Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa


leo anapewa mkate wake sawa na alioutoa wanakuja chawa wake na kumtetea.
 
S

Siyo ya kwetu vipi? Mwaga data hapa, si umbeya
Kama umbeya basi aliuleta Hayati Magufuli maana ndio alikua Rais na ndie alietusanua kuhusu gas labda kama ulikua usikilizi hotuba zake.
 
View attachment 1752792

Badala ya chadema sasa kambi rasmi ya upinzani bungeni mnawaona ni kina nani??
WASOMI !

Akina Assad
Akina Muhongo
Akina Kichere
Etc
Hapa sipo kwa ajili ya upinzani madudu tuliyokua tunalalamikia miaka mingi Serikali ilikua ni CCM na wasomi walikuwa wa CCM haohao sishangai kuwaona wakirudi tena hii Dunia bro.
 
Ndo walichokueleza na ukaamini... USISAHAU HAO HAO WALIKUELEZA NDEGE ZETU MWAKA 2018 ZILITENGENEZA FAIDA NA WENGINE WAKAMWAGA NA MAGAWIO SERIKALINI...
Ndio maana Spika kasema lugha za kihasibu sio kila mtu atazielewa niambie shirika la ATCL ambalo lilikufa limefufuliwa kwa shilingi ngapi ili tuweze ku compare na hiyo hasara ya billion 60.
 
Profesa Muhongo yupo sahihi ni vile tumezoea kupiga kelele tuu gesi tunayo tuitumie hiyo hata maji kama tunaweza kuzalisha umeme wake nao unasaidia kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka na mahitaji ya umeme yanaongezeka kila kukicha ina maana mpaka sasa hatujui tunahitaji nini na pia kunatakiwa kuwepo na taasisi imara za kusimamia haya mambo sio maeazo ya mtu mmoja akitoa hata likiwa la hovyo linafanyiwa kazi..
 
Mabeberu mpaka Faida yao irudi ndio inakua ya Watanzania wanyonge vipi unajua mkataba ni wa mda gani?
Beberu yupi? Au na wewe upo lile kundi la wajinga wanaosema JK aliwapa wachina gas yote baada ya Rizwan kushikwa China na madawa ya kulevya? Really!! Mapunda yote yaliyojaa Dar yanasubiri kazi ya kubeba unga, rizwan abebe unga mwenyewe akakamatwe! Kweli Tanzania kuna mazuzu!
 
Ndio maana Spika kasema lugha za kihasibu sio kila mtu atazielewa niambie shirika la ATCL ambalo lilikufa limefufuliwa kwa shilingi ngapi ili tuweze ku compare na hiyo hasara ya billion 60.
Lugha za kihasibu ndio hizo hizo hasara ni hasara na faida ni faida asitake kutoa mpira nje kwa sababu zisizo na mashiko...
 
..waswahili wana msemo, " mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. "

..musukuma na lusinde walipokuwa wakidhalilisha wabunge wa vyama vya upinzani hakuna mwana-ccm aliwakemea.
 
Naomi yeyote anapoamua kufanya mambo yake Kwa kiwango cha Chini kama wa darasa la Saba, adharauliwe tu hamna namna!!

Na kiukweli Elimu zetu zinaposhindwa kabisa kubadiri umaskini wa watu wetu, Acha tuitwe vilaza, Kwa sababu haiwezekani, mtu umewahi kuwa waziri Kwa mfano, lakini ulichokifanya huko licha ya usomi wako, ni vitu vya hovyo, vya kuwakandamiza wananchi,

Na ifike mahali pia kama mtu anataka aheshimiwe, yeye mwenyewe aheshimu wenzake Kwanza, huwezi mtu ukaanza kuwadharau darasa la Saba Kwa sababu tu, Una PhD, haiwezekani

Tutumieni vema Elimu ambayo Mungu ametupa ili tuwakomboe wenzetu na sio kudharauliana
 
Maprofesa wengine mpaka kiingereza tatizo

Maprofesa wameingia mikataba ya kihayawani

Maprofesa maprofesa bora tukae kimya

Ila jomba Kama musukuma kakuchoma hivi ,ukiona makelele ujue limekugusa
Kama profesa kingereza tatizo, kwa hiyo darasa la sana ndie kingereza kitakuwa nafuu? Mapungufu ya msomi, mafanikio(kifedha) ya mbumbumbu mmoja mmoja yasihalalishe kubeza umuhimu wa elimu. Hiyo Mike anayo itumia kupayuka hayo aelewe haikubuniwa, kuendelezwa na kufikia kiwango iliopo na mtu wa elimu kama ya msukuma.
 
Mapro wa kibongo wengi ni michosho tu tuseme ukweli tusioneana haya wametugharimu sana
 
Yeye kuwa tajiri asiye na elimu zaidi ya ile ya darasa la saba sio sifa kama anavyodhani. Wapo watu wengi tu wanaoshindwa kufika popote kimaisha sababu ya elimu zao ndogo.
Elimu kubwa inafundisha kuwa bilionea? au hadi uibe? Yaani unakuta mtu anajisifu kasoma sana alafu hakuna jambo lolote analoletea faida binadamu kuhusu elimu yake...
 
Ndio maana Spika kasema lugha za kihasibu sio kila mtu atazielewa niambie shirika la ATCL ambalo lilikufa limefufuliwa kwa shilingi ngapi ili tuweze ku compare na hiyo hasara ya billion 60.
Numbers never lie.... Yaani wewe ndo unataka kutuambia, lugha ya kihasibu inawea ikageuza ile hasara ya 150B kwa miaka mitano mfululizo iwe faida? ACHA WEHU
 
Hapa sipo kwa ajili ya upinzani madudu tuliyokua tunalalamikia miaka mingi Serikali ilikua ni CCM na wasomi walikuwa wa CCM haohao sishangai kuwaona wakirudi tena hii Dunia bro.
MY POINT IS.... Kwao wao, kila anawapa mawazo mbadala wanamnyooshea vidole... kila anayesema maovu yao wanamnyooshea vidole... WAKAAMUA KUWAONDOA WOTE... sasa wamebaki kunyoosheana vidole wao wenyewe
 
Inshort Ngumbaru wamemtumia Profesa Muhongo kama punching bag lao la kutolea stress zao za ungumbaru wao.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kosa lake ni kuwa mkweli kwenye nchi ya watawala waongowaongo, incompetent!
 
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…