu? Watu wa mazingira je? Vema kusikiliza hoja za kila upande, kwani hiyo ndiyo mantiki ya kujenga nchi moja.

Chanzo:Mwananchi
     
Mkuu kiuhalisia gazeti la mwananchi na citizen NI magazeti ya Kenya ambao ni wapinzani wetu kiuchumi ambao hawaitakii Tanzania mema.
Wao wanajua ya kuwa usitawi wa Tanzania ni kifo Cha Kenya kiuchumi.
Watafanya watakavyofanya ili kutuvuruga Watanzania
Kenya wana SGR.mpya walijenga kwa ajili ya soko la Africa mashariki.
Tanzania tunajenga SGR kwa ajili ya soko Africa mashariki,kwa hesabu ndogo tu Kenya unadhani wanafurahi?
Ukizingatia kwamba Tanzania kwenda Uganda,Rwanda,Burundi na DRC ni karibu kuliko Mombasa Kenya?
Tukiwa Wazalendo wa kweli,Tanzania itakuwa giant kiuchumi in the next twenty years kwa ukanda was Africa Mashariki,Wakenya wanalijua hilo,unafikiri wanafurahi?
TAFAKARI
 
Hapa unamtukana Salary Slip Au Nani? Hivi kwanini hamsomagi mabandiko mnaishia kuponda tu hata bila kusoma? you guys grow up and argue with reason atleast.

Hebu kasome hilo Bandiko lote urudi kusoma jibu lako
Nimesoma bandiko lake lote limejaa nukuu za Nape, Zitto nk na akamalizia na poor conclusion pia huyu jamaa namjua hana la maana ni mpingaji tu na hana chochote cha maana alishatueleza humu kuwa Dreamliner haitakuja ikaja sasa unataka awa reference kwa lipi la maana may be kwako!
 
Mzee tuliza mapepe basi. hilo bandiko ulilonukuu halina wazo lolote la mleta mada nenda kalisome tena. hiyo conclusion unayosema labda kwenye bandiko jingine
 
  • Thanks
Reactions: etb
Kama hesabu yangu iko sahihi, naona ni kama tutakuwa tumebakiza trilioni moja tu kabla ya kufikia ukomo wa kukopa iwapo tutaenda hivi tunavyoenda(tutaamua kuikamilisha yote) unless tunajitaahidI kulipa haya madeni na hii miradi tukaendanayo taratibu(kwa hatua) hasa huo wa SGR.
kwa ufahamu wako ukomo wa kukopa kwaTanzania ni dola bilioni ngapi
Ili nchi ifikie hali ya kutokopesheka ni hali gani inabidi itokee?
Usifungue mada kwa vijihabari vya kuokoteza,naomba majibu ya kiyakinifu
 
Tufunge mkanda ndg zangu watanzania... tupo katika safari ya kuelekea Uchumi wa kati...! mataifa mengi haya pendi kutuona tukielekea huko hata wakenya hawa pendi hahahahahaaa...

hasa baada ya kutamka tuna pesa... tuna jenga kwa pesa zetu wenyewe... wana tuonea wivu sana...

hivi karibuni tutaacha matumizi ya haya maneno tuna... kwa pesa zetu wenyewe
Embu toa u.j.i.n.g.a wako upeleke chooni
 
Binafsi nimeshafikia Hatua Mbaya sana Kifikra, ninasema hapa kwa Uwazi bila kumumunya maneno. Simwamini Mtu wala Serikali katika haya. Tuliaminishwa Gas ya Mtwara ingekuwa Tiba kwa nchi na nyingine tungeuza nje lakini cha kustaajabisha, Kiwanda cha Dangote tu wameshindwa kukilisha kwa umeme wa gesi. Limekuja hili la Stig nini sijui linamaliziwaje huko mbele, tunaambiwa ndio Mwarobaini. Wacha nibaki kuwa Tomaso.
 
Mkuu jamaa ana point ya msingi TRL ni shirika ambalo kuanzia mabehewa mpaka vichwa vyake ni teknolojia za zamani kingine tumerithi toka kwa wakoloni. so si sahihi sana kulinganisha TRL na hii treni ya umeme, kingine tazara ilikuwa ni mradi mkubwa sana ulioanza from scratch kama ambavyo itakuwa hiyo treni ya umeme so nadhani kuna usahihi fulani kulinganisha. Kuna ukweli kuwa watz tunashindwa kuendeleza vitu vyetu vikawa katika ufanisi unaokubalika kimataifa mf mdogo tu ATCL imewahi kuchelewesha safari kisa inamsubiri waziri! na sasa ina kashfa ya ufaulisha ticket!! yaani full uswahili, mabasi ya Mwendokasi si umeona changamoto zake zilivyo kubwa!! Kwa anayejua TAZARA kweli inasikitisha sanaaaaaaaa. Hili shirika lilikuwa na best ever railway workshop ambapo walikuwa wanachonga mpaka matairi ya traini, leo hii imebaki historia!! shirika lipo busy kuuza ardhi yake!!! shirika lina madeni ya kutisha kwa wastaafu wake mpaka wazabuni wa huduma na bidhaa, mishahara kuna wakati inatoka tarehe 90! Sasa ndipo inapaswa serikali ijiulize imeshindwa changamoto hizi je imejiandaa na changamoto za treni ya kisasa ya umeme!! kumbuka kenya karibia itatwaliwa na mdeni wake ambaye ni china!!!!
Wanasiasa na wanaonufaika na posho za miradi hiyo hawawezi kukuelewa kabisa. Ila kwa kuchukulia mfano wa tazara tu inasikitisha sana na kunalakujifunza kwenye miradi hii kabla ya kuingia kwenye madeni mengine.
 
Back
Top Bottom