Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa

Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa

Mbunge Msukuma sasa hivi anavyokejeli wenye elimu ni hatari. Yuko kama mganga wa kienyeji anayeweza kukulisha kinyesi, nawe ukimwamini utapata kila aina ya magonjwa mwilini.

Kimsingi ugonjwa utakupata sababu yz UJINGA!

Ndivyo alivyo huyu mwenzetu, fundi wa kuongea na kughilibu akili za watu wenye elimu kama yake ndogo.

Naweza kukubali Prof Muhongo si ajabu alikosea katika comments zake za gesi, lakini hatujamsikiliza argument zake au alimaanisha nini.

Mtu wa darasa la saba, mwenye kiburi ya pesa, tukimnyanyua kama ndiye one of the standard beares wa hatma ya nchi , tumepotea.
Akisaidiwa na wengine kama kina Kibajaji ati ndio wasemaji wa mustakabali wa Taifa -tumekwisha!

Tukumbuke mfano wa mbwa koko , wakiwa wengi kila mmoja ananyofoa mnofu.
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni....
Hoja ya Muhongo haina tatizo, tatizo ni hilo kusanyiko la Walafi hapo Dodoma ambalo Watanzania mmedanganyika na kuliita Bunge. Ni kusanyiko la Wapiga deal ambao wakisimama kuongea unaona kama kuna wanachotetea juu ya nchi.

Hawana lolote zaidi ya maslahi binafsi na ndo maana wanasutana kwamba Magufuli aliwapeleka bungeni kwa nguvu zake na si kwa uchaguzi,wa Wananchi. Ni kikao cha Wachumia tumbo ambacho hata kisingekuwepo bado nchi ingekwenda.

Hayo wanayoongea hata yakipuuzwa yote bado bajeti itapita na maisha yataendelea. Usimsikilize Msukuma wa Geita wala Mgogo wa Mtera, hawa wote ni kundi la wezi waliojihalalisha kutokana na ujinga wa Watanzania.
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni.....
Tatizo wasomi wengi wameamua kujidhalilisha wenyewe kwa kutumiwa na wanasiasa. Mwangalie Kabudi, Kabudi yule wa katiba na huyu Ni tofauti kabisa. Huyu anamuabudu Magu, anasema alimuokota jalalani..sasa sijui chuo kikuu cha Dar es Salaam ndo jalalani? Hata Prof Assad alisema hili.. corruption of mind
 
Hoja ya Muhongo haina tatizo, tatizo ni hilo kusanyiko la Walafi hapo Dodoma ambalo Watanzania mmedanganyika na kuliita Bunge. Ni kusanyiko la Wapiga deal ambao wakisimama kuongea unaona kama kuna wanachotetea juu ya nchi...
Spika anaongelea suala la bandari ya Bagamoyo baada ya JPM kufariki, ina maana kama angeishi basi tusingekuja kusikia hili suala likiibuliwa tena!.

Wanasiasa ni wanafiki wa viwango vya kimataifa.
 
Anachosahau Musukuma ni kuwa moja ya faida ya elimu ni pamoja na kutokushambulia personality. Anachotakiwa kufanya ni kujikita kwenye hoja na kuzitetea kwa ufahamu wake wote....na kwa namna hiyo atajikuta anaheshimisha kiwango cha Elimu yake na Wenzake wa kundi hilo.

Moja ya sifa za asiye na Elimu ni kupenda zogo na malumbano.
 
Msukuma ni mgonjwa wa akili, kutoelewa kwake hoja ya Prop Mhongo ndiko kulikosababisha personal attack zake..

Speaker naye ni wakuaumiwa kwa kuruhusu bunge kufanya personal attacks na sio kujikita kwenye hoja. Speaker ndio msimamizi wa hii mijadala sasa kama anashindwa kusimamia na kuwa mshabiki kwa maslahi yake binafsi mbeleni huko tutapata shida....
Trust me,tunaenda kushuhudia wimbi kubwa la wasomi wazuri na wazoefu wakikaa kimya na kuwaachia la Saba na wafanyabiashara "dimba" Mkuu ukiona bunge linaitwa DIMBA Kama alivyosema Lusinde,Kuna shida kubwa sana sana sana.
Rejea kauli ya spika kwa Kimei utajua there still a stoke of nonsense to be delivered!!!
 
shida inaanzia pale maprofesa wanapoanza kuchafua wenzao kisa eti wao wamesoma, ndio mana wanageuziwa kibao cha hasira

NOTE - kila mwanadam awe msomi, mdini, au hajasoma anakipande chake cha ujinga flani kichwani mwake kuna siku kinalipuka especially kunapotokea maslahi
 
Gas ya Mtwara siyo yakwetu bado turudie huu upuuzi tukimaliza umeme wa maji tutaenda kwenye gas tena kwa pesa zetu za ndani.
Magufuli alipenda sana nchi yake. Hilo halina ubishi. Alipoona mikataba ya uchimbaji wa gas kwamba ile gas wawekezaji walishapewa 70 asilimia, ndipo akaona bora tuanze na umeme wa maji maana sijui kama duniani kuna kuuza maji kwa wawekezaji. Kwa hiyo tutapata 2100MW pale Rufiji. Baada ya hapo tutaongeza si chini ya 1000 MW kwenye moto mingine.

Baada ya hapo ndipo tutaanza umeme wa gas . Maana siku Tanzania itakapokuwa na mahitaji ya MW 10,000 kwa vyovyote tutaangalia na vyanzo vingine. Kosa la Profesa Muhongo ni kutaka kutuaminisha kuwa umeme wa gas PEKE yake ndio unafaa. Hivi Profesa ana imani kuwa inahitaji kuwa na phd ndie ujue abc za gharama na vyanzo vya umeme .

Hapana anakosea kwa fikra hiyo. Ni academic arrogance ambayo ni maumbile ya mtu wala si wasomi wote wanna dharau kama yeye. Lakini Msukuma maybe hana uhalali wa kudharau phd za watu eti hazina faida kea jamii. Hao ndio wanaoongoza mustakabali wa ulimwengu hii. Kwanza inakera kila wakati mtu wa darasa la saba kila akisimama anajitambulisha kea elimu hiyo. Lakini sijasikia ma phd holder wakininasibu nayo kila wanaposimama .

Darasa la saba wanna kutojiamini bungeni kea hiyo wanajitambulisha ili iwe kings wasikoslewe maana ukiwakosoa wanasema wanadharauliwa kwa elimu yao. Wachangie tu kadri ya uslewa wao ambayo mara nyingi ni kusfia serikali ispokuwa mhe. Kishimba PEKE yake anachambua mambo mpaka spika nampa uprofesa wa hekima ya kujua mambo.
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni...
Hapa ku mawili au tuseme matatu.

Mosi, Professor Muhongo tangu tumfahamu, na hata tamko lake la juzi, hajaweza kuturidhisha kama ni Professor kweli. A professor has all-round knowledge of things, he brings new things. Sijui kama huko Geology (husemwa ni miamba, whatever that is) labda ni tofauti lakini huku huku nje ni zero, sifuli. Kumwita darasa la 7 au kumwita mjinga au kusema hafai au yuko halfbaked - zote ni namna moja tu ya kumtambulisha kuwa hafai. Pale unapomtukana mtu huchagui tusi.

Pili, Msukuma siyo Darasa la 7, kwa uelewa wangu wa Wasukuma, iwapo kweli angekuwa hajui Kiswahili. Kama kaamua kupeperusha bendera ya darasa la 7 kwa wapiga kura wake, au kwa nonacademics (that's what he is, otherwise is shrewder and sharper and a good manager than many a professor, at least one of whom is Muhongo). Kwa hiyo si kweli kwamba Musukuma literary anamlinganisha professor na darasa ka 7. Ni hilo hilo la kutochagua tusi.

Tatu, kwa nini Muhongo asijitetee mwenyewe? He does not represent professors, na wala hatujamtuma aseme hydro ni aghali kuliko gas. He was Minister in 2 key functions - madini na nishati - he goofed both. Let him pick his own chestnuts out of the fire, next time atajipima.

Finally, sisi wote ni Darasa la 7, wewe ni darasa la 7, Bashiru ni daras la 7, Halima Mdee ni darasa la 7, Muhongo ni darasa la 7, mimi ni darasa la 8 (enzi zetu hizo!). Kwa hiyo kusema darasa la 7 hakuna nia yoyote ya kunyanyapaa udarasala7. What is the big deal?

Joseph, mishaga Mami, a miyo gasoma seminari jilatini, otherwise mko sawa nao tu.


TATU
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni...
Huyu prof anatungo tata, Viongozi wa kitaifa inatakiwa watunze kauli zao
 
Shida ilianzia pale wasomi walipokubali mambo ya kienyeji yakiwamo ya kupigishwa kupigishwa hadi nyungu huku wao wakiwa wameuchuna.

Wasomi uchwara waliposhindwa kuongea lugha walizopaswa kuzijua kwa usomi wao, ikasemekana ni kukuza kiswahili, hali wao wakiwa wameuchuna tu.

Wasomi waliporuhusu njaa za matumbo yao kufunika akili vichwani kwao kufanana tu na za akina msukuma.

Usaka fursa kwa gharama yoyote umewagharimu sana bandugu hawa.
Haya ndiyo matokeo ya kutotumia taaluma zetu sawa sawa katika maamuzi tunatanguliza ulaji mbele na kusahau taaluma zetu,hapo heshima ya matumizi ya ELIMU YETU inakuwa ndogo sana.
 
Maprofesa wengine mpaka kiingereza tatizo

Maprofesa wameingia mikataba ya kihayawani

Maprofesa maprofesa bora tukae kimya

Ila jomba Kama musukuma kakuchoma hivi ,ukiona makelele ujue limekugusa
Hii ya mikataba nawatetea elimu unatumia kama tools,unaweza itumia kutapeli,kuleta maendeleo kama prof kaingia mkataba mbovu ila wakisomi ujue aliempa kazi alimwelekeza anataka output gani,kwamfano kujenga Corona kubwa unatumia engineer na kubomoa utahitaji engneer lisiletemadhara
 
Swali moja tu ambalo inampasa aliyekejeliwa ajiulize Kwamba, Je amekosea wapi? Akija kujigundua, hatamkasirikia mkejeli wake
 
Magufuli akipenda sana nchi yake. Hilo halina ubishi. Alipoona mikataba ya uchimbaji wa gas kwamba ile gas wawekezaji walishapewa 70 asilimia, ndipo akaona bora tuanze na umeme wa maji maana sijui kama duniani kuna kuuza maji kwa wawekezaji. Kwa hiyo tutapata 2100MW pale Rufiji. Baada ya hapo tutaongeza si chini ya 1000 MW kwenye moto mingine. Baada ya hapo ndipo tutaanza umeme wa gas . Maana siku Tanzania itakapokuwa na mahitaji ya MW 10,000 kwa vyovyote tutaangalia na vyanzo vingine. Kosa la Profesa Muhongo ni kutaka kutuaminisha kuwa umeme wa gas PEKE yake ndio unafaa. Hivi Profesa ana imani kuwa inahitaji kuwa na phd ndie ujue abc za gharama na vyanzo vya umeme . Hapana anakosea kwa fikra hiyo. Ni academic arrogance ambayo ni maumbile ya mtu wala si wasomi wote wanna dharau kama yeye. Lakini Msukuma maybe hana uhalali wa kudharau phd za watu eti hazina faida kea jamii. Hao ndio wanaoongoza mustakabali wa ulimwengu hii. Kwanza inakera kila wakati mtu wa darasa la saba kila akisimama anajitambulisha kea elimu hiyo. Lakini sijasikia ma phd holder wakininasibu nayo kila wanaposimama . Darasa la saba wanna kutojiamini bungeni kea hiyo wanajitambulisha ili iwe kings wasikoslewe maana ukiwakosoa wanasema wanadharauliwa kwa elimu yao. Wachangie tu kadri ya uslewa wao ambayo mara nyingi ni kusfia serikali ispokuwa mhe. Kishimba PEKE yake anachambua mambo mpaka spika nampa uprofesa wa hekima ya kujua mambo.
Napenda sana napokutana na uchambuzi wa kina wa namna hii. Very balanced analysis!

Labda niongezee kwa kusema kwamba dharau za akina Msukuma kuhusiana na maprofesa zina msingi wake. Kusema ukweli kati ya mambo yanayohitaji mapinduzi makubwa nchini ni mfumo wa elimu yetu.

Ukienda leo hii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vikuu vingine vinavyotoa mafunzo ya uzamili na uzamivu (Masters na PhD) na namna wanavyuo wanavyopanda ngazi kufikia ranks za uprofesa utasikitika au kulia kabisa kama unaelewa dhana ya nini maana ya uPhD au uprofesa.

Ukiangalia research topic namna zinavyopatikana, mazingira ya kufanyia research, pre- and post-PhD mentorship, research rigor, financing ya research, evaluation ya research output ili kumqualify mtu kwamba amekidhi sifa za kuwa profesa unaona wazi kabisa kwamba kiwango cha hizi professorial qualifications hakitoshi kukidhi mahitaji ya Tanzania ya karne ya 21. Tunao watu wenye elimu na wana vyeti, hadi kiwango cha PhD lakini maarifa waliyoyapata hayatoshi kutengeneza Tanzania ya ushindani wa karne ya 21 kiuchumi, kiujuzi, kiteknolojia. Elimu bora na maarifa ya kiwango cha juu kabisa vinahitaji uwekezaji si wa kitoto. Serikali haijapata kushauriwa namna gani ifanye uwekezaji wa namna hii, kujenga vyumba vya madarasa si aina ya uwekezaji unaohitajika.

Kwa upande mwingine kupata utajiri wa fedha na mali hauhitaji elimu na maarifa. Kinachotofautisha Tanzania (na nchi nyingi za kiAfrika) na zile zilizotangulia, ni kwamba nchi zilizotangulia zimejifunza kutumia utajiri wa fedha na mali kuwekeza kwenye ujuzi na maarifa. Sisi huku badala ya wenye mali na fedha kuwekeza kwenye elimu na ujuzi ili elimu na utajiri vishirikiane kujenga nchi imara, wenye mali wanaona suala la elimu si kitu. Hii nayo ni laana nyingine inayoitafuna nchi yetu.
 
Professor anaonekana ni 'dalali' kwenye ishu ya umeme wa gesi, akiwa waziri alitumia lugha kali na ya kuuzi kwa wawekezaji wa ndani akina mengi, aliwaita eti matajiri wenye uwezo wa kuwekeza kwenye 'pipi' na sio kwenye gesi. Unajiuliza hao matijiri Wazungu wenye uwezo walianzaje? Walizaliwa matajiri? Pasipo kuthaminiwa na kuaminiwa wangefika pale?

Ukweli ni kua wasomi wa nchi hii wengi wanaendeshwa na wanasiasa au matajiri. Wanaosoma sana ila wanaishia kwenye umasikini hivyo huamua kujiuza wenyewe
 
Hilo ni jambo tofauti, mheshimiwa. Elewa mada. Musukuma, darasa la 7, ndiye hawezi hata kuelewa jinsi ya kupambana na mabeberu. Rais Magufuli alipounda zile timu 2 za madini hakuweka hata mtu 1 anayefanana na Musukuma au Kibajaji. Wote ni wasomi wanaoelewa madini, uchumi, sheria, negotiation, na mifumo ya kodi. Mada ndiyo hiyo; tunawahitaji akina Muhongo kwa kuielewa dunia ya sasa. Ila mimi nawakubali akina Musukuma kwa kutukumbusha tulikotoka zamani na kutuchekesha
Ulisikiliza hoja ya Muhongo mpaka ikapelekea watu kumshambulia alisema umeme wa maji hauna faida kwa haraka ivyo tuachane nao na tujikite katika umeme wa gas ambao ni wa kisasa. Sasa ule umeme wa Rufiji ambao ni pesa zetu za ndani tuufugie popo? Je nchi zilizoendelea hawatumii umeme wa maji? Tukitaka kutumia umeme wa gas kama alivyosema pesa tunayo ya kuchimba gas au ndio yale yale ya Mtwara na Bagamoyo? Mikataba mibovu ya madini ilitungwa na wasomi na kwamanufaa ya Mtanzania maskini na ndio hiyo Magu alituma wataalamu tena wa kuipitia upya.
Magufuli ni Genius mawazo yake yatumike kuijenga nchi.
 
Back
Top Bottom